Sakata la Bandari na DP World: Serikali yashtakiwa Mahakamani

Wamefanya vizuri tatizo wameenda mahakama ya ccm hii ndio shida.Ila Sa100 kwa hili DP world nimemshangaa mno mtu unawezaje kufanya kitu kama hiki. Au hakuwa na mwanasheria ambae na yeye angesema kuna vipengele havipo sawa yeye kaenda kule ni ndio ndio ndio.Ama kweli mtemi Mangungo amerudi tena Tanzania na safari hii karudi kwa jinsia tofauti
 
Mahakama gani? au unaongelea hizi Mahakama za CCM?
Rostam, myamwezi wa Tabora ameshasema Mahakama zetu za Kisutu haziaminiki; zinazoaminika ni zile za South Africa ambako ndege yetu ya Boeing inashikiliwa kwa karibuni mwaka mmoja sasa na inaweza ikapigwa mnada. Serikali ilisha mute kuhusu suala hilo la ndege yetu. Sasa tayari tumeshasaini na bunge kuridhia mkataba wa IGA wa bandari zetu zote kushitakiwa South Africa kama tutavunja hiyo IGA.
 
Isijekua wanatumika ili ishu hii ije ihalalishwe!
 
Ni vizuri sasa TLS ikajiunga kwenye kesi hii kama interested party ili munyukano huu wa kisheria mahakamani uwe na nguvu kubwa hadi kieleweke. Na uendelee hadi mahakama yetu ya upeo (rufaa) na mahakama ya katiba. Hii itakuwa funzo kwa spika wetu huyu Tulia kuacha kuliburuza bunge letu kwa msimamo ya kisiasa. Spika wa bunge anapaswa kuwa neutral katika mijadala ya bunge na kuruhusu free debate ya pande zote mbili: ile inayounga mjadala wa serikali na ile inayopinga mjadala wa serikali. Huyu spika kajionesha wazi wazi kuwapinga na hata kuwazuia wasiseme wale wote wanaopinga mijadala ya serikali kama akina Mpina. Amepoka demokrasia kwenye bunge letu. Yeye kapoka kazi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali (AG) ya kuitetea kisheria mijadala / misuada ya serikali inayofikishwa bungeni. Huyu spika ndiye amesababisha suala hili la mkataba wa IGA kufikia hatua hizi tunazozishuhudia. Kwa spika mweledi hatungalifika huku.
 
Hakuna kitu hapo ni Wakili anatafuta kiki kwenye CV yake. Hakuna Mahakama onevu na oga kama Mahakama ya Tz. Mahakama inayochukuwa haki ya mbuzi inampa fisi. Ndiyo maana DPW wameistudy Mahakama ya Tz na kugundua ni tarishi na nyapara wa serikali, DPW ikaogopa na kutaka kesi zote za kimkataba ziende Afrika Kusini. Mahakama ya Tz inaendeshwa kwa akili za Pilato, Herode, Herodia na Yuda wa Iskariote.

Wakili Alphonce anapoteza muda. Mbona Wakili Wangwe ameshinda hadi Mahakama ya EAC lakini bado nchi inaendesha chaguzi ndogo za marudio za Madiwani bila kuzingatia uamuzi wa Korti hiyo ya EAC kwenye shauri la Wakili Wangwe aliyepewa haki (ushindi).

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
AG hana kazi, Spika anafanya kazi ya AG.
Dubai kusaini mikataba pia AG hakwenda, hatujui kama rais alichukuwa ushauri wa AG au alivaa makoti 2 ya rais na AG kama Spika alivyovaa koti 2 za Spika na AG.

Katika hali ya kawaida kabisa, AG alitakiwa hadi sasa ameishajiuzulu ili kutetea usafi na weledi (professionalism) wake.

Sijajuwa hadi sasa VP, PM, CDF wanashiriki kumpoteza mama kwa kumshauri visivyo au labda wamesondwa? Nini mchango wao kwenye abracadabra hii?

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
daah mmetukosea sana waTanganyika mnaoangalia maslahi yenu na familia zenu
 
Kusoma ni jambo moja, kusaliti elimu yako na uzalendo wako ni jambo jingine.

Taratibu taratibu tutawaelewa Magufuli na Ndugai.

Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
Ambacho hujui ni kwamba hatutegemei kushinda, bali huu ni mchakato mahsusi wa kuamsha nguvu ya UMMA! Be careful
Wafuatao waunge mkono jitihada za Wakili hawa ili tujiridhishe na uhalali wa ufunguaji wa shauri hili:-

1. Viongozi wa Dini (akina Kitima, Kilaini, Kakobe, Niwemugizi, Mwingira, Bagonza, Eliona Kimaro, Hananja, wengine ni Madeganyanga)
2. Wanahabari.
3. Wasomi Vyuo Vikuu.
4. Wapinzani.
5. Wanaharakati.
6. Wamachinga.
7. Trade Unions ambao maelfu ya wanachama wao wanapoteza kazi kwenye bandari 65 (58 za ziwa, 5 za bahari na 2 bandari kavu).

Madai yao:-
1. Mkataba huu na mingine chechefu ipigiwe kura ya maoni (referendum) kuikataa au kuikubali.

2. Wahusika wote wawajibishwe.

3. Mamlaka ya rais yapunguzwe kwa 50% kwa njia ya kuandika Katiba Mpya.

4. Rais avunje Bunge nchi iende kwenye uchaguzi, maana Bunge haliaminiki tena, Serikali haiaminiki tena, Mahakama nayo haiaminiki tena kwa kuwa inaendesha tu mashauri lakini hukumu inaandikiwa na serikali.

5. Mafao ya wafanyakazi wa bandari zote 65 wanaoachishwa ajira na mkataba huu. Vyama vya wafanyakazi DOWUTA, TRAWU, TUCTA vianze jaramba la kudai mafao bora, kikokotoo cha kueleweka kwa kuwa wao ndiyo jasho lao lilichangia asilimia kubwa 39% ya bajeti ya taifa.

6. TAKUKURU ifanyiwe marekebisho upya ya sheria iliyoiunda ili sheria mpya iifanye kuwa taasisi huru kabisaaa 100% ya uchunguzi. Kwa jinsi hii itatenda haki na itatendewa haki pia. Aidha, itakuwa na weledi kitaifa na kimataifa kiasi kwamba itaweza kushinda zabuni za uchunguzi za kimataifa kama zilivyo Scotland Yard, Federal Bureau of Investigation, Central Intelligence Agency, US Intelligence Coy, Federal Security Services, Research Analysis Wing, M16, Secret Intelligence, Canadian Security Intelligence na (SVR, FSB, FSO, GUSP za Urusi zilizochukuwa nafasi ya KGB) na kuliingizia taifa la Tz mapato pia.

NB.
Nina wasiwasi hii kesi ya Wakili Alphonce Lusako na Wakili Chengula Emmanuel ni geresha la dola kuwahadaa na kuwachanganya wananchi. Time and circumstance will prove me correct later.


Sent from my SM-A260F using JamiiForums mobile app
 
wangekua wameishitaki serikali nje ya Africa hapo ningewaelewa.

ila hapa hapa Mahakama yenyewe ni ya Serikali halafu unaishtaki Serikali ?

wategemee kupewa kesi za kutolipa kodi nk.

niko hapa nimekaa
 

Attachments

  • C2EE77F4-C290-4C6C-ACEF-962CEC7F4451.jpeg
    17.4 KB · Views: 4
Natamani kujitoa mhanga pale katikati ya bunge.
[emoji23]
nisepe na kijiji cha wajinga
Nasemaje.. Nasemaje...! Wa husika wote yaani na wale wamjengoni Dodoma waongeze ulinzi hadi vijijini kwako... Babu na bibi zao wawe na mabody guard.. Wasije kusema sijawaonya... 😁 😁 😁
 
Safi sana
 
Samia tunataka BANDARI zetu
 

Attachments

  • tweeload_12010876.mp4
    2.6 MB
Fisadi Rostam alisema nendeni mahakamani

Ujue tayari mfumo wa mahakama umejuaanda kuwadhulumu watanganyika na kuwahalalisha waarabu kuuziwa nchi

Hapa ni kula sahani moja na hawa mafisadi
Kazi ipo!!
 
100%
 
4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…