Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Kama tunatafuta mbia wabkuendesha Bandari kwa nini na Ikulu tusitafute mbia
Naamini hata hapo Ikulu tunaweza kufanikiwa zaid.
Tulifanikiwa sana tulipotafuta mbia wa kuendesha
Airport.
Ttcl
Dawasa
.....
Tuwalete tu hao wabia
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Duuuh, yaani mtu aje aendeshe engine ya nchi yetu?! Tumechanganyikiwa?!! Hawa waarabu wa UAE watachukua kila kitu awamu hii
 
Hapana, hawa hatuwataki. Tunataka "mbia" wa kwelikweli anayetoka Arabuni, China au Beberu kabisa. Hawa wababaishaji wenzetu ni wapiga dili tu!
Serikali inatakiwa itafute mbia wa kwelikweli kuendesha shughuli zake. Hawa waliopo wote wameshindwa.
Litakuja kampuni la kichina linaitwa Liugong kumbe fake na mmiliki Ni Mimi hahahahahaaaa

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Ongea ueleweke, wacha kuongea kwa mafumbo kwenye mitandao ya kijamii, usifikiri kila mtu anaeingia na kusoma JF anaweza kusoma mawazo yako.
Hujaelewa kwasababu hukubaliani na hoja yangu. Huyo mama kwa hili la kubinafsisha bandari ya Dar asijaribu maanake tutakua tumeuza nchi .
 
Naunga hoja na tumchelewa sana.mbongo kuendesha makampuni ya umma hatuna uzalendo.ni heri tu tubinashishe tuwe tunachukua kodi kila mwezi
 
Hivi hata yeye sianaweza kuwa mbia au haiwezekani naomba kuelimishwa.
 
Vitabu vitakatifu vyeke Muumba wa mbingu na nchi vinasema mwanamke lake jiko, ukiona hujaelewa achananayo.
 
Naunga hoja na tumchelewa sana.mbongo kuendesha makampuni ya umma hatuna uzalendo.ni heri tu tubinashishe tuwe tunachukua kodi kila mwezi
Hapo unamaanisha sisi Kama nchi hatuna kabisa akili.
Kama hayo mashirika tu tumeshindwa kuyaongoza basi sisi ni maiti zinazotembea
 
Hapo tayari atakuwa kashapatikana, wanapima upepo tu
Ten percent ya udalali
Hiyo imeshaisha tayari, kumbuka ishu ya tozo ilianza na Zungu kama utani,,, angalia ishu ya ngorongoro kama utani vile lakini ndio ushaambiwa nyumba zishaanza kujengwa huko handeni.
 
SIO BANK tu taasisi nyingi ambazo zinaendeshwa binafsi kwa asilimia kubwa hufanya vizuri, serikali ikashakua tu na hisa nyingi tatizo huanzia hapo
Ndio tujiulize kwa nini mashirika ya kiserikali hayafanyi vizuri?
Kama unajua uchumi utaelewa sababu.
 
Ukipima ufanis wa TICTS na TPA, TICTS wapo mbele sana kwenye huduma zao richa ya mapungufu waliyonayo. Ndugu zangu TPA wamelala sana, wamebweteka.

Sijui ni nani aliyetuloga.
 
Naunga hoja na tumchelewa sana.mbongo kuendesha makampuni ya umma hatuna uzalendo.ni heri tu tubinashishe tuwe tunachukua kodi kila mwezi
Ni Hivi Serikali inakula Chake / Kodi
Muwekezaji anakula Chake Faida
Pesa inatoka kwa mtuamiaji i.e. Mteja

Sasa kama wateja wapo na hawajapungua na tunaongeza mtu kati ili tugawane faida unategemea ni nini kitatokea ? (Mapato kuongezeka bila kuongeza Bei)?

Je ni kwamba kama taifa tumeshindwa kuweka unangalizi na kusimamia pesa na kudhibiti wizi ili tupate faida yote ?, Au tunahitaji uwekezaji mkubwa wa mtaji ? Is this Rocket Science..., Kama tunashindwa hata hiki, Kusimamia mizigo inayoingia ambayo ni lukuki tumezungukwa na land locked countries (je tunaweza nini )?

Kwanini hao wawekezaji tusiwapeleke huko in the middle of nowhere ili waanze kuwekeza from scratch ? Yaani tuwape vitu kwenye silver platter ?
 
Back
Top Bottom