Sakata la DP WORLD bado kizungumkuti, Mbunge Luhaga Mpina ahoji uhalali wa Mkataba Bungeni

Sakata la DP WORLD bado kizungumkuti, Mbunge Luhaga Mpina ahoji uhalali wa Mkataba Bungeni

..mkataba unasema Dp world atawekeza usd 250 mil.

..bwana zake Jpm wa barrick waliahidi kutulipa kishika uchumba usd 300 mil.
 
Ajichunge naona maisha yake yapo mashakani maana anaenda tofauti na maazimio ya vikao vya ndani.
 
Luhaga mmoja ni zaidi ya Wabunge wote wa Upinzani
Hata wakumpigia makofi hamna, Ni Kama mijitu iliyomwagiwa maji, au watu wanaojua binti zao wanabakwa lakini wamepewa big G Kama kifuta jasho wakijua kabisa utamu wa big G Ni wa muda tu lakini watafanyaje big G walishatia mdomoni.
 
"Mkataba wa bandari kati ya TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania) na DP World hadi hivi sasa Waziri ameshindwa kueleza huyu DP WORLD anakwenda kuwekeza shilingi ngapi? Na anakwenda kuwekeza maeneo gani.

Kama tathimini imeshafanyika kuna shida gani kutueleza huyo DP WORLD anakwenda kuwekeza shilingi ngapi?

Na tathimini imefanywa na nani kuthibitisha mahitaji ya uwekezaji tunaoutaka" Luhaga Mpina, Mbunge wa jimbo la Kisesa
yaani hoja itolewe na mpina then ilete kizungukuti?
 
Hivi punde watamziba mdogo kwa kumpatia UWAZIRI.
 
Huyu Luhanga sii mbunge wa jimbo kama tunavyofikiri.
Huyu ni mbunge wa taifa[emoji123]

Sent using Jamii Forums mobile app
Tunawahitaji wengi wa aina hiyo wakati huu kuliko wakati mwingine wowote..
Nchi yetu inanyemelewa sana wakati huu na mafisi ya dunia, na kwa bahati mbaya kwetu, tunao viongozi wasiotambua wajibu wa uongozi wao kwetu ni nini.
Wapo tayari kutuuza hawa.
 
Mwenyezi Mungu amlinde! Maana asipoangalia atajikuta anaanza kufukua Makaburi.
Kitu ambacho ni hatari.
Kama sikosei Hayati JPM alimpenda huyu jamaa kwa sababu alikuwa na kau Ukichaa kama Yeye.
 
"Mkataba wa bandari kati ya TPA (Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania) na DP World hadi hivi sasa Waziri ameshindwa kueleza huyu DP WORLD anakwenda kuwekeza shilingi ngapi? Na anakwenda kuwekeza maeneo gani.

Kama tathimini imeshafanyika kuna shida gani kutueleza huyo DP WORLD anakwenda kuwekeza shilingi ngapi?

Na tathimini imefanywa na nani kuthibitisha mahitaji ya uwekezaji tunaoutaka" Luhaga Mpina, Mbunge wa jimbo la Kisesa
Hakuna hatakaye thubutu kueleza ukweli wa huo mkataba kwakuwa hauna ukweli hata kidogo.
 
Wacha Mpina aendelee kuzichangamsha bongo zilizolala kule bungeni.
Na nyengine zilizolala humu. Inakuwaje kila mtu anaekosoa kwa maslahi ya taifa anapigwa vita na kuonekana hafai atapewa ubalozi kumpoteza kabisa?
Serikali kama ipo makini inahitaji watu kama hawa coz vyama vya upinzani vimejikita kuwapiga vta wanaharakati na wakosoaji wa Serikali. Masuala nyeti ya kitaifa wanafumba mdomo
 
Tatizo jina litakatwa kwenye kura za maoni.
CCM siyo wapumbavu kama mnavyofikiria. Wanaangalia upepo, kanda ya ziwa imani imeshuka, washafanya tathmini, jjii wa Naibu PM na paulo.
Kama kukatwa jina angekatwa Nape kipindi alichomsema JPM ikavuja. Mnavyowafikiria CCM sivyo walivyo, wanajibadilisha sana kama.kivyonga kulingana na upepo wa kisiasa
 
Back
Top Bottom