DOKEZO Sakata la binti wa Yombo lilishatokea kama hilo Kilindi -Tanga

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Habari zenu wanajukwaa. Nimatumaini yangu kwamba mmeamka salama salmin
Moja kwa moja kwenye mada ni kwamba lipo sakata linalofanana na la binti wa Yombo ambapo limetokea wilayani Kilindi mkoani Tanga. Ni zaidi ya wiki kama tatu hivi tangu tukio hilo lifanyike lakini rushwa ndio inatembea.

Tukio hilo limetokea jirani na mji wa Songe Kijiji kiitwacho Kwamwande ambapo binti huyo aliitwa na jamaa aliyekuwa amezaa nae kwamba eti akachukue matumizi.

Baada ya msichana huyo kufika kumbe walijiandaa vijana nane kumuingilia dada huyo ambae alikuwa amejifungua hata siku arobaini hajamaliza.

Inasemekana vijana waliofanikiwa kumuingilia walikuwa watano. Ingawa baadhi walikamatwa na polisi pia walipewa dhamana kwa sharti la kila mmoja kutoa laki tano. Kilichopo ni ukimya usiokuwa na majibu.
Rushwa imetumika kumkosesha binti huyu haki yake.

OCD Songe achunguzwe kwa kulikalia kimya suala hili na kutowafuatilia wabakaji wengine Ili kumpatia haki msichana huyo.

Hata baada ya kutoka hospitalini msichana huyo aliendelea kupata tabu maumivu makali ya kubakwa na watu watano huko akiwa bado alijifungua siku sio nyingi.

Natoa rai kwa makundi mbalimbali wasaidie haki ya mtanzania huyo
Kuna tatizo kubwa kwenye haki jinai kubwa sana
 
BILA PICHA AU KAVIDEO NI UZUSHI
 
Mwezi wa nane kuna matukio matatu muhimu nchini kwetu ambayo ni nanenane, simba day, na siku ya wananchi. Sasa ili kukomesha haya mambo ya ubakaji na maovu mengine ni rasmi sasa rais atangaze iwe ni mwezi wa kujichukulia sheria mkononi ili kukomesha usengerema wa namna hii 😀.
 
Ukinisaidia kuniunganisha na walalamikaji itakuwa vema sana. Wakati huo, kwa taarifa hii, ngoja tuwasiliane na huko Tanga.
Habari mama. Zinaendelea kufanyika juhudi hata kupatiwa namba ya simu ya binti au mzazi wake
Ahsante mama
 
Kama wale wakipata hukumu basi watakamatwa wengi sana , hiyo michezo ya kijinga wanaita ''mtungo'' wanafanyia sana mabinti za watu , halafu wanajisifu kabisa kwenye maskani zao .

Hawa vijana wenye vyumba wanaita ''geto" wengi ni wajinga sana kweny kutesa mabinti za watu.
Mambo ya hovyo sana
 
Akina Mwamposa na wenzake badala wakemee haya mapepo kwenye madhabahu yao wao kila siku ni matamasha. Leo ya kuwasha mishumaa, kesho tochi za simu mara sijui komboa nyota. Vitu vya ujingaujinga tu mradi wapige hela. Haya mapepo ya ukatili yaliyoibuka ndo ya kudili nayo kama huo uwezo wanao
Kazi ya mwamposa ni kuhubiri tu ila kukamata,kushitaki na kufunga ni kazi ya serikali
 
Back
Top Bottom