You hit the nail on the head. Yote uliyosema ni kweli tupu. Nakubaliana pia na wengi wa wachangiaji wa uzi huu. Kwa mfano kwenye Uzi #5 Mlaleo anasema 'we are moving backwards'. Kwenye Uzi #8 Vyamavingi anakejehi kwa kusema 'tupate pia mbia wa kuiendesha Serikali'. Kwenye Uzi #11 KeyserSoze anasikitika kwamba 'ufunguaji wa nchi unapitiliza kiasi'.
Tujikumbushe historia. Miaka ya 80 Rais Mwinyi alitamka kwamba kwa kuwa Hoteli ya Kilimanjaro inafanya kazi kwa hasara, tuwape kampuni ya kigeni waiendeshe. Waandishi wa habari wakaenda kumhoji Timothy Kasela, aliyekuwa Mkurugenzi wa shirika la utalii, ambalo hoteli hiyo ilikuwa chini yake, kuhusu kauli hiyo ya Rais. Yeye akasema kufanya biashara kwa hasara kwa Kilimanjaro si kwa sababu ya wafanyakazi wabovu wa Kitanzania. Badala ya kuwapa wageni hoteli waiendeshe, wawape ardhi wajenge hoteli yao ili tuone kama watatengeneza faida. Hiyo ilichukuliwa kama 'insurbodination' kusema kitu kinyume na alivyosema Rais. Kasela alisimamishwa kazi kwa karibu mwaka mzima 'uchunguzi' ukifanywa. Baada ya hapo, akafukuzwa kazi.
Mfano wa vitu ambavyo vilikuwa vikitia hasara Kilimanjaro ni kwamba ufuaji wa nguo wa hoteli ya Africana ulikuwa ukifanyika Kilimanjaro. Hoteli zote mbili zilikuwa zimepewa mwendeshaji mmoja ambapo mwenye mali Africana ilikuwa kampuni ya binafsi ambapo Kilimanjaro ilikuwa ya Serikali. Matumizi yanakwenda Kilimanjaro, mapato yanakwenda Africana. Mwisho Serikali iliamua Kilimanjaro iuzwe kabisa; kwanza kwa Hilton, Sheraton, etc. Kwa hiyo tulikuwa na Kempinski Kilimanjaro Hotel na sasa hoteli inaendeshwa na Hyatt Regency Hotels tangu 2012. Kila mwendeshaji aliyepewa alikuja na mbinu zake za kuiba mpaka miaka mitano ya nafuu ya kodi inapita halafu anaiuza.
Tuliona pia ubia ulioingiwa na ATC na South African Airways jinsi tulivyokuwa tukipigwa. Serikali ikagutuka mkataba ukasitishwa. Tukaingia ubia mwingine wa watatu: ATC, Uganda Airways, na kashirika kadogo ka ndege ka Afrika Kusini. Ubia huu ukadumu kwa kama mwaka mmoja tu. Mapungufu yakagundulika na kuufuta ubia huo.
Tukaingiza TRC ubia na Wahindi waendeshe treni zetu. Haukupita muda tukagundua tunaibiwa. Tukasitisha ubia.
Sasa tunataka ubia wa kuendesha bandari. Mifano niliyoitaja hapo juu inatosha kutukanya kwamba ubia si kwa manufaa yetu. Tujiulize kwanza wapi tunakwama kunakosababisha tusitengeneze faida inayopaswa? Jee, ni ukosefu wa utaalamu, au uwekezaji mdogo, au ni kitu gani hasa? Tukigundua hilo, hapo ndipo tuchukue hatua zipaswazo. Tusikimbilie kuingia ubia. Labda tuanzie kwanza kuingia ubia wa kuendesha Serikali na baadaye ndiyo tufikirie kuingia ubia kwenye kuendesha bandari.