Sakata la Kampuni ya Lugumi: IGP na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani watupiana mpira

Sakata la Kampuni ya Lugumi: IGP na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani watupiana mpira

Hata kama huo mkataba uliingiwa na wizara kwa niaba ya jeshi la polisi, lazima uongozi wa jeshi uwe na copy ya huo mkataba. Kwa sababu hao ndio "user department" na wao ndio walipeleka hayo mahitaji huko wizarani. Sasa labda waeleze kuwa hawakushirikishwa kwenye mchakato wa kumpata huyo mzabuni (lugumi) au hawautambui huo mkataba.

Kinachofanyika hapa ni kutupiana mpira kwa sababu wanajua ule mkataba una madudu ndani yake.

Na katibu Mkuu wa wizara anachofanya ni kumsuta IGP "wewe si ulikuwepo kabla yangu, kwa hiyo unaulewa vizuri huo mkataba"

Lakini mwisho wa siku IGP Mwema nae ajiandae "kutenguliwa"
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini,Ernest Mangu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani,Jaji Meja Jenerali Projest Rwegasira, wameripotiwa kutupiana mpira kuhusu kuhusu ni nini kimesababisha kutokuwasilishwa kwa mkataba huo kwa kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali siku ya jana.

Mangu anasema: "Iliyoagizwa ni wizara kwahiyo siwezi kuzungumza kwa niaba ya wizara na hiyo siku Katibu Mkuu alikuwepo."

Alipoulizwa kwamba,kwa upande wao wamekwishawasilisha mkataba huo wizarani alisema: "Kwani anayesaini mkataba si katibu mkuu,hivyo wasaliana na ofisi ya katibu mkuu au waziri."


Gazeti lilimtafuta Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ambae alisema: "Ninaomba uwasiliane na IGP."

Baada ya kauli hiyo,Tanzania Daima lilimweleza kwamba IGP Mangu amesema atafutwe Katibu Mkuu kwani siku hiyo alikuwapo(siku walipokutana na kamati ya PAC) ambapo Rwegasira alisema: "IGP atoe maelezo siyo Katibu Mkuu,kwani hata siku hiyo tulipokwenda aliyekuwa anajibu maswali ni IGP siyo mimi."

Alipoulizwa ulipo mkataba huo,Katibu Mkuu huyo alisema: "Hata kama ofisi yetu ndiyo inasaini mkataba,lakini suala hilo lilielekezwa moja kwa moja kwa IGP ambae alikuwa anajibu."

"Mimi nategemea aliyeambiwa kupeleka ni IGP,huu ni uelewa wangu na kama alijua hana angeeleza kwamba hana ili kamati ya Bunge itoe maelezo ya jinsi ya kumsaidia kuupata." aliongeza Rwegasira.

Baada ya ufafanuzi huo wa Rwegasira,Tanzania Daima lilimtafuta kwa mara nyingine IGP Mangu ambae hakupatikana kwani simu yake ya kiganjani ilikuwaa ikiita bila kupokelewa.

Chanzo: Tanzania Daima

Bora ya yule mama!
Hivi huyo mangu ni chaguo la ngosha au mkwere? Maana hapo naona kama safari yake ya kurudi ziwa singidani kuvua samaki ndio inawadia na huyo katibu ajiandae kwenda kwao bukoba kuvuna kahawa
 
Kama IGP alimsimamisha afisa manunuzi wake, mbona la kupeleka documents anasita? Au nae anamjengo mmoja kati ya hizo 40? Kwa katubu mkuu bado mgeni sana kwenye hiyo Wizara. Haelewi historia ya hicho kitu.
Kuja mambo hapo.
Wacha wapapatuwane tu
 
Magu kivipi tena wewe fisi wakati ngoma ipo chini ya kamati ya Bunge? Au mnataka mpewe fursa ya kusema Magu dikteta anaingilia Bunge?
Wewe fisi wa lumumba wacha kutokwa na mapovu, naona yamekujaa kwenye migongo ya midomo yako utadhani umebugia uyoga wenye sumu tulia sindano ikuingie vizuri
1460479902800.jpg
 
Likishajadiliwa Bungeni mapendekezo/maazimio ya Bunge hupelekwa wapi kwa ajili ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na wahusika kuchukuliwa hatua?

Acha kukurupuka kama hujui kaa kimya.
Mkuu huyo wacha kuhangaika naye maana ni mfagiaji pale lumumba
 
Kitaeleweka tuu uyu mjeda nae anagwaya nini kama yeye ndo custodian wa mkataba si awape copy.
Ingawa am sure IGP na Katibu wote wana mikataba ila as long as aliyekuwa anajibu maswali ni IGP yeye ndo apeleke mkataba kwa PAC
 
Itafahamika ni swala la muda tu.!
Muda sawa hata miaka kumi au ishirini ni muda pia ila tungesikia basi hata tetesi tu juu ya Escrow inge tupa moyo,haya majipu ni kama yana fanyiwa sorting vile.
 
Tanzania Daima nanyi wachokozi! Hamjui hilo jipu limekaa pabaya sana - liktumbuliwa ina maana mhusika inabidi awe ameishaandika wosia! Haya ndio yale mzee wa 'wapigwe tu' alikuwa akiyasema 'ukiwagusa nchi itayumba'.
Teeeeeeh teeeeeeeeh umenikumbusha mzee wa wapigwe cheki alivyo lala chali chezea mkwere weye?
1460480192089.jpg
 
Back
Top Bottom