Pole ndugu, usijali utakua sawa. Zipo njia nyingi tu. Kuna technique moja inaitwa replacement, kwa maana ya kutoa kitu na kuweka kingine bora zaidi. Replace muda na nguvu unayoitumia kuwekeza kwenye kufikiria kwa kufanya activities bora zaidi kama mazoezi ya viungo, kusoma vitabu, kuangalia movies, kufanya usafi n.k.
Zaidi socialize, socialize, socialize, jichanganye na watu bro, ukiweza fanya uoe kama bado. Kwa kufanya hivyo hutakuwa na muda wa kuwaza, badala yake utakuwa unafanya ya muhimu zaidi. It will not end over night, ila mdogo mdogo utatoboa freshi tu. Hali unayoipitia nimeipitia pia, naijua nje ndani ndani nje, kwa hiyo nikutie moyo tu kwamba utakua poa usijali kabisa, ila kwa kufanya kwa vitendo hayo niliyoyaelezea.