Mdude_Nyagali
Member
- Dec 11, 2022
- 79
- 1,444
Sakata la bandari zetu kupigwa mnada wakili Boniface Mwabukusi Boniface Mwabukusi amefanya uchambuzi wa mwisho na kuanisha mapungu ya kisheria yaliyopo kwenye mkataba huo.
Kwamba kutokana na mapungufu hayo ya kisheria tutaenda Mahakama Kuu Tanzania kufungua shauri kwa hati ya dharura. Tutaiomba Mahakama imuamuru mara moja Waziri mwenye dhamanakuurejesha Mkataba ule Bungeni ukiwa na MoU, IGA na Mchanganuo wa Mradi ili Bunge na wananchi wapate haki yao ya Kikatiba ya Kutoa maoni.
Kwamba lengo la shauri hilo ni:
(a) kuwezesha na Kutoa Muda wa Kutosha wa Bunge Kuujadili na kuufanyia Marekebisho.
(b) Kutoa Muda wa Kutosha kwa wadau na Wananchi kuuelewa, kuujadili na kutoa Maoni yao kuhusu mambo yanayojumuishwa katika IGA.
(c) Kuweka Utaratibu maalum ambao wadau wote (ikiwemo Indegenous people) ambao kwa msingi wa Maisha yao, Maeneo yao, jamii yao na shughuli zao Kiuchumi zimefungamana na Maziwa. Kwamba jamii yao na shughuli zao Kiuchumi zimefungamana na Maziwa , bahari ,Strategic Economic Zone ambazo utekelezwaji wa IGA hii unaweza moja kwamoja kwa kwanjia zisizo za moja kuathiri maisha, Mila, itikadi za watu hawa ni (Wenyeji wa asili wa Maeneo ambayo mradi inayojumuishwa katika IGA –katika ukanda wa bahari na maziwa makuu.
(d) Ili kuondoa Utata uliopo Mahakama iamuru serikali kupitia Waziri mwenye dhamana kutoa IGA katika lugha ya Kiswahili na kuisambaza kwa wadau na wananchi wote pamoja na kuzingatia matakwa yote ya kisheria kwa mujibu wa Mikataba ya namna hii.
(e) Kuboresha Makubaliano ya IGA na kuweka bayana
i. Ukomo na mawanda ya Mradi na utekelezwaji wa shughuli zote
zilizokubaliwa katika mradi husika
ii. Kuweka kifungu cha kuongoza uvunjaji wa Mkataba.
iii. Kuondoa Vifungu vinavyoashiria umilele.
iv. Kuondoa Vifungu vyote ambavyo moja kwa moja au kwa matokeo yake vinaondoa Haki ya nchi ya umiliki wa raslimali (Sovereignty), haki ya nchi kufanya ushindani na fursa ya nchi kuruhusu wawekezaji wengine katika eneo la uwekezaji wa bandari.
v. Kuhakikisha Uzingatiwaji wa Sheria Zingine za Nchi na kuhakikisha kwamba Mkataba huu hauwi juu ya Katiba ya nchi, sheria za Ardhi na sheria zinazolinda raslimali asili za nchi.
Mdude Nyagali 7 x 70 Sumu ya Nyigu.
Habari zaidi, soma: