Saikolojia ya Mtanzania ikoje? Kwanini wengi hushangilia kiongozi anapoonesha au kufanya jambo la kikatili?

Saikolojia ya Mtanzania ikoje? Kwanini wengi hushangilia kiongozi anapoonesha au kufanya jambo la kikatili?

Nadhani kama nchi, lazima tulishafanya study ya saikolojia na tabia za kabila, wilaya, mkoa wa nchi yetu. Hii inasaidia kiongozi akifika huko, anajua jinsi ya ku-deal na watu wa upande aliopo.

Hivi karibuni nilimsikia TAL akilalamika jukwaani, kabla ya kulalamika, ailikuwa akitoa historia ya jinsi JPM alivyomshughulikia kweli kweli, na wakati akitoa maelezo hayo, baadhi ya wananchi walikuwa wakitoa sauti za vicheko. Lissu akahoji, kwamba mimi ninawasimulia madhila niliyopata halafu mnacheka, akauliza kuna jambo la kuchekesha na kifurahisha hapo?

Hili hata mimi lilinitia huzuni, jambo la mtu kupigwa risasi linatakiwa kusikitisha na kuhuzunisha pale linaposimuliwa. Watanzania wanacheka, sasa jambo gani litamfanya mtanzania asikitike?

Tumekuwa tukiona hata majukwaani, inapotokea kiongozi kaonyesha ukatili, wananchi humshangilia, mpaka leo watanzania wakikumbushwa ukatili wa JPM, wao hukataa, wanaamini kwamba wale waliookotwa kwenye viroba, utekaji, na mengine machafu, kwa sio "issue".

Nini kimetufikisha hapa? Nani ana wajibu wa kusimika wema katika nchi? Kwa nini watu makatili wanafurahiwa sana na watanzania?
Sadism ni kasoro ya kisaikoljia ambapo mtu hufurahia maumivu ya wengine au kuwatesa kabisa.

Maskini wengi ni ma sadist hivyo hakuna ajabu yoyote kwa watanzania kufurahia vitendo vya ukatili alivyofanyiwa Lissu.

Hata leo bado wengi tu wanatamani kiongozi awe mkatili kwa maneno na vitendo ndio roho zao ziburudike.

Kuna kitu kimeharibu sana afya ya akili ya hili taifa mkuu.
 
Nimefurahi kusikia taarifa hizi!
Hadi leo anamnanga marehemu kwasababu gani!? Mtu gani asiejua kufanya mambo mengine zaidi ya kutafuta public sympathy.

Na mkewe akisema apite alalamike alivyo mtelekeza na kwenda kuoa mzungu atasemaje

Apumzike sasa maana hata siasa imemshinda anapigana chama utasema kabaki peke yake kwenye chama😂
 
mimi nadhani ni kawaida ki saikilojia ya kibinadamu watu wakiwa kwenye kundi kubwa wana behave tofauti,

sio Tanzania ni binadamu kwa ujumla
wakiwa kwenye kundi kubwa mass psychology.

na wanaweza kufanya mambo mengi irrationally. ambayo akiwa mtu mmoja tu bila wengine hafanyi mfano kuchoma moto mwizi n.k
 
Yeye mwenyewe alikuwa anachekelea madhila tuliyokuwa tunapata kama nchi. Nà kumtukana Rais wazi wazi.
 
Kuna mtu Yuko serious na Watanzania? Kwa taarifa yake JPM ni shujaa wao kama Makonda bila kujalisha alichomfanyia yeye na wengine.

Watanzania ni kama punda wanahitaji kuendeshwa Kwa Nguvu,Leo hii Samia wanamnanga na anaonekana mjinga na dhaifu kisa tuu hajaamua kuwa dikteta,katoa uhuru wa kuongea na mambo kama hayo.
Kwani tunamuona maza dhaifu au ni DHAIFU kweli? Tusiumeume maneno, maza hawezi.
 
Kwani tunamuona maza dhaifu au ni DHAIFU kweli? Tusiumeume maneno, maza hawezi.

Upo sahihi. Lengo la chama cha siasa ni kushika dola kupitia sanduku la kura, ili upate kura lazima uonyeshe udhaifu wa yule anayeongoza(Raisi ). Raisi ana majeshi na mabunduki sasa akiwa dhaifu kweli atamshughulikia kila anayemkosoa na kumkejeli. Kwa maandishi yako haya ingekuwa kwenye utawala uliopita (Raisi) siajabu tungekuta mwili wako kwenye kiroba kule fukwe za Coco Beach.
 
Hili hata mimi lilinitia huzuni, jambo la mtu kupigwa risasi linatakiwa kusikitisha na kuhuzunisha pale linaposimuliwa. Watanzania wanacheka, sasa jambo gani litamfanya mtanzania asikitike?
Mleta hoja wa Tanzania wengi ni mambumbumbu karibu kuwa mazezeta kwelikweli
Ndio maana CCM wanatuchezea wanavyotaka wamekuwa wanavunja katiba waliyoapa nayo watakavyo, kuhujumu nchi watakavyo, wizi, kupora mali za umma na mengi ya AIBU tupu.
 
Kwani tunamuona maza dhaifu au ni DHAIFU kweli? Tusiumeume maneno, maza hawezi.
Kinachothibitisha au kukushawishi wewe kwamba hawezi ni nini?

Mbona Mimi Nina sababu Bilioni za kuonesha sio tuu anaweza Bali amewazidi woote waliotangulia except Nyerere na Mkapa
 
Walicheka kwa kuwa wote tunajua kilichomtokea, sasa mbona anakuwa na nongwa na marehemu ?

Amwache JPM si hayupo tena?

Aeleze atakavyoibadili nchi na kurejesha maliasili zetu.
Kumkashifu Mkuu wa nchi akiwa madarakani tena hadharani kwa kujisifu huku ukimtaja jina lake huwa ni habari ingine na ya hatari na huwa na matokeo yasiyotarajiwa maana utawachukiza watu wengi wanaomkubali na huwezi kujua nani atakufanya nini katika hilo. Huwa si jambo lenye afya kokote duniani. Hata hivyo lazima tukiri lilikuwa tukio baya na la kikatili linalopaswa kulaaniwa na kila mtu mwenye akili timamu.

Nadhani raia walicheka sababu mnyampaa alileta mambo ya kale ya wahenga kina Chifu Mangungu sababu hiyo kitu ilishaenda , wabongo huwa hatuna tabia ya kutembea na kumbukumbu za mambo ya kale na kukomaa nazo, sie tunaishi leo, now now, here here, sio habari za jana na juzi!!
 
Huo ni ujumbe tosha kwake kwamba "NOBODY CARES"

Hiyo chorus imeshachuja imekuwa kichekesho tu
 
Kila siku nasema na ntasema sana CHUMA kiliponyoosha rula watu hapa walibweka kama mbweha ,
OOoh ,ooooh,vikaenda vikarudi haya CHUMA kikaenda kaja mama Kizimkazi wale wale tena ooh bora CHUMA ooooh blah blah uongozi umemshinda blah blah ila mkae mkijua tu kwa watu aina ya wabongo hawaitaji kubembelezana hawana wema ni rula mwanzo mwisho,na kama mtu haamini hata kwenye maisha tu ya kawaida jifanye mwema sanaaaa alafu uone kitakachokukuta.
 
Usichanganye mambo.
Nadhani unakumbuka issue ya Rufiji, Kibiti. Umaskini wetu ulitaka kuharibu Amani maeneo ya kusini. Vijana walienda kusoma ugaidi badala ya dini. Wakarudi na utaalamu wa kutumia silaha kuua.
Tumshukuru mwendazake kwa kutumia mbinu zote kuondoa balaa.
BORA UMSHUKURU MBAKAJI KULIKO HUYO TAKATAKA.
 
Back
Top Bottom