Kulwa Jilala
JF-Expert Member
- Sep 6, 2022
- 3,891
- 8,448
Wakili Msomi Alphonce Lusako akishirikiana na Wakili msomi Chengula Emmanuel pamoja na wenzao wawili wameiburuza serikali mahakamani kwa kupitisha mkataba wa ubinafsishaji wa bandari zetu bila kuzingatia maslahi ya nchi.
Washtakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi, Waziri wa Ujenzi Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi.
Wote wanne wanashtakiwa kwa makosa yafuatayo:
1. Washtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini Makataba wa kimataifa na kuupeleka bungeni kwa ajili ya kupitishwa bila kushirikisha umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutoa maoni yao, kinyume na sheria ya rasilimali za taifa no.5 ya mwaka 2017 kifungu cha 11 (1) na (2).
2. Washtakiwa no.1 na no.4 wanashtakiwa kwa kuwaongoza wabunge vibaya, kupiga kura ya ukasuku (ya kupayuka NDIOO) badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja kama sheria inavyotaka (Natural Wealth and Resource Contract Act) no.6 ya mwaka 2017 kifungu cha 5 na 6.
3. Mshtakiwa no.1 na no.4 wanashtakiwa kwa kushindwa kuliongoza bunge vizuri kufanya kazi yake ya kushauri serikali na kusimamia maslahi ya umma kwenye mikataba ya kimataifa kinyume na ibara ya 63(2) na (3) ya Katiba ya nchi.
4. Mshtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai wenye vipengele vinavyovunja Katiba (ibara ya 28(3) pamoja na sheria mbalimbali za nchi.
5. Washtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba wa "hovyo" unaozigawa rasilimali zetu za kimkakati kwa mamlaka ya nje ya nchi, kinyume na Katiba ibara ya 1, 8 na 28.
6. Kwamba Mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai una vipengele vinavyoweka rehani enzi kuu ya taifa letu (National sovereignty) na kuuza uhuru wetu, kinyume na ibara ya 1, 8 na 28 ya Katiba.
7. Kwamba Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai haukufuata sheria ya manunuzi ya umma no.64 ya mwaka 2011 na hivyo Mkataba huo kuwa batili tangu mwanzo (null & void ab-initio).
Washtakiwa wote wameitwa Mahakamani tar.3 July 2023 kujibu tuhuma zinazowakabili. Kesi hiyo itasikilizwa na Jaji Dunstun Ndunguru na Jaji Abdi Kagomba.!
View attachment 2670319