Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

SIO BANK tu taasisi nyingi ambazo zinaendeshwa binafsi kwa asilimia kubwa hufanya vizuri, serikali ikashakua tu na hisa nyingi tatizo huanzia hapo
Ndio tujiulize kwa nini mashirika ya kiserikali hayafanyi vizuri?
Watu wengi wanafikiria kupiga dili za kujitajirisha huko ! Kwa watu binafsi sio rahisi kupiga dili huko !!
 
Tatizo kubwa ni usiri wa maamuzi na mikataba hivi vitu ni hatari sana. Tulishapigwa mara nyingi sana na sasa tuna hatari ya kuingizwa tena kwenye mkataba wa hovyo. Kwanini tusiajiri baadhi ya wataalamu kutoka nchi zenye kuendesha bandari zao kwa ufanisi tukawalipa vizuri wakaja kuwa Train vijana hapo Bandarini? Singapore, Hong Kong nk. Inanuka vibaya hii kitu, kina Bakhre wanataka kuchukua bandari nini? Hapa lazima kuna kitu kimefichwa. Lazima kuna jambo si hivi hivi, time will tell.
 
Yani huu ndo ukweli mtupu.wanapanga kuludisha nchi nyuma .watu wamepambana kukuza bandari wao wanagawana kila kitu..
 
Kwamba sisi wenyewe tumeshindwa kabisa,,,, tunamleta mtu wa nje aje ajichukulie mafeza kadri ya urefu wa kamba yake...

Mtanzania ukitegemea wanasiasa,, hakika utakufa mapema sana
 
Mbia wa nini? kwanini wasitafute CEOs wenye uzoefu mkubwa waliowahi kuendesha bandari kubwa za kueleweka kama Amsterdam, New York etc nina uhakika wapo na wanaweza kunyoosha hiyo bandari kwa mshahara tuu bila ubia
Unawajua watz kwa fitina lkn atapigwa majungu ata kurogwa ili atoke hapa mwarobaini Ni kutafuta mbia tu.
 
Hujaelewa kwasababu hukubaliani na hoja yangu. Huyo mama kwa hili la kubinafsisha bandari ya Dar asijaribu maanake tutakua tumeuza nchi .
Nchi unaiuza unamuuzia nani? Hii lugha ya "kuuza nchi" ni ya kijinga sijapata kuona.

Bandari ni chanzo kikubwa sana cha fedha, hususan kwa geography ya Tanzania. Kama tunashindwa kuiendesha wenyewe na tunashindwa kiasi nchi zote zinazoitegemea bandari yetu zinaihama kwenda kutumia bandari za nchi jirani halafu bado tunaiuza nchi? Kuiuza nchi ni huko kutokuwa na watendaji waadilifu, wanatumaliza huku tunajiona, tusijikaze kisabuni, ni wakati muafaka tuwape wanaoweza kuiendesha/kuziendesha bandari zetu kwa faida ili nchi ifaidike.

Namuunga mkono Mama Samia kwenye hili kwa 100% tena tumechelewa sana kufanya hivyo. Serikali ibaki tu kuwa "facilitators" biashara tuwache zifanywe na wanaoijuwa biashara.

Tusifanye mambo yetu kwa "feelings" tufanye mambo yetu kwa "reality".
 
Huenda walijifunza kutokana na makosa ya kipindi hicho.
Nipe mfano wa project mojawapo iliyofanikiwa.

Unaimwakumbuka Net solution na Tanesco? Kwanini tulivunja mkataba? Unajua watu waliokuwepo kipindi kile ndo hao hao wenye sauti mpaka Leo?
 
Lobists watampoteza sana mama. Mama asaidiwe.
 
Masuala ya ubia hayajawahi kufanikiwa nchi hii.
 
Jambo lakujiuliza,NI wapi Bandari imeshindwa kujiendesha? Mpaka impelekee MH Mama Samia anataka kuitafutia MBIA. Maana nijuavyo Mimi mpaka hapa Leo haya yanayokea Bandari haijawahi kujiendesha kihasara. Wala haijawahi kukwama kupeleka Ruzuku Serikalini. Au mama kasahau Bandari ilipelwka Gawiwo kumahinda mashitika yake yote? Mama kaa Chini tafakari kwanza
 
ccm bhna mnamatatz
 
Lete usha
Lete ushaidi wa uliloandika kama huna chuki binafsi .mwanzo kama nilianza kukuelewa lkn hapa si sawa.changamoto za uendeshaji wa bandari TPA inashindwa kutokana na vitu kadha wa kadha
gharama za ukarabati
tekinologia ya kisasa
ushindani uliopo kwenye bandar za Africa n.k
ebu lete nn kifanyike sio kama unaleta chuki binafsi
 
Wale jamaa wameshaingiza mabega tayari. Wacha tupigwe na kitu kizito
 
Nyie watumishi wa Umma mnaenda Lunch masaa ma 3 mtaweza kujifananisha na private sector tukikamata bandari
 
Hayo yote yamefanywa na ninyi CCM kuanzia baba yako mpaka wewe mwenyewe
ndio umekuja kuiuza Tanzania kabisa sijui unampango wa kuishi Omani
ukishaiuza.
Hivi ninyi hamna akili za kufikiri mpaka mnarudia mataptap yaliyo kwisha feli?
Nyie ni wezi hamna nia njema na hili taifa.
Kitu kimoja ambacho nina uhakika nacho hamta dumu kwenye hii dunia.
Mtu umebakiza chini ya miaka 30 ya kuishi lakini unaiba kama utaishi milele,
wakati ukubwa wa kaburi lako halizid futi sita na hutaondoka na chochote.
Au ndio mnaponda raha kufa kwaja?
 
Kweni sout

South Africa, Kenya, ethiopia Egypt wao wanaendeshaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…