Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.
Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?
Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.
Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.
--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.
Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.
View attachment 2153881
Hii kitu ni unrealistic kupata mapato robo tatu ya kuendesha bajeti ya serikali. Bajeti ya serikali kama trilioni 38-40.. Je sasa hivi bandari wana mapato kiasi gani?
Kiasi kutamani kwenda hapo?
Watatumia mbinu gani? Wataongeza ghati mpya au hizi za sasa...? Imekuwaje sasa hivi wasipate hayo mapato waje kuyapata baada ya mwekezaji mpya.?
Uzoefu umeonyesha wawekezaji huja kupata faida wao na si vinginevyo.. Kwa hiyo mwekezaji apate faida yake na aiachie au alete mapato kwa serikali kwa 75% ya bajeti.
Ni kauli ya kuvutia sana, lakini haina uhalisia... Ahadi kama hizi zimetolewa kwenye tozo mbalimbali na mpaka sasa , serikali imebidi iende ikakope kujenga mashule ... Hata kwenye mashule hatujajua kama huo uwezo zaidi wa madarasa na wanafunzi wa sekondari na msingi..Tunayo ziada ya kuendesha , hilo ni swala la siku nyingine.
Sasa kwenye bandari , kweli lipo tatizo , meli kuchelewa kuingia bandarini , meli chache kutumia bandari yetu, mizigo kidogo kutumia bandari yetu. Hivyo mapato kuwa madogo. Changamoto kama hizi zinaweza tatuliwa kwa kuongeza sehemu za kupokelea mizigo nje ya bandari , mageti ya kuingiza na kutoa mizigo bandarini, hivyo kuongeza uwezo kupokea na kutoa mizigo na maeneo mengine kama bandari kavu.. Kuimarisha barabara na vivuko mbalimbali vinavyounganisha bandari zetu na nchi jirani..Mifumo ya kikodi na utendaji wa taasisi mbali mbali zinazohusika na mizigo inayoingia Tanzania ikiwemo TRA....
Haya yote yanaweza kufanyika , lakini mapato hayatoongeza kuweza kukidhi robo tatu ya bajeti ya Tanzania... Na haya yanaweza kufanyika kwa uwekezaji wa serikali kuimarisha miundo mbinu mbalimbali.... Kama haya hayafanyiki na unamuleta mwekezaji atakuja kuleta maajabu gani?
Au ndiyo yale yale , huyu anakuja anafanya yake , halafu awamu ya uongozi mwingine inakuja kubadilisha ya awamu iliyopita..
Tuwekeze kwenye miungo mbinu yetu, tuongeze uwezo wa taasisi zetu , wafanyakazi wa Kitanzania .. Hakuna mjomba atakayekuja kuleta maendeleo TANZANIA.