Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Watanzania acheni kulialia nchi inafunguliwa mnaendelea kulalamika why?.

Issue ya kuwapa watu sector muhimu ilikwepo na matokeo yake yanafahamika ila mlilia mambo magumu sasa yanarahisishwa mnalalamika WHY?.
 
Katika hili sikubabliani naye kama ni kweli kwasababu huko nyuma, approach hii ilifeli kwa Tanesco na Air Tanzania na Mashirika mengine. Kitu ambacho ningekubaliana naye ni kupata CEO yeyote na kutoka popote duniani asimamie Bandari kama wamatumbi tumeshindwa. Si lazima awe mmatumbi akaishia kuweka wapwa zake na kuharibu kazi.
 
Aiseee! Kuna siku tutatafuta mbia wa kuiendesha serikali maana tumeshashindwa kuiendesha bandari.

Ili bandari ifanye vizuri zaidi inatupasa kuachana na siasa kwenye uendeshaji wake Menejimenti ya Bandari iwekewe malengo na wasiingiliwe na serikali.

Kuwe na mkataba baina ya serikali na menejimentj ya TPA, iwapo watashindwa kufikia malengo yaliyowekwa kwa kila robo mwaka basi kibarua kinaota nyasi na iwapo kuna jinai sheria ichukue mkondo wake.

Nadhani tuanzie hapo.

Vv
Haya unayosema yafanyike nchi gani? Raisi aligundua kasainishwa mkataba mbovu, kawafanyaje waliofanya hivyo?
 
Hii haipo sawa. Waziri husika na wataalamu wake Planners wa wizara wote kazi yao haswa ni nini? Mishahara ya mamilioni wanalipwa kwa ajili gani?. Kwamba nchi haina wataalam kabisa wa kuendesha bandari kwa ufanisi na tija?
Hii ndio sehemu ambayo waziri alipaswa kupimwa utandaji wake kwa kusimamia baandari. Ni Kama tunavyompima waziri wa nishati kwenye Tanesco. Ila. Ndio hivyo
 
mi naona si bandari tu bali tuwarudishe Waingeleza watusaidie kutuwekea mifumo mizuri kwa mkataba maalum wa miaka 5 tu, maeneo ya kuwakabidhi yawe ni:-
1. Utawala bora
2. Usafirishaji
3. Viwanda
4. Kilimo
5. Elimu
6. Majeshi.
7. Afya
 
Katika hili sikubabliani naye kama ni kweli kwasababu huko nyuma, approach hii ilifeli kwa Tanesco na Air Tanzania na Mashirika mengine. Kitu ambacho ningekubaliana naye ni kupata CEO yeyote na kutoka popote duniani asimamie Bandari kama wamatumbi tumeshindwa. Si lazima awe mmatumbi akaishia kuweka wapwa zake na kuharibu kazi.
Hata akija huyo CEO akikaa hapo atapigwa majungu hadi ataondoka mwenyewe, tumelaaniwa
 
mi naona si bandari tu bali tuwarudishe Waingeleza watusaidie kutuwekea mifumo mizuri kwa mkataba maalum wa miaka 5 tu, maeneo ya kuwakabidhi yawe ni:-
1. Utawala bora
2. Usafirishaji
3. Viwanda
4. Kilimo
5. Elimu
6. Majeshi.
7. Afya
Tuwe na raisi Hadi mawaziri waingereza. Ila hawa kina mwigulu na January???? Alafu tunatemea maendeleo
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.
Kwa hali ilivyo naunga mkono hili la kuleta mbia, yaani meli zinakaa nje kusubiri nafasi kwa siku 23! Nani ataleta meli zake DSM? Tena tumechelewa sana sana na ni aibu!
 
Hakuna cha kulaaniwa wala majungu ni kuendekeza ujinga na njaa tu. Ni kutunga kanuni za kumtimua na kumfilisi kila atakayebainika kuleta ujinga kwenye Mashirika ya umma. Wangeacha kupongezana pale mtu anapopewa uteuzi katika mashirika ya umma.
Hata akija huyo CEO akikaa hapo atapigwa majungu hadi ataondoka mwenyewe, tumelaaniwa
 
Kwa hali ilivyo naunga mkono hili la kuleta mbia, yaani meli zinakaa nje kusubiri nafasi kwa siku 23! Nani ataleta meli zake DSM? Tena tumechelewa sana sana na ni aibu!
Shida bado ipo pale pale, tuliwahi kufanya hivyo kwenye reli, shirika la ndege, Tanesco na bado kotr huko tulichemsha . Tena hayo yakifanyika kipindi tunasema raisi alikua na wataalamu
 
Back
Top Bottom