Sakata la ESCROW: IPTL na PAP Watinga Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Kisheria wa Maazimio ya Bunge

Tetty umezungumza ukweli ikulu ndipo wezi wanapofichama

Sasa wewe unataka wote waliotuhumiwa mpaka sasa wangekuwa wapo ndani how? kwa detention law ? au sharia hizi hizi maana wakati mwingine inashangaza sana mtu hana imani na mahakama za Tanzania lakini hapo hapo anataka watuhumiwa wote wawekwe ndani kwa njia ipi? kwa sababu zito kasema au bunge?
 
Hayo ni madhara ya serikali kuwekwa mfukoni!mihimili ya dola yote inawekwa mifukoni mwa mafisadi.
 
serikali ionyeshe uwepo wake wana jamii tunaona sarakasi mara sijapewa hela za PAP ,ukisikiliza upande mwingine mara sijiuzulu ,hii jeuri inatoka wapi ,wewe ni nani,umefanyia nini nchi hii hadi uote mapembe na kupanda ngazi za hoteli ya nyota kumi unakusanya watu eti sijiuzulu na mlete uthibitisho wa hizo pesa .ukiwa kama waziri wewe ni kioo cha jamii na pia ni sehemu ya serikali ,umetajwa na akaunti imethibitika hizi hadithi na jeuri na tambo zinatoka wapi ,nasisitiza kuna idara nyeti za serikali ziamke sasa waseme basi muda wa kucheza na ofisi za serikali umefika mwisho.mulongo ,tibaijuka sijui wakina ruge ,habinda wasiachwe wakitamba humu kana kwamba nchi haipo.serikali ionyeshe uwepo wake .na maamuzi ya bunge ,ripoti ya CAG ,PAC,ZIHESHEMIWE
 
Hapa dawa ni moja tu: Kuifutilia CCM mbali kwa njia ya sanduku la kura!

Naona hawa wa PAP wanatafuta kufanya kwa CCM walichokifanya kwa KANU.CCM wasipokuwa makini itakula kwao. Natoa angalizo. Naona hawajajua hili jambo linavyowakela sana wananchi.
 
Ukweli utazidi kubainika vizuri ndipo hapo tutajua kuwa PAC ni mbugila wa hali ya juu.
Hivi vichwa vya ccm bana tabu tupu,PAC inawajumbe 19,Taarifa yao imejadiliwa na wabunge zaidi ya 350 including mawaziri na makada wa ccm na mwisho kufikia maamuzi yaliyofikiwa,wewe na elimu yako ya kuunga unga unakuja na uharo hapa.
 
Mfa maji haishi kutapatapa,Maamuzi ya Bunge ni maamuzi ya Wananchi,Kikatiba hayahojiwi mahala popote pale,sio Mahakamani wala Rais anaweza kuyahoji.
 
Tusione aibu watanzania kusema mahakama yetu ni chafu.

Huku ikitambua bunge ndio muhimili mkuu tumeona kwa uchungu mahakama ikijaribu kuzuia bunge lisifanye kazi hivi majuzi ili kuwalinda wezi waliothibitika kukwapua kiwanda na mabilioni fedha ya umma. Eti sasa hao wezi wameenda tena mahakamani kuzuia maazimio ya wananchi kupitia bunge lao yasitekelezwe. Mahakama sasa imekua mwizi wa haki badala ya kutoa haki. si muda mrefu mahakama itadharauliwa kabisa jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

Mahakama imekua imewekwa ganzi kufanya haki kwa mambo ya umma na tumekua tunaona wezi na matapeli wa nchini na kimataifa wakipewa ruksa na mahakama kutia taifa kabali kutokana na hukumu za kustaajabisha.

Kuanzia richmond dowans iptl wananchi tumeshuhudia maslahi ya umma yakibwagwa mahakamani mfulilizo huku wanasheria wetu wakilipwa mabilioni kwa kushindwa kesi. sasa kwa hili la escrow tunasema wananchi kupitia wawakilishi wao wameamua. Kama mahakama ni biashara kwa escrow wameliwa na tunamuonya rais wa jamhuri kama akitetereka.

Jaji mkuu ana kazi ya kusafisha nyumba yake, hakika ni chafu kabisa
 
tusione aibu watanzania kusema mahakama yetu ni chafu. huku ikitambua bunge ndio muhimili mkuu tumeona kwa uchungu mahakama ikijaribu kuzuia bunge lisifanye kazi hivi majuzi ili kuwalinda wezi waliothibitika kukwapua kiwanda na mabilioni fedha ya umma. eti sasa hao wezi wameenda tena mahakamani kuzuia maazimio ya wananchi kupitia bunge lao yasitekelezwe. mahakama sasa imekua mwizi wa haki badala ya kutoa haki. si muda mrefu mahakama itadhagrauliwa kabisa jambo ambalo ni hatari kwa taifa. mahakama imekua imewekwa ganzi kufanya haki kwa mambo ya umma na tumekua tunaona wezi na matapeli wa nchini na kimataifa wakipewa ruksa na mahakama kutia taifa kabali kutokana na hukumu za kustaajabisha. kuanzia richmond dowans iptl wananchi tumeshuhudia maslahi ya umma yakibwaga mahakamani mfililizo huku wanasheria wetu wakilipwa mabilioni. sasa kwa hili la escrow tunasema wananchi kupitia wawakilishi wao wameamua. kama mahakama ni biashara kwa escrow wameliwa na tunamuonya rais wa jamhuri kama akitetereka. jaji mkuu ana kazi ya kusafisha nyumba yake, hakika ni chafu kabisa

usikimbie weee, andika kwa uzuri plus mpangilio (paragraph).
 
Ccm idumu milele , vyama vingine vitabana escrow kutoka ,kwa tz ccm inafaa lakini kwa wenzetu Kenya KANU iliondolewa ,ndo juzi wamepigana bungeni kutafuta haki ,lakini tz tuko vizuri tu hata baada ya kila kila kitu kuwekwa wazi , labda warioba angeshika nchi !
 
Wadau, katika kile kinachoonekana kuwa huenda Bunge likaingia tena kwenye mgogoro na Mahakama juu ya sakata la ESCROW, Leo Mwanasheria wa IPTL na PAP, Joseph Makandege amesema kuwa wamepeleka shauri Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Kisheria juu ya Maazimio yaliyotolewa na Bunge juu ya sakata la ESCROW. Mtakumbuka kuwa IPTL na PAP walitoa taarifa ya kupinga maazimio hayo na kuyaita ni ya kipuuzi.

Inaonekana IPTL na PAP wametafskari vya kutosha na wameona kuwa kuna haja ya Mahakama Kuu kutoa ufafanuzi juu ya maazimio hayo hasa kutokana na kuonekana kuwa yanaingilia mihimili mingine ya dola na yanajichanganya.

Source: TBC1
We punguani watu tumesha acha kuangalia TBC1 hilo ni danguro la ccm, hawawezi ikosoa ccm jambo ambalo ni baya sana. Pili, mahakama za Tanzania hazina uwezo kisheria kutoa maamuzi juu ya sakata la ESCROW kwasababu mkataba ulifungwa chini ya mahakama ya kimataifa ya biashara, na hawa ndiyo wanapaswa kutujulisha ikiwa IPTL imelipwa au la, na siyo mahakama ya Tanzania; hili fahamu kabla haujaleta mada za kipumbavu huku jf.
 
Wadau, katika kile kinachoonekana kuwa huenda Bunge likaingia tena kwenye mgogoro na Mahakama juu ya sakata la ESCROW, Leo Mwanasheria wa IPTL na PAP, Joseph Makandege amesema kuwa wamepeleka shauri Mahakama Kuu kuomba ufafanuzi wa Kisheria juu ya Maazimio yaliyotolewa na Bunge juu ya sakata la ESCROW. Mtakumbuka kuwa IPTL na PAP walitoa taarifa ya kupinga maazimio hayo na kuyaita ni ya kipuuzi.

Inaonekana IPTL na PAP wametafskari vya kutosha na wameona kuwa kuna haja ya Mahakama Kuu kutoa ufafanuzi juu ya maazimio hayo hasa kutokana na kuonekana kuwa yanaingilia mihimili mingine ya dola na yanajichanganya.

Source: TBC1
Wanahangaika. Kumbuka pia muda mfupi kabla ya bunge kujadili suala hili walienda mahakamani na sasa muda mfupi kabla rais haja huku wa hatua wanakimbilia tena mahakamani. Ninatumaini mahakama italiona hili kuzuia mgangano usio wa lazima kati ya mihimili ya dola.
 
Hivi vichwa vya ccm bana tabu tupu,PAC inawajumbe 19,Taarifa yao imejadiliwa na wabunge zaidi ya 350 including mawaziri na makada wa ccm na mwisho kufikia maamuzi yaliyofikiwa,wewe na elimu yako ya kuunga unga unakuja na uharo hapa.

mkuu huyo jamaa anashindwa kuelewa kuwa yale mapendekezo si ya PAC tena bali ni ya BUNGE
 
Popote ulipo Habinder Singh Seth hakikisha unakwamisha maazimio ya Bunge letu TUKUFU ili mziki huu uwe mnene mwaka mzima mpaka uchaguzi MKUU utasaidia sana na watanzania wengi watakuwa wameamka juu ya wizi wa kutisha uliofanywa.JK na wewe kaa kimya ili watu wawe na akili maana uvivu wa kufikiri kwa watanzania ni mkubwa ili wajue kama wameibiwa wanatakiwa hata wakienda hospitali Wafie milangoni maana Dawa hakuna,UMEME upande ikiwezekana watu walipe laki mbili na nusu kwa mwez.maana hili TAIFA ni la Vilaza.kikwete oyeeeeeeee,Harbinder Singh Seth oyeeeeeeeee,maisha magumu kwa kila MTANZANIA safiiiiiiiiiiiiiii.
 
Tusione aibu watanzania kusema mahakama yetu ni chafu.

Huku ikitambua bunge ndio muhimili mkuu tumeona kwa uchungu mahakama ikijaribu kuzuia bunge lisifanye kazi hivi majuzi ili kuwalinda wezi waliothibitika kukwapua kiwanda na mabilioni fedha ya umma. Eti sasa hao wezi wameenda tena mahakamani kuzuia maazimio ya wananchi kupitia bunge lao yasitekelezwe. Mahakama sasa imekua mwizi wa haki badala ya kutoa haki. si muda mrefu mahakama itadharauliwa kabisa jambo ambalo ni hatari kwa taifa.

Mahakama imekua imewekwa ganzi kufanya haki kwa mambo ya umma na tumekua tunaona wezi na matapeli wa nchini na kimataifa wakipewa ruksa na mahakama kutia taifa kabali kutokana na hukumu za kustaajabisha.

Kuanzia richmond dowans iptl wananchi tumeshuhudia maslahi ya umma yakibwagwa mahakamani mfulilizo huku wanasheria wetu wakilipwa mabilioni kwa kushindwa kesi. sasa kwa hili la escrow tunasema wananchi kupitia wawakilishi wao wameamua. Kama mahakama ni biashara kwa escrow wameliwa na tunamuonya rais wa jamhuri kama akitetereka.

Jaji mkuu ana kazi ya kusafisha nyumba yake, hakika ni chafu kabisa

Rejea kauli ya spika kwamba wabunge nao wanapewa pesa na wafanyabiashara wakubwa ili kulinda maslahi yao bungeni, hilo nalo unaliwekaje mkuu mihimili yote inatia kinyaa, bunge, mahakama na Serikali/dola
 
Popote ulipo Habinder Singh Seth hakikisha unakwamisha maazimio ya Bunge letu TUKUFU ili mziki huu uwe mnene mwaka mzima mpaka uchaguzi MKUU utasaidia sana na watanzania wengi watakuwa wameamka juu ya wizi wa kutisha uliofanywa.JK na wewe kaa kimya ili watu wawe na akili maana uvivu wa kufikiri kwa watanzania ni mkubwa ili wajue kama wameibiwa wanatakiwa hata wakienda hospitali Wafie milangoni maana Dawa hakuna,UMEME upande ikiwezekana watu walipe laki mbili na nusu kwa mwez.maana hili TAIFA ni la Vilaza.kikwete oyeeeeeeee,Harbinder Singh Seth oyeeeeeeeee,maisha magumu kwa kila MTANZANIA safiiiiiiiiiiiiiii.
Well said. You have made my day.
 
na mimi naombea hivyo,hali izidi kuwa mbaya zaidi labda ndio wajinga watapata akili
 
Back
Top Bottom