Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Sakata la DP WORLD: Rais Samia asema Serikali itatafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar, sasa kuchangia robo tatu ya bajeti ya nchi

Nyakati zote ulizozitaja waliingia ubia na watu ambao hawakustahili ! Reli walipewa wahindi ambao watu wakasema ni wahindi wa kariakoo !! Yaani kwa muonekano wao tu walionekana kuwa ni choka mbaya ! Sasa hapo unategemea nini ? Unataka kuingia ubia watafuteni wale munaowaita mabeberu waje waongoze hiyo bandari uone itakavyokua, lakini ukawape watu kama Richmond ya umeme yule mhindi alikuwa na kiofisi cha internet pale kariakoo nyuma ya Keys Hotel eti ikasemekana ni kampuni ya kutoka marekani !! Salaalee!! Kwa kweli tunafanya utani na Nchi !! Ingieni ubia na mabeberu wanaotambulika kimataifa kazi itafanyika !!
Sio kweli, hili taifa tuna laana. MSI ni waholanzi na Ni kampuni kubwa ya kibeberu Ila si tulipigwa TTCL mchana kweupe
Barrick nayo ni kampuni kubwa sana ila si unaona kwenye madini washatushinda.
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Hapa hatuna kiongozi, huyu tumepigwa mwanzoni nilikuwa namuona wa maana ila kwangu mimi ameshindwa mapema sana, hatutakiwi kufanya kosa tena, huu muda umemtosha.
 
Katika hili sikubabliani naye kama ni kweli kwasababu huko nyuma, approach hii ilifeli kwa Tanesco na Air Tanzania na Mashirika mengine. Kitu ambacho ningekubaliana naye ni kupata CEO yeyote na kutoka popote duniani asimamie Bandari kama wamatumbi tumeshindwa. Si lazima awe mmatumbi akaishia kuweka wapwa zake na kuharibu kazi.
Kwa style hiyo, ni vizuri pia Rais na Mawaziri watafutwe kutoka popote duniani. Ni vigumu kuamini kuwa nchi yenye watu milioni sitini hakuna mtu aneyezea kuongoza bandanri, tatizo ni kuwa ni la nani mwenye ukaribu na wenyewe (kulingana na Nape) anayezea kuongoza Bandari. Kwa Bahati mbaya wenye ukaribu huo wote ni bogus. Tungesema CEO ni mtu atakeyomba kazi hiyo, kufanyiwa interview na kamati maalumu ya wataalamu, na kuajiriwa kwa contract. lakini hii ya kuteuliwa kutokana na marafiki na jamaa zao ni utani mtupu.

Kuteuliwa kwa Makamba kushika nafasi ya Kalemani au kuteuliwa kwa Riziwani kushika nafasi kama ya Lukuvi ndiyo jokes zenyewe hizo. Lakini unfortunately hao ndio wenyewe.
 
Kwani mbia wa kuendesha DART kapatikana? Mpaka tunakimbilia majini.
 
Unawajua watz kwa fitina lkn atapigwa majungu ata kurogwa ili atoke hapa mwarobaini Ni kutafuta mbia tu.
Mbia tutaishia kupigwa tuu kama experience inavyoonyesha akishajua weakness za wabongo atawanunua wote wanaohusika na kutukomba kila kitu, CEO at least unamlipa akufanyie kazi akishindwa unafukuza na hamgawani chochote zaidi ya mshahara na bonus yake,kutafuta CEO mzuri ndio makampuni yote makubwa ya wazungu wanachofanya, ndio maana CEO mshahara analipwa hata 20 milion dollars na mara nyingi inaenda na perfomance, naamini CEO mzuri na timu yake wanaweza kuinyosha hiyo bandari mpaka ukashangaa ila siasa zikae mbali na wapewe freedom ya kufanya kazi bila kuingiliwa na wahuni serikalini
 
Hii chuki itakufanya ukose mbingu, angalia dada yangu...Nilikuwa nakuamini sana enzi hizo kwa balanced opinion; haya ya siku hizi daah!
Rudia kunisoma halafu onesha kipi cha chuki na kipi cha uongo hapa...

Eehh kweli kabisa, tukapeleka na Airport ya Kimataifa Chato, sasa wanatua mbayuwayu tu. Tukawaibia na majumba na magari yao matajiri. Tukawatolea bastola kuwatisha mawaziri hadharani waliposema ukweli. Tukafumua utawala wa bandari na kuweka "The" gang ndiyo waiendeshe. Usiyasahau yote hayo.
 
This is long overdue. Sio bandari tu hata mashirika mengine ya umma yaendeshwe na wabia wenye ujuzi wa hizo kazi. Ukienda bandarini, TRA, Tanesco nk ni uozo mtupu. Kitu cha dakika 2 nchi zingine bongo utafanya mwezi mzima na rushwa juu.

USA Kuna toll roads na taasisi zingine zinazoendeshwa na makampuni binafsi kwa faida ya umma. Serikali haiwezi kuendesha Kila kitu kwa ufanisi.
 
Kuteuliwa kwa Makamba kushika nafasi ya Kalemani au kuteuliwa kwa Riziwani kushika nafasi kama ya Lukuvi ndiyo jokes zenyewe hizo. Lakini unfortunately hao ndio wenyewe
Huwa sipendi kuongea vitu au kumsifia mtu au kumchikia mtu bila sababu. Nini shida ya kimsingi ya Ridhiwani na Makamba? Kama shida ni watoto wa viongozi, je ni mtoto gani wa kiongozi wa nchi hii ambaye hakuteuliwa uongozi huko nyuma. Why only Ridhiwani na January? Tuna Geoffrey Pinda, tuna akina Mwinyi, tuna Malima, tumekuwa na watoto Kawawa, watoto wa Nyerere. Nk nk.

Uendeshaji wa Bandari au mashirika ya umma ni suala la utaalam, tofauti na urais. Unaposema hata viongozi wa kisiasa tuwatoe popote duniani huko ni kutoitendea haki akili yako. Duniani kote kwa nchi zinazojielewa, hakuna mipaka kwa wataalam flaniflani. Hata kagame hapo mnaemsifia humu kila uchao hiyo model ameitumia na imeleta mageuzi. Usilinganishe nafasi za kitaalam na nafasi za kiuongozi wa nchi.
 
Siku hizi bandari zote kubwa duniani zinaendeshwa kibiashara. Kuna makampuni mahsusi yaliobobea kazi hizo.

Kuingia ubia ndio njia sahihi kwa dunia ya leo.

Nnamini bandari ya Dar ilivyokaa vizuri geographically, na nchi landlocked zinavyotuzunguka, bandai ya Dar pekee inaweza kuendesha budjet ya serikali kwa Tanzania nzima.

Nchi kama Singapore na Dubai hazina zinachojivunia zaidi ya badari zao nandio vyanzo vyao vyote vya mapato vinatokea hapo. Kwanini sisi tusindwe? Wizi mtupu banadarini Dar. Wizi wa Bandarini ni kansa iliyopo kila idara (each and every department).

Kama yalivyokufa mashirika yote umma na badari haipo salama tukiedelea kuiedesha wenyewe. Apewe tajiri mmoja aiendeshe tujionee mabadiliko.

Wala haina haja ya kuwa rocket science kuelewa kuwa bandari kwa Tanzania ina faida kubwa sana ikiendeshwa ipasavyo. Mfano mzuri ni Bagamoyo, nchi na wafanya biashara matajiri wa nje wapo tayari kuingiza na kuwekeza pesa kibao kujenga banadari na mji mpya kabisa wa kisasa, ili waingie ubia wakuiendesha bandari tu. Watafanya hivyo kama hawajaiona faida kwenye upembuzi wao?

Mama hata polisi ingia ubia iendeshwe professionally, maana imeshindwa kabisa kulinda mali za Watanzania na badala yake wanaua raia kwa thamani ndogo tu.
Unaonaje wakabidhi nchi hao matajiri ili nchi iendeshwe na wenye hela wengine tubaki kuwa wafanyakazi wa wenye pesa na urais tumkabidhi tajiri?
 
Nimeona Rais akisema Serikali kutafuta mbia wa kuiendesha bandari ya Dar es Salaam ili kuleta ufanisi na kuongeza mapato.

Ni kweli tunahitaji mbia wa kuiendesha bandari ya Dar? Sisi wenyewe imeshindikana kabisa?

Tumewahi kufanya hivi kwenye reli, shirika la ndege lakini tunajua kilichotukuta.

Hii haiwezi kuja kuiua hii bandari kwa maana tunajuana vizuri sisi hasa linapokuja suala la maslahi.

--
Rais Samia Suluhu amesema maboresho yanafanyika kwenye Bandari ya Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kupata mbia wa kuiendesha, kubadili uongozi na miundombinu ili kuongeza ufanisi.

Amesema robo tatu ya bajeti ya nchi inaweza kutegemea bandari endapo zitafanya kazi inavyotakiwa.

Sielewi hii
 
Kwa style hiyo, ni vizuri pia Rais na Mawaziri watafutwe kutoka popote duniani. Ni vigumu kuamini kuwa nchi yenye watu milioni sitini hakuna mtu aneyezea kuongoza bandanri, tatizo ni kuwa ni la nani mwenye ukaribu na wenyewe (kulingana na Nape) anayezea kuongoza Bandari. Kwa Bahati mbaya wenye ukaribu huo wote ni bogus. Tungesema CEO ni mtu atakeyomba kazi hiyo, kufanyiwa interview na kamati maalumu ya wataalamu, na kuajiriwa kwa contract. lakini hii ya kuteuliwa kutokana na marafiki na jamaa zao ni utani mtupu.

Kuteuliwa kwa Makamba kushika nafasi ya Kalemani au kuteuliwa kwa Riziwani kushika nafasi kama ya Lukuvi ndiyo jokes zenyewe hizo. Lakini unfortunately hao ndio wenyewe.
Duh!
 
Kwani Expatriates mbona tangu zamani wapo duniani kwa minajili ya kufanya kazi mbalimbali katika nchi wanazohitajika ?! Kama kuna ma- CEO wanafanya madudu katika sehemu zao basi waajiriwe Expatriates waje wafanye kazi !! Au waingie ubia na wanaotambulika kimataifa tena labda kwa msaada wa umoja wa mataifa ,
 
Back
Top Bottom