Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Duh, hatari.
Wale wa ATC na TRC ilikuwaje vile? Hatujifunzi tu?

Serikali inawekeza mabilioni ya miundombinu halafu bado inatafuta mwekazaji . Kwa nini mwekeAjichuyo asiwekezeckwanza ndo anendeleea na ubia
 
Nchi unaiuza unamuuzia nani? Hii lugha ya "kuuza nchi" ni ya kijinga sijapata kuona.

Bandari ni chanzo kikubwa sana cha fedha, hususan kwa geography ya Tanzania. Kama tunashindwa kuiendesha wenyewe na tunashindwa kiasi nchi zote zinazoitegemea bandari yetu zinaihama kwenda kutumia bandari za nchi jirani halafu bado tunaiuza nchi? Kuiuza nchi ni huko kutokuwa na watendaji waadilifu, wanatumaliza huku tunajiona, tusijikaze kisabuni, ni wakati muafaka tuwape wanaoweza kuiendesha/kuziendesha bandari zetu kwa faida ili nchi ifaidike.

Namuunga mkono Mama Samia kwenye hili kwa 100% tena tumechelewa sana kufanya hivyo. Serikali ibaki tu kuwa "facilitators" biashara tuwache zifanywe na wanaoijuwa biashara.

Tusifanye mambo yetu kwa "feelings" tufanye mambo yetu kwa "reality".
Tatizo linakuja watakaopewa kuendesha hizo bandari ndio hao hao waliokuwa kwenye menejimenti na wakafeli unategemea lipi jipya hapo.
 
Hapo unamaanisha sisi Kama nchi hatuna kabisa akili.
Kama hayo mashirika tu tumeshindwa kuyaongoza basi sisi ni maiti zinazotembea


😄 Halafu najiuliza hao wataalamu wote serikalini baada yakumpa mbia watakuwa na kazi gani…kupanga mafile?!
 
Hayo yote yamefanywa na ninyi CCM kuanzia baba yako mpaka wewe mwenyewe
ndio umekuja kuiuza Tanzania kabisa sijui unampango wa kuishi Omani
ukishaiuza.
Hivi ninyi hamna akili za kufikiri mpaka mnarudia mataptap yaliyo kwisha feli?
Nyie ni wezi hamna nia njema na hili taifa.
Kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho hamta dumu kwenye hii dunia.
Mtu umebakiza chini ya miaka 30 ya kuishi lakini unaiba kama utaishi milele,
wakati ukubwa wa kaburi lako halizid futi sita na hutaondoka na chochote.
Au ndio mnaponda raha kufa kwaja?
Yaaah, tuliiba fedha za Watanzania tukaenda kujenga International Airport Chato. Usisahau hilo.
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Kama tumeshindwa kwenye Madini na Utalii ambapo tunawabia bandari ndio itatupa robo tatu ya mapato ya bajeti?

Hebu tuache michezo hii. Angefanya maamuzi haya kwa TANESCO ningemueleza zaidi
 
ccm bhna mnamatatz
CCM au Chadema, haijalishi. Vyama vyote hivyo unavyoviita vya upinzani vilianzishwa Ikulu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Viivyomaliza kazi yake unaona vimebaki mabango tu, na vilivyobaki vikimaliza kazi zake ni hayo hayo tu.

Usijidanganye kuwa Tanzania kuna upinzani wa kweli, ni Simba na Yanga tu.
 
Hakuna cha kulaaniwa wala majungu ni kuendekeza ujinga na njaa tu. Ni kutunga kanuni za kumtimua na kumfilisi kila atakayebainika kuleta ujinga kwenye Mashirika ya umma. Wangeacha kupongezana pale mtu anapopewa utezi katika mashirika ya umma.

Magufuli alikuwa anafanya hivyo ila wapembe wakadai alikuwa anasingizia watu kesi sijui mara ni dictator ,hafuati utawala bora na kilele za kadai katiba zikaongezeka , watanzania ni wahuni sana
 
CCM au Chadema, haijalishi. Vyama vyote hivyo unavyoviita vya upinzani vilianzishwa Ikulu ya Mzee Ali Hassan Mwinyi.

Viivyomaliza kazi yake unaona vimebaki mabango tu, na vilivyobaki vikimaliza kazi zake ni hayo hayo tu.
Kuna raisi failure hapa Tanzania kama Zumaridi na huyo mzee?
 
Tatizo linakuja watakaopewa kuendesha hizo bandari ndio hao hao waliokuwa kwenye menejimenti na wakafeli unategemea lipi jipya hapo.
Hapana. Itapewa kampuni ya nje yenye vigezo vya kuendesha bandai kama vile zinavyoendeshwa Dubai, Singapore, Hongkong na kwengineko. Dunia ya leo si ya jana.
 
Kama yeye Rais anamteua Polisi mstaafu kuwa mwenyekiti wa bodi ya Bandari.

Hivi tutarajie miujiza gani hapo?

Au ndio mkakati wa kuididimiza Bandari yetu zaidi?

Ikumbukwe kwamba ukiishaingia mikataba leo haitakuwa rahisi kuja kuwaondoa huko mbeleni.

Hata iwapo wanaendelea na madudu yao.

Magu alinajisi uchaguzi akajaza wawakilishi wa ccm bungeni, wala usijali hao wabunge wa ccm kwa wingi wao maana ni wazalendo watapinga mkataba huo.
 
Kama yeye Rais anamteua Polisi mstaafu kuwa mwenyekiti wa bodi ya Bandari.

Hivi tutarajie miujiza gani hapo?

Au ndio mkakati wa kuididimiza Bandari yetu zaidi?

Ikumbukwe kwamba ukiishaingia mikataba leo haitakuwa rahisi kuja kuwaondoa huko mbeleni.

Hata iwapo wanaendelea na madudu yao.
Huo ulikuwa worst ever uteuzi duniani, worst uteuzi katika Karne hii, mama sijui kama Yuko sawa, huo ndio uteuzi ulinifanya niamini tuna boya liko Ikulu.
 
Tumefanya hivyo kipindi Cha mwinyi, tukashindwa, tukafanya hivyo kipindi Cha mkapa tukashindwa, tukafanya kipindi Cha JK tukashindwa.
Kipi kimebadilika sasa tusishindwe? Juzi tu hapa raisi na jopo zima waliingizwa kwenye mkataba wa kinyonyaji hapo bandari na kampuni hewa
Nyakati zote ulizozitaja waliingia ubia na watu ambao hawakustahili ! Reli walipewa wahindi ambao watu wakasema ni wahindi wa kariakoo !! Yaani kwa muonekano wao tu walionekana kuwa ni choka mbaya ! Sasa hapo unategemea nini ? Unataka kuingia ubia watafuteni wale munaowaita mabeberu waje waongoze hiyo bandari uone itakavyokua, lakini ukawape watu kama Richmond ya umeme yule mhindi alikuwa na kiofisi cha internet pale kariakoo nyuma ya Keys Hotel eti ikasemekana ni kampuni ya kutoka marekani !! Salaalee!! Kwa kweli tunafanya utani na Nchi !! Ingieni ubia na mabeberu wanaotambulika kimataifa kazi itafanyika !!
 
Jambo lakujiuliza,NI wapi Bandari imeshindwa kujiendesha? Mpaka impelekee MH Mama Samia anataka kuitafutia MBIA. Maana nijuavyo Mimi mpaka hapa Leo haya yanayokea Bandari haijawahi kujiendesha kihasara. Wala haijawahi kukwama kupeleka Ruzuku Serikalini. Au mama kasahau Bandari ilipelwka Gawiwo kumahinda mashitika yake yote? Mama kaa Chini tafakari kwanza kabla ya maamuzi
 
-Bandari zetu, kuingia ubia,ili iweje tunakwama wapi watanzania.
-Serikali iache utaratibu wa kupeana nafasi kwa kujuana
-Serikali ichague watendaji wa Taasisi zake kwa kufuata weledi na kuzhindanishwa -Serikali iache utaratibu wa kuweka Menejimenti kwa kujuana.
-Nafasi za menejimenti zishindanishwe na watanzania wenye uwezo wapewe fursa ya kuongoza,
-Serikali isitegemea kupata tija kwa kuingia ubia.(rejea ubia wa Serikali /ATCl/TRC/TANESCO etc)
 
Back
Top Bottom