Yaliyopita si ndwele, tugange yajayo; swali ni kivipi?
1. Rudisha akili yako nyuma, tafakari yaliyopita kwa lengo la kujifunza - lakini usizamie huko huko.
Ndio. Msongo wa mawazo unaweza kuutumia ukusaidie kesho,hata kama una maumivu kiasi gani. Jiulize maswali kama;
- Ni nini hasa kilitokea? Jipe majibu ya kweli (usijidanganye mwenyewe).
- Kilichotokea kinakufanya ujisikiaje? Aibu? Fedheha? Hasira? Wivu? n.k - Ukiweza andika. (mimi huwa naandika kila kitu).
- Unawezaje kutumia tukio hilo/matukio hayo kuji-empower mwenyewe na kutibu hisia zako?
Kwa mfano; Mimi niliwahi kuwa na mafanikio sana kimaisha nikiwa na umri mdogo. Ghafla nikapoteza kila kitu - ilinichukua miaka takribani 8 kukabiliana na msongo wa mawazo. Nilikuwa nawaza vitu kama - Fulani ananichukuliaje? Yule fulani mimi nilimsaidia mbona yeye amenipotezea? Na yule fulani anaeneza habari kwa watu kuwa nimefulia, nimfanyaje? Nitafanyaje ili nirudi kwenye hali yangu yakiuchumi fasta? Au nimerogwa, maana yule fulani alinidokezea kuwa ni muhimu nikawa na kinga!
Utagundua maswali mengi niliyokuwa najiuliza yalikuwa nje ya uwezo wangu; I could do nothing about them. Kwa mfano; Nilipaswa kujua kuwa siwezi kubadili mtazamo wa watu juu yangu bali naweza kubadili namna ninavyo-react endapo watanicheka, watavunja urafiki na mimi n.k. Lakini katika situation kama hiyo huwezi kujua mpaka ukae chini, ukiwa na dhamira ya kutatua hii changamoto - ndipo ujiulize maswali magumu - jipe majibu ya kweli bila kujifariji/ kujidanganya.
Ukishapata majibu, songa mbele - ni rahisi kujua ufanyaje ili kusonga mbele.
2. Express yourself. (Funguka)
Usijizuie kuonesha hisia zako, usijizuie kutema nyongo, usijizuie kutoa yaliyo moyoni - usibaki na vitu moyoni. Mimi nilianza kwa kuwafuata wale niliokuwa naogopa kukutana nao baada ya kufulia. Hii ni mbinu ya kisaikolojia - facing your own fears head on. Inawezekana kuna mtu alikuumiza, namna nzuri ya kutoa donge moyoni mwako ni kumfuata na kuongea nae. Haijalishi kitatokea kitu gani lakini kile kitendo cha wewe kumfuata na kumweleza unavyojisikia utakuwa umetua mzigo mzito sana.
Na kama haiwezekani kuongea na mhusika basi tafuta mtu - ongea nae - mweleze ukweli wa unavyojisikia. Amini nakwambia the moment unavyoeleza utakuwa unaondoa sumu moyoni mwako (Ingawa unaweza kujisikia aibu/ fedheha/ uzito/ hatia/ n.k) Na zaidi ya yote, siku hizi kuna mitandao ya kijamii - andika watu wasome; Eee si ndio - Bila shaka unamfahamu Oprah Winfrey, na Shilole - ukiniuliza mimi nitakwambia kati ya vitu vilivyowasaidia sana ni kuweka wazi kuwa waliwahi kubakwa. The moment walipoweka wazi, naamini hawakujisikia hatia/ aibu/ fedheha/ stress tena mpaka leo.
Na kama ukija kunieleza mimi, na kisha kati kati ya simulizi ukaanza kulia kwa mfano; sitakubembeleza. Unajua kwanini? Unapotoa machozi ndio tiba yenyewe, so nitakuacha ulie mpaka umalize - kisha simulizi iendelee. On that note nashauri ukiona mtu analia kwa uchungu, usimnyamazishe - mwache alie, amalize - it is good for their health.
3. Acha kunyooshea watu vidole.
Kujichukulia wewe ni mhanga ni rahisi sana na huwa inamfanya ajisikie vizuri wakati mwingine. Badala ya kukubaliana na ukweli watu wengi huwa tunakimbilia kutafuta wa kumlaumu kwa matatizo tunayopitia. Tatizo ni kuwa, lawama zinatukwamisha tusisonge mbele. Na kuwanyooshea watu vidole ni lawama. Ukimlaumu mtu unamruhusu akutawale, na inakufanya ujisikie dhaifu kwake. Na lawama ni ugonjwa mbaya sana - ukikupata utalaumu kila kitu... utalaumu mkeo, utamlaumu Mungu, utamlaumu mshkaji wako, utalaumu mvua, utalaumu uchawi, utalaumu umeme... utalaumu, utalaumu utalaumu.
Kubali ukweli wa mambo; kama kuna maamuzi ya kipuuzi ulifanya - kubali kisha songa mbele. Kama kuna kosa ulifanya, kubali moyoni mwako kuwa ulikosea - kisha songa mbele. Usitafute visingizio, havitakusaidia hata kidogo... ofcourse ukipata kisingizio kizuri kitakufanya ujisikie vizuri kwa muda mfupi lakini kadiri muda unavyosogea utakuwa unajisikia hatia moyoni. Ki
4. Check company lako.
Wafanyie upembuzi waliokuzunguka. Nani yuko negative na kila siku anakukwamisha? Ni akina nani ambao walikuwa washkaji zako zamani na sasa unataka kuachana nao? Piga chini wote hao bila kusita sita, tafuta wale watakaokutia moyo. Ndugu hatuchagui lakini marafiki tunachagua.
Kuna namna nyingi za kupata marafiki wapya, na naamini zinafahamika.
5. Samehe waliokukosea - ukiwemo 'wewe mwenyewe'.
Umeumizwa na mtu fulani? Msamehe, mtendee wema bila kutarajia shukrani kisha endelea na maisha yako. Na usisahau kujisamehe wewe mwenyewe. Hakuna aliye mkamilifu duniani, sote tunakosea - tunawakosea wengine, tunamkosea Mungu, tunajikosea sisi wenyewe. Usijiadhibu kwa makosa ya zamani, badala yake jifunze na uyafanyie kazi yale uliyojifunza. Ukishazibwaga hizo hasira na kujihukumu, utaweza kusonga mbele.
6. Make new memories.
Anza saivi, tengeneza kumbukumbu mpya, positive memories ili ziwe mbadala wa zile za zamani. Tumia muda wako pamoja na watu wanaokufanya uwe na furaha, pamoja na vitu vinavyokupa faraja na maeneo yanayokupa amani. Kumbukumbu za zamani zikiwa nyingi kuliko za sasa ni mbaya kwa afya yako.
Kwahiyo ,achana na stori za 'nilikuwa', tengeneza mpya. Hakuna namna utaibadilisha jana, lakini kesho inategemea unachokifanya leo. Ukiua mtu leo - kesho utakuwa 'most wanted'. Ukimfanya mtu afurahi leo, kesho utakuwa na amani moyoni mwako. Ukimsaidia mtu leo, kesho utajisikia furaha moyoni mwako. Ukitatua changamoto inayokukabili leo, kesho utajisikia nguvu zaidi za kukabiliana na changamoto.
Ishi leo, furahia kila sekunde. Here's to living in the now. 🍷 Cheers!