Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Kwa namna hii rasilimali za Tanzania zitaanza kuheshimika.

Angalau tumeanza kuuona mwanga tuongeze elimu kwa wananchi ili tuwe na umoja kwenye masuala nyeti juu taifa letu
 
Hv yule jamaa alifunguaga kesi dhidi ya mitandao ya smu,,, iliishia wapi?
 
Mawakili Alfonce Lusako na Emmanuel Chengula wakishirikiana na wenzao wamefungua Kesi Mahakamani dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakipinga 'makubaliano ya mkataba' ulioingiwa baina ya Serikali hiyo na Serikali ya Dubai kupitia Kampuni ya DP World, makubaliano yanayolenga uendelezaji wa Bandari Nchini

Katika Kesi ya msingi iliyofunguliwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya ambao washtakiwa wake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Dkt.Eliezer Feleshi, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi Prof.Makame Mbarawa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Uchukuzi) Gabriel Migire na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi,
ambapo Mawakili hao wameeleza kuwa Washtakiwa wote wanne wanakabiliwa na makosa yafuatayo:

1.) Washtakiwa namba 2 na namba 3 wanashtakiwa kwa kusaini Mkataba wa Kimataifa na kuupeleka Bungeni kwaajili ya kupitishwa bila kushirikisha Umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa Wananchi kutoa maoni yao, kinyume na Sheria ya raslimali za taifa namba 5 ya mwaka 2017 kifungu cha 11 (1) na (2),

2.) Washtakiwa namba 1 na namba 4 wanashtakiwa kwa kuwaongoza Wabunge vibaya kupiga kura ya "NDIO" badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja kama Sheria inavyotaka (Natural Wealth and Reasource contract Act) namba 6 ya mwaka 2017 kifungu cha 5 na 6,

3.) Mshtakiwa namba 1 na 4 wanashtakiwa kwa kushindwa kuliongoza Bunge vizuri kufanya kazi yake ya kuishauri Serikali na kusimamia maslahi ya Umma kwenye mikataba ya kimataifa kinyume na ibara ya 63 (2) na (3) ya Katiba ya Nchi,

4.) Mshtakiwa namba 2 na 3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 'Emirate' ya Dubai wenye vipengere vinavyovunja Katiba, Ibara ya 28 (3) pamoja na Sheria mbalimbali za Nchi,

5.) Washtakiwa namba 2 na 3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba wa 'hovyo' unaozigawa raslimali za taifa za kimkakati kwa mamlaka ya nje ya Nchi, kinyume na Katiba, Ibara ya 1, 8 na 28,

6.) Kwamba, Mkataba kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 'Emirate' ya Dubai una vipengere vinavyoweka rehani enzi kuu ya taifa (National Sovereignty) na 'kuuza' uhuru wa Nchi, kinyume na Ibara ya 1, 8 na 28 ya Katiba, Nk

Washtakiwa wote wameitwa Mahakamani July 03.2023
Hao mawakili waliofungua kesi wasijekuwa ni maofisa kipenyo ili kuharibu
 
Hv yule jamaa alifunguaga kesi dhidi ya mitandao ya smu,,, iliishia wapi?
Yule aliingia mitini

Sijui aliminyiwa, kila akiulizwa atoe mrejesho jiiii

Ova
 
Wakili Msomi Alphonce Lusako akishirikiana na Wakili msomi Chengula Emmanuel pamoja na wenzao wawili
Kwenye jambo muhimu kama hili, ninapendekeza mawakili wote wanne wanaohusika katika jambo hilo majina yao yatajwe na yapewe uzito stahiki.
Hawa ni mashujaa wa nchi, iwe wamefanikiwa au hawakufanikiwa katika juhudi zao za kuipigania Tanzania.
 
Wakili Msomi Alphonce Lusako akishirikiana na Wakili msomi Chengula Emmanuel pamoja na wenzao wawili wameiburuza serikali mahakamani kwa kupitisha mkataba wa ubinafsishaji wa bandari zetu bila kuzingatia maslahi ya nchi.

Washtakiwa ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali Eliezer Feleshi, Waziri wa Ujenzi Makame Mbarawa, Katibu Mkuu Uchukuzi Gabriel Migire na Katibu wa Bunge Nenelwa Mwihambi.

Wote wanne wanashtakiwa kwa makosa yafuatayo;

1. Washtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini Makataba wa kimataifa na kuupeleka bungeni kwa ajili ya kupitishwa bila kushirikisha umma na kutoa nafasi ya kutosha kwa wananchi kutoa maoni yao, kinyume na sheria ya rasilimali za taifa no.5 ya mwaka 2017 kifungu cha 11 (1) na (2).

2. Washtakiwa no.1 na no.4 wanashtakiwa kwa kuwaongoza wabunge vibaya, kupiga kura ya ukasuku (ya kupayuka NDIOO) badala ya kura ya Mbunge mmoja mmoja kama sheria inavyotaka (Natural Wealth and Resource Contract Act) no.6 ya mwaka 2017 kifungu cha 5 na 6.

3. Mshtakiwa no.1 na no.4 wanashtakiwa kwa kushindwa kuliongoza bunge vizuri kufanya kazi yake ya kushauri serikali na kusimamia maslahi ya umma kwenye mikataba ya kimataifa kinyume na ibara ya 63(2) na (3) ya Katiba ya nchi.

4. Mshtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai wenye vipengele vinavyovunja Katiba (ibara ya 28(3) pamoja na sheria mbalimbali za nchi.

5. Washtakiwa no.2 na no.3 wanashtakiwa kwa kusaini mkataba wa "hovyo" unaozigawa rasilimali zetu za kimkakati kwa mamlaka ya nje ya nchi, kinyume na Katiba ibara ya 1, 8 na 28.

6. Kwamba Mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai una vipengele vinavyoweka rehani enzi kuu ya taifa letu (National sovereignty) na kuuza uhuru wetu, kinyume na ibara ya 1, 8 na 28 ya Katiba.

7. Kwamba Mkataba kati ya Serikali ya Tanzania na Emirate ya Dubai haukufuata sheria ya manunuzi ya umma no.64 ya mwaka 2011 na hivyo Mkataba huo kuwa batili tangu mwanzo (null & void ab-initio).

Washtakiwa wote wameitwa Mahakamani tar.3 July 2023 kujibu tuhuma zinazowakabili. Kesi hiyo itasikilizwa na Jaji Dunstun Ndunguru na Jaji Abdi Kagomba.!

View attachment 2670319
Safi sana
 
Back
Top Bottom