Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
SAKATA LA BARAKA SHAMTE: HATARI YA KUSEMA YASIYOTAKIWA KUSEMWA
Katika kila jamii kunakuwa na ''mwiko,'' yaani kitu kisichotakiwa kufanywa na kwa kawaida huwa watoto wanafunzwa toka udogoni.
Katika jamii nyingi watoto wa kiume hufunzwa kutofungua mifuko ya wanawake uwe mama au dada zao.
Hufunzwa kutofunua chungu au sufuria iliyoko jikoni nk. nk.
Haya kwa wanaume na ipo miko ya jumla kwa jamii nzima kwa mfano kutofagia usiku au kukata kucha usiku.
Haya yanafahamika.
Katika siasa za uendeshaji dola kuna vitu vinafahamika si siri lakini ingawa si siri havitakiwi kusemwa hadharani.
Mkasa wa Baraka Shamte umenikumbusha kisa cha Sheikh Abubakar Mwilima na Julius Nyerere.
Kipande hicho hapo chini nimekitoa katika taazia niliyomwandikia Mzee Aboud Jumbe alipofariki mwaka wa 2016:
''Aboud Jumbe alikuwako katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM siku Abubakar Mwilima alivyomkabili Nyerere uso kwa macho kama Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM na kumuuliza imekuwaje Waislam wako nyuma wakati wenzao wanasongambele.
Nyerere alikuwa kimya.
Ukumbi mzima vilevile ulikuwa kimya. Wajumbe walikuwa wameshika roho zao mkononi.
Swali hilo hakuna aliyekuwa hajui kuwa ni mwiko mkubwa kuulizwa. Kwa sekunde chache ilikuwa kama vile dunia imesimama, haizunguki, imetuwama mahali pamoja.
Nyerere aliahirisha kikao wajumbe wakanywe chai.
Aboud Jumbe alikuwako na alishuhudia jinsi wajumbe wa mkutano walivyomkimbia Mwilima.
Hakuna aliyetaka kumkaribia wala kuongea na yeye. Mwilima alikaa mezani akinywa chai peke yake.
Wenzake wote hata wale marafiki zake wa siku zote walimkalia mbali. Waliporudi kikaoni Nyerere aliendelea na mkutano kama vile hakuna kilichopitika.
Nyerere hakutaka kulijibu swali la Sheikh Mwilima.
Haukupita muda Sheikh Abubakar Mwilima aliitwa kuhojiwa kuhusu kuuza dola za Kimarekani kinyemela.
Haukupita muda akajikuta yuko nje ya siasa.''
Kisa hiki alinihadithia Sheikh Abubakar Mwilima mwenyewe na baadae nikakipata kutoka kwa Mzee Aboud Jumbe nyumbani kwake Mji Mwema.