Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Binafsi sijaelewa vizuri, Ila unahisi kwa nini hizo kampuni nzuri hazikuwahi kuja?
 
Huyo mbia atafanya nini ikiwa hao watu bado wapo? Si itakua Kama ilivyokua atcl, Tanesco na wengine?
 
Ipo siku nchi itapigwa mnada.
( nimekosa mimi nimekosa sana)
 
Umechanganua vizur sana mkuu
 
KWa mtazamo wangu; sheria ya kuchapa viboko wafanyakazi wazembe hasa kwenye sekta nyeti bora INGERUDI; Bandari, TRA, BOT, ATCL nk tukianza na hao watu hakika tutasogea mbele; watu wamesoma hadi mwisho wa vyeti but kusimamia vitu vidog vidogo tu hawawezi, JINGA kabisa
 
Hata ulichoandika pengine wewe mwenyewe hujaelewa.

Kuendesha kwa ufanisi Wala halihitaji mbia, tumewahi kufanya ubia karibu mashirika yote makubwa na tulishindwa, yapo yaliyokufa na yapo yaliyobaki na madeni makubwa
 
Hufahamu yaliyofanyika huko, labda ulikuwa mdogo sana.
Mm niwe mdogo kwenye hayo mashirika? Ikiwa nilikua nafanya kazi sehemu mojawapo?
Ni kipi kilifanyika Tanesco,trl na ATCL tulipokabidhi kwa wabia?
Hii inahitaji uwe na akili kujua kilichofanyika?
 
😂, kumbe hata Chamvino tunaweza kuwa na mbia.
 
Binafsi sijaelewa vizuri, Ila unahisi kwa nini hizo kampuni nzuri hazikuwahi kuja?
Mazingira ya uwekezaji Tanzania ni magumu sana hayavutii mpaka kwenye visa za kazi tu ni gharama kubwa na tax ni kubwa sana Tanzania mazingira sio rafiki na kubwa zaidi hatuna mwendelezo wepesi wa kuvunja mikataba kwa pressure tu angalia kama kina Dangote wanapata tabu kufanya biashara Tanzania, makampuni makubwa yatakuja tu kukiwa na sera imara sio unakuta RC tu anamtia pingu mwekezaji bila sheria kufuatwa haya mambo hayakubaliki. Sera za biashara ziwe haziingilani na siasa za ndani biashara kitu kingine na siasa kingine.
 
Hizi unazoeleza hapa ni theories, kampuni haziji sio sababu ya sera au RC sijui kafanyaje. Haziji kwa kuwa wanashindana kwenye maslahi, ni Hilo tu.
Kuna kampuni kubwa zimewekeza pale congo, pamoja na vita kila siku.
 
Bandari ya Dar kwa sasa wangeacha utaratibu huu huu wa Sasa uendelee ila Serikali ipeleke nguvu ya ubia kwenye bandari ya Dar.

Pia Mradi wa Dart ndio unatakiwa upelekwe kwenye ubia na sekta binafsi..

Mwisho kama ni lazima ishu za ubia na bandari ya Dar iwe ni baadhi ya section zinazoleta failures
 
Mm niwe mdogo kwenye hayo mashirika? Ikiwa nilikua nafanya kazi sehemu mojawapo?
Ni kipi kilifanyika Tanesco,trl na ATCL tulipokabidhi kwa wabia?
Hii inahitaji uwe na akili kujua kilichofanyika?
Inategemea ulikabidhi vitengo gani,mbona banks zinafanya vizuri.
 
Hii kitu ni unrealistic kupata mapato robo tatu ya kuendesha bajeti ya serikali. Bajeti ya serikali kama trilioni 38-40.. Je sasa hivi bandari wana mapato kiasi gani?

Kiasi kutamani kwenda hapo?

Watatumia mbinu gani? Wataongeza ghati mpya au hizi za sasa...? Imekuwaje sasa hivi wasipate hayo mapato waje kuyapata baada ya mwekezaji mpya.?

Uzoefu umeonyesha wawekezaji huja kupata faida wao na si vinginevyo.. Kwa hiyo mwekezaji apate faida yake na aiachie au alete mapato kwa serikali kwa 75% ya bajeti.

Ni kauli ya kuvutia sana, lakini haina uhalisia... Ahadi kama hizi zimetolewa kwenye tozo mbalimbali na mpaka sasa , serikali imebidi iende ikakope kujenga mashule ... Hata kwenye mashule hatujajua kama huo uwezo zaidi wa madarasa na wanafunzi wa sekondari na msingi..Tunayo ziada ya kuendesha , hilo ni swala la siku nyingine.

Sasa kwenye bandari , kweli lipo tatizo , meli kuchelewa kuingia bandarini , meli chache kutumia bandari yetu, mizigo kidogo kutumia bandari yetu. Hivyo mapato kuwa madogo. Changamoto kama hizi zinaweza tatuliwa kwa kuongeza sehemu za kupokelea mizigo nje ya bandari , mageti ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini, hivyo kuongeza uwezo kupokea na kutoa mizigo na maeneo mengine kama bandari kavu.. Kuimarisha barabara na vivuko mbalimbali vinavyounganisha bandari zetu na nchi jirani..Mifumo ya kikodi na utendaji wa taasisi mbali mbali zinazohusika na mizigo inayoingia Tanzania ikiwemo TRA....

Haya yote yanaweza kufanyika , lakini mapato hayatoongeza kuweza kukidhi robo tatu ya bajeti ya Tanzania... Na haya yanaweza kufanyika kwa uwekezaji wa serikali kuimarisha miundo mbinu mbalimbali.... Kama haya hayafanyiki na unamuleta mwekezaji atakuja kuleta maajabu gani?

Au ndiyo yale yale , huyu anakuja anafanya yake , halafu awamu ya uongozi mwingine inakuja kubadilisha ya awamu iliyopita..

Tuwekeze kwenye miungo mbinu yetu, tuongeze uwezo wa taasisi zetu , wafanyakazi wa Kitanzania .. Hakuna mjomba atakayekuja kuleta maendeleo TANZANIA.
 
Hapo kuna kiongozi mstaafu anaitaka bandari. Tunapiga kweupe
Mkuu unakumbuka enzi za wale jamaa waliokuja kuongoza Tanesco kutoka SA. walipiga afu wakatoka nduki.
 
Hakuna haja ya mbia ila inatakiwa tuwekeze mzigo wenyewe na faida tule wenyewe sidhani hizo fedha atakakazokuja kuwekeza mbia sisi tutashindwa.
 
Tungeanza na Tanesco.
 
namkubali sana Dr msukuma kwamba wasomi wameirudi nyuma kwa kiasi kikubwa sana.sasa Ndugai walimlazimisha kujiuzuru kwa nn wkt inaonekana kabisa nchi inaenda kuuzwa kama awali?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…