Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Kwa bandari aambiwe hapana. Kama Waarabu wamempa masharti, aachane nao.Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.
Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?
Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.
Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.
--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.
Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.
Tuache utani. Maswala ya ubia yakishatuangusha sana.
Nilishasema hapa haya ndio matokeo ya mikopo, misaada na kijipendekeza.