Sakata la Kampuni ya Lugumi: IGP na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani watupiana mpira

Hamumjui Ngosha. N
Masikini ngosha wa watu!!!!!
Duuuh panya watakuwa wameula,nchi hii bwana

Usihofu Mkuu. Mh. Tayari ana kila kitu, taarifa zote anazo na mpaka mkataba anao. Mkwere aliwapuuzia jamaa wa nusa nusa kila wakimpelekea taarifa za kiintelejensia. Kumbe alikuwa anafanya hivyo kwa maksudi kwa kuwa yeye ndo alikuwa mpiga ngoma. Kipindi hiki Ngosha anawatumia sana Nusa nusa kwa hiyo anajua kila kitu. Hizo briefings za kila siku kutoka kwenye vyombo vyake anazifanyia kazi. Hatokubali watu 50,000 waumize population ya watu mil 50. Mungu akupe Maisha Marefu Mh. Rais uwapiganie watanzania
 
Kuanzia former prez,mtoto,igp, lugumiz wote majipuu ktk sakata hilo,shida ni moja hakuna ambaye anaweza kulitumbuaaa jipuz hilo.
Sana Sana hayo matume yakatayoundwa na wanasiasa wataishiaaa kupiga makelele tu
 
Ndio maana unaona hizi dana dana zote zinaendelea

Watanzania wangejiuliza kwanza kabla ya kujadili huu mpira wanaotupiana

Vifaa vilivyotarajiwa kununuliwa ni vitendea kazi vya Polisi
Mkuu wa jeshi la Polisi alipaswa kujua mradi wa vitendea kazi vyake unakwendaje

Hapa angejiuliza, kama mradi ulikuwa wa vituo zaidi ya 100 nchini, iweje vituo 14 ndivyo vipate huduma tarajiwa kama ilivyoandikwa na gazeti moja?

Angeangalia bajeti na kuwasiliana na wahusika haya yasingefika hapa.
Kwa maneno mengine, mkuu wa jeshi hakuwa na taarifa wala kujua mkataba
Tumefikaje hapa!

Pili, Watanzania wajiulize, kulipokuwa na harufu za ufisadi bandarini timu iliondoka mapema tena wakiwa na nyaraka zote za kuonyesha makontena yaliyopita hadi walinzi.
Vipi kuna kigugumizi kutafuta ukweli wa suala hili?

Tatu, tuliona habari za mita za mafuta zikiibuliwa na wahusika kutakiwa kujieleza.
Vipi hili lina kigugumizi na wale wale waliokuwa wanashangiliwa hawaonekani?

Nne, kashfa kama hii si ndogo. Inahusisha jeshi la Polisi wenye dhamana kubwa katika jamii. Ni wakati serikali itoke na kueleza wananchi nini hasa kimetokea.

Iwe ni uzushi basi ielezwe, iwe ni ukweli ielezwe, tumezoa mikataba ya magumashi
Huu utumbuaji mbona umejikita katika vijipu uchungu, matambazi hayaguswi?

Watu ni wale wale na sera ni zile zile za kulindana. Wanafeli !!

Nyani Ngabu The Boss Mzee Mwanakijiji Mag3
 
mkuu natangaza hadharani furaha kubwa sana niliyonayo baada ya kusoma andiko lako humu tena , nilipatwa na mashaka makubwa sana kutokana na kimya chako , BAK is back , Welcome home mkuu , thank you god .

Nakala kwa Chakaza
 
Hawa nao wajinga sana, wamepewa mkataba mnono na kwa zaidi ya miaka mitano wameshindwa kufunga mashine ktk kila wilaya sawa sawa na mkataba wanategemea nini eti!!??

Aisee, acha tu watumbuliwe.......hakuna jinsi nyingine!!
Ukishakuwa mdhulumati huwezi fanya mambo ya halali
 
Mhh! Ngoja tusubiri Jipu uchungu hili
 
Halafu cha kushangaza wakati sakata hili likiendelea Magufuli na Majaliwa wamepiga kimya kama haliwahusu. HAPA KAZI TU! 🙂

 
Ahsante sana Mkuu Erythrocyte kwa kuonyesha furaha yako kubwa sana ya uwepo wangu hapa jamvini, shukrani sana.

mkuu natangaza hadharani furaha kubwa sana niliyonayo baada ya kusoma andiko lako humu tena , nilipatwa na mashaka makubwa sana kutokana na kimya chako , BAK is back , Welcome home mkuu , thank you god .

Nakala kwa Chakaza
 
Ahsante sana Mkuu Erythrocyte kwa kuonyesha furaha yako kubwa sana ya uwepo wangu hapa jamvini, shukrani sana.
Duh, BAK, umetokea wapi tena! Karibu sana, nilianza kuingiwa na wasiwasi kuhusu uwepo wako humu. Naomba nikupe tahadhari moja tu, viwavi vingi vimemwagwa humu na wapo wenzetu wachache wamesalimu amri na kuweka silaha chini kwa ule mtindo wa if you can't fight them, join them.

Taasisi za serikali zilizokuwa mstari wa mbele zikihusishwa na ufisadi bado ziko pale pale...Jeshi la Polisi lipo pale pale, jukumu lao kubwa kwa sasa ni kuwashughulikia wanaokosoa serikali. Badala ya kuwalinda raia wema na mali zao, wamejikita katika kukilinda chuo cha Mafisadi na wahitimu wake!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…