Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Fisadi Rostam alisema nendeni mahakamani

Ujue tayari mfumo wa mahakama umejuaanda kuwadhulumu watanganyika na kuwahalalisha waarabu kuuziwa nchi

Hapa ni kula sahani moja na hawa mafisadi
Masikini hulka yenu ni kuchukia tu matajiri na hili aliwaharibu sana yule Ibilisi kule Chato
 
Hakuna kesi hapo. Hawa majaji maandazi wa mahakama kuu wanaotegemea huruma ya rais ili kupata hizo nafasi unadhani watafanya nn?

Nchi ngumu Sana. Tu aposema tunataka katiba mpya ni pamoja na kuiondoa maujinga haya.

Hapa bongo rais ni kama Mungu
 
Mbona yule aliyesema yeye ndio alikuwa Kiongozi wa Timu ya majadiliano hajashtakiwa ?
Daa yule jamaa jau kweli. Aliwadanganya viongozi wa dini mchana kweupe wakawa wanamwangalia tu nadhani jamaa hajui watu kama TEC huwa wana taarifa za ndani kabisa na wana elimu kubwa katika kila sekta. Ila jamaa alinimaliza zaidi pale aliposema wao ni wazalendo kweli kweli na waliweka maslahi ya taifa mbele na huwa analia anapoona watu wanauzungumzia vibaya mkataba mtandaoni halafu eti mkewe huwa anambembeleza.

Hii nchi ukifa kwa "stress" utakuwa umejitakia mwenyewe.
 
Mawakili Alfonce Lusako na Emmanuel Chengula wakishirikiana na wenzao wamefungua Kesi Mahakamani dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipinga 'makubaliano ya mkataba' ulioingiwa baina ya Serikali hiyo na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World, makubaliano yanayolenga uendelezaji wa Bandari Nchini

Katika Kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambao washtakiwa wake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt.Eliezer Feleshi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi,
ambapo Mawakili hao wameeleza kuwa Washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na makosa yafuatayo:

1.) Washtakiwa namba 2 na namba 3 wanashtakiwa kwa kusaini Mkataba wa Kimataifa na kuupeleka Bungeni kwaajili ya kupitishwa bila kushirikisha Umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa Wananchi kutoa maoni yao, kinyume na Sheria ya raslimali za taifa namba 5 ya mwaka 2017 kifungu cha 11 (1) na (2),

2.) Washtakiwa namba 1 na namba 4 wanashtakiwa kwa kuwaongoza Wabunge vibaya kupiga kura ya "NDIO" badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja kama Sheria inavyotaka (Natural Wealth and Reasource contract Act) namba 6 ya mwaka 2017 kifungu cha 5 na 6,

3.) Mshtakiwa namba 1 na 4 wanashtakiwa kwa kushindwa kuliongoza Bunge vizuri kufanya kazi yake ya kuishauri Serikali na kusimamia maslahi ya Umma kwenye mikataba ya kimataifa kinyume na ibara ya 63 (2) na (3) ya Katiba ya Nchi,

4.) Mshtakiwa namba 2 na 3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 'Emirate' ya Dubai wenye vipengere vinavyovunja Katiba, Ibara ya 28 (3) pamoja na Sheria mbalimbali za Nchi,

5.) Washtakiwa namba 2 na 3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba wa 'hovyo' unaozigawa raslimali za taifa za kimkakati kwa mamlaka ya nje ya Nchi, kinyume na Katiba, Ibara ya 1, 8 na 28,

6.) Kwamba, Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 'Emirate' ya Dubai una vipengere vinavyoweka rehani enzi kuu ya taifa (National Sovereignty) na 'kuuza' uhuru wa Nchi, kinyume na Ibara ya 1, 8 na 28 ya Katiba, Nk

Washtakiwa wote wameitwa Mahakamani July 03.2023
 
Hatua nzuri transparency /uwazi ujulikane.

Maana kauli gongana zimekuwa nyingi kutoka serikalini na bunge lake juu ya mazuri na mapungufu wanayosema serikali imesikia kutoka kwa maoni ya wananchi na washika dau kibao.
 
Back
Top Bottom