Sakata la Baraka Shamte: Hatari ya kusema yasiyotakiwa kusemwa

Sakata la Baraka Shamte: Hatari ya kusema yasiyotakiwa kusemwa

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
SAKATA LA BARAKA SHAMTE: HATARI YA KUSEMA YASIYOTAKIWA KUSEMWA

Katika kila jamii kunakuwa na ''mwiko,'' yaani kitu kisichotakiwa kufanywa na kwa kawaida huwa watoto wanafunzwa toka udogoni.

Katika jamii nyingi watoto wa kiume hufunzwa kutofungua mifuko ya wanawake uwe mama au dada zao.

Hufunzwa kutofunua chungu au sufuria iliyoko jikoni nk. nk.

Haya kwa wanaume na ipo miko ya jumla kwa jamii nzima kwa mfano kutofagia usiku au kukata kucha usiku.

Haya yanafahamika.

Katika siasa za uendeshaji dola kuna vitu vinafahamika si siri lakini ingawa si siri havitakiwi kusemwa hadharani.

Mkasa wa Baraka Shamte umenikumbusha kisa cha Sheikh Abubakar Mwilima na Julius Nyerere.

Kipande hicho hapo chini nimekitoa katika taazia niliyomwandikia Mzee Aboud Jumbe alipofariki mwaka wa 2016:

''Aboud Jumbe alikuwako katika kikao cha Kamati Kuu ya CCM siku Abubakar Mwilima alivyomkabili Nyerere uso kwa macho kama Rais wa Tanzania na mwenyekiti wa CCM na kumuuliza imekuwaje Waislam wako nyuma wakati wenzao wanasongambele.

Nyerere alikuwa kimya.

Ukumbi mzima vilevile ulikuwa kimya. Wajumbe walikuwa wameshika roho zao mkononi.

Swali hilo hakuna aliyekuwa hajui kuwa ni mwiko mkubwa kuulizwa. Kwa sekunde chache ilikuwa kama vile dunia imesimama, haizunguki, imetuwama mahali pamoja.

Nyerere aliahirisha kikao wajumbe wakanywe chai.

Aboud Jumbe alikuwako na alishuhudia jinsi wajumbe wa mkutano walivyomkimbia Mwilima.

Hakuna aliyetaka kumkaribia wala kuongea na yeye. Mwilima alikaa mezani akinywa chai peke yake.

Wenzake wote hata wale marafiki zake wa siku zote walimkalia mbali. Waliporudi kikaoni Nyerere aliendelea na mkutano kama vile hakuna kilichopitika.

Nyerere hakutaka kulijibu swali la Sheikh Mwilima.

Haukupita muda Sheikh Abubakar Mwilima aliitwa kuhojiwa kuhusu kuuza dola za Kimarekani kinyemela.

Haukupita muda akajikuta yuko nje ya siasa.''

Kisa hiki alinihadithia Sheikh Abubakar Mwilima mwenyewe na baadae nikakipata kutoka kwa Mzee Aboud Jumbe nyumbani kwake Mji Mwema.

1655291283307.png

1655291321428.png

1655291351109.png
 
Nyerere alikuwa sahihi sana kukaa kimiya kwani yeye huyo Mwilima alitakiwa swali hilo akaliulize Msikitini,hapakuwa mahali pake pale,hakukuwa na majibu sahihi pale kwenye hadhira ile.
Dah. Hii si sawa kabisa 😀
😀 😀
 
Hata wewe ungekuwa ndiye Mwalimu ungemjibu nini?.

Hilo swali alipaswa kujiuliza yeye na Wenzake na watafute ufumbuzi.
 
Kama agenda ya hicho kikao cha Kamati Kuu ya CCM haikuwa kujadili mada hiyo basi ni Mwilima pekee alitakiwa atolewe nje.

Cake ndiyo uchafu inapowekwa chooni.

BTW:Wajumbe walimsusa sababu ya woga na unafiki tu ila wengi walitaka ajibiwe.😁
 
Nyerere alikuwa sahihi sana kukaa kimiya kwani yeye huyo Mwilima alitakiwa swali hilo akaliulize Msikitini,hapakuwa mahali pake pale,hakukuwa na majibu sahihi pale kwenye hadhira ile.
Steve...
Wala lile halikuwa swali la msikitini.
Kuna historia yake.

Nyerere alikuwa anajua chanzo cha tatizo lile na ni katika masuala ambayo yakimtia hofu kubwa.
 
Tatizo wafuasi wa dini ya mnyazi mnakuwaga na inferiority bila sababu za msingi, sasa inamaana huyo mwilima alikua hajui kuwa watu wa dini yake wanakazania watoto waende madrasa kuliko shule? angalia hata misikiti mingi badala ya kujenga shule au huduma za afya wao wanajenga frem ili wauze dawa za kisuna na kuweka kijiwe cha gahawa kwa mtindo huo kwanini msibani nyuma? Mfano hata msikiti uliofunguliwa na rais huko bukoba umegharimu bilioni tano ila zaidi ya madrasa hakuna huduma ya kijamii itakayotolewa mkiugua mnaenda hospital za kanisa ila wanawasaidia bila ubaguzi kwakuwa Yesu Kristo aliwafundisha Upendo na mwisho wote mtakiri jina lake.
Kaya...
Ingekuwa jibu la swali la Sheikh Abubakar Mwilima ni jepesi kiasi hicho jibu lingetoka.

Lakini hilo swali ni zito sana hadi leo.
Serikali haiwezi kutoa jibu hadi leo.
 
Kaya...
Ingekuwa jibu la swali la Sheikh Abubakar Mwilima ni jepesi kiasi hicho jibu lingetoka.

Lakini hilo swali ni zito sana hadi leo.
Serikali haiwezi kutoa jibu hadi leo.

Shekhe mwilima alikua ni mdhaifu kifikra na kiakili kwani ilitakiwa ajiulize pia Kwanini kipindi hicho jamii kubwa ya wachaga walikua mbele sana kimaendeleo kuliko jamii nyingi za watu wa Rukwa, kigoma, dodoma au Kwanini mikoa ya dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro, Tanga ilikua imeendelea kuliko mikoa ya lindi, mtwara, ruvuma, singida. Serikali ije na majibu gani kwa maswali hayo.
 
Steve...
Wala lile halikuwa swali la msikitini.
Kuna historia yake.

Nyerere alikuwa anajua chanzo cha tatizo lile na ni katika masuala ambayo yakimtia hofu kubwa.
Nikuulize kitu Mkuu,ungekuwa wewe ndio Nyerere ungejibu nini?
 
Nikuulize kitu Mkuu,ungekuwa wewe ndio Nyerere ungejibu nini?
Steve...
Haya mambo si mepesi kama unavyodhania.

Inataka uijue historia ya Mwalimu Nyerere mwenyewe kwanza na hali ya siasa Tanganyika alipofika Dar es Salaam mwaka wa 1952.

Aliwakuta nani wameungana katika vita ya kupiga na dhulma ya ukoloni.
Yaliyotokea wakati wa kupigania uhuru na nini matokeo yake unayajua?

Inataka utulivu usome historia hii yote.
Hapo unaweza ukaelewa.

Unawajua hawa walioko kwenye picha hii ya 1955/56?
Umepata kusomeshwa historia yao au hata kuwasikia wakitajwa popote pale?

Jiulize kwa nini?
Hii ni historia ya kizazi kizima ilifutwa.

1655328522096.jpeg
1655328638619.png
 
Shekhe mwilima alikua ni mdhaifu kifikra na kiakili kwani ilitakiwa ajiulize pia Kwanini kipindi hicho jamii kubwa ya wachaga walikua mbele sana kimaendeleo kuliko jamii nyingi za watu wa Rukwa, kigoma, dodoma au Kwanini mikoa ya dar es salaam, Arusha, Kilimanjaro, Tanga ilikua imeendelea kuliko mikoa ya lindi, mtwara, ruvuma, singida. Serikali ije na majibu gani kwa maswali hayo.
Ujamaa...
Tatizo si hilo.
Nyerere alikuwa anamjua Mwilima na ndiyo maana alikaa kimya na alibakia kimya kwa swali hilo hadi anaingia kaburini.

Kwani ulikuwa unaijua historia unayosoma kutoka kwangu?
Hujiulizi kwa nini historia hii ilifutwa?
Mohamed Said dini inakupa tunnel vision pamoja na usomi wako.
 
Ujamaa...
Tatizo si hilo.
Nyerere alikuwa anamjua Mwilima na ndiyo maana alikaa kimya na alibakia kimya kwa swali hilo hadi anaingia kaburini.

Kwani ulkiuwa unaijua historia unayosoma kutoka kwangu?
Hujiulizi kwa nini historia hii ilifutwa?

Sio yako tu historia nimezisoma nyingi sana na vitabu vingi sana vingine vinaelezea watu tofauti kabisa hata historia unayotusomesha hapa nayo naisoma pia, wapo watu wengi sana ambao hata wewe hujawaandika na walikua wakipigania uhuru wa nchi hii na hao ndugu zako historia zao hazijafutwa bali hazikuandikwa kama za watu wengine ndo maana wewe ukachukua jukumu la kuandika historia zao kwa mitazamo yako.

Mwalimu alibaki kimya kwasababu jibu la hilo swali angejibu nini ingali kipindi hicho mpaka leo hii jamii kubwa ya wakristu, waislamu na wanaoabudu mizimu na wasio abudu kitu bado wapo hoe hae na hali za kimaisha ni za kuogofya, Mbona mambo yapo wazi.

uko vijijini hali ni tete umaskini ni mkubwa kwa jamii yote ya waislamu na wakristu. mijini makundi ya watu wapo wanalala nje na huruzi ustazi umekulia kariakoo hili unalijua, kiuhalisia jamii nzima ya watanzania hali ni mbaya sana hata milo na mienendo ya kimaisha ni tete.

sasa hao waislamu wa mwilima ni wapi ingali kipindi hicho jamii zote zilikua hoi hata usafiri tu na miundombinu yake ilikua hakuna na bado mpaka sasa jamii nzima ya watanzania ni makapuku wa kutupwa na nchi bado haijakizi vigezo vya kuitwa nchi ilio endelea bado ni third world country.

Jamani zungukeni mikoani zungukeni vijijini hali ni mbaya pili mwalimu hayupo toka 1999 hata wapigania uhuru waliopo hawapo kwene mamlaka na wengine ndo wanaumaliza mwendo wapo hoi kwa umri. tunafanya nini kutokomeza umaskini wa wa wananchi wa nchi hii hizo historia za kina mwilima ndo zinaishilizia hivyo lakini jamii nzima ya watanzania ni makapuku kabisa.
 
Back
Top Bottom