Amejiridhisha kanisa kuwepo katikati ya barabara ?
Hivi huu sio umbea na majungu ya mji wa Tabora kweli?
Inawezekanaje kanisa lijengwe na kuwepo "katikati" ya barabara lenyewe tu kama mbwa aliyegongwa na gari na kuachwa hapo?
Huu ni uongo. Ukisema limejengwa katikati ya makazi ya watu, hapo nitakuelewa...
Hata hivyo, kanisa au msikiti ni huduma za kiroho zinazopaswa kuwa katikati ya makazi ya watu. Kanisa siyo kiwanda cha kemikali kuwa ulitenge porini mbali na watu....
Na ktk utaratibu wa mipango miji sidhani kama kuna eneo maalumu hutengwa kwa ajili ya kujengwa makanisa au misikiti yote....
Ni kwa sababu, huwezi kuyarundika makanisa au misikiti yote mahali pamoja unless uwe unayekuja na mpango huo uwe unataka kusababisha vurugu miongoni mwa waumini wa madhehebu au dini hizo. ..
Kwa kesi yenu hapo Kariakoo, mnachotakiwa kufanya ni kujaribu kudhibiti kelele kwa kuongea na uongozi wa kanisa hilo kuwakumbusha kuwa HAKI na UHURU WAO WA KUABUDU usitumike vibaya ku - violate UHURU na HAKI za wengine. Hilo ni kosa na wanastahili kuchukuliwa hatua za kisheria...
Kama furaha yao iko katika kujipigia muziki mkubwa kwa sauti ya juu, sheria inawataka kuweka "SOUND PROOF" kwenye jengo ili kuzuia sauti kupaa na kutoka nje kusumbua watu wengine...
It's simple like that. Hayo mengine mnayoandika ni fitna na chuki tu isiyo na sababu. Kasoro pekee ni "sauti ya juu ya muziki wao wanaopiga usiku kucha". Kama hili ni la kweli, basi hili ndilo tatizo la kutatuliwa. Na hii haipo Tabora tu. Tatizo hili liko maeneo karibu yote Tanzania...
Hata maspika ya waislamu waliyoyatundika juu ya misikiti yao na usiku na alfajiri kuwashwa na kuanza kupiga kelele, nalo laweza kuwa tatizo pia...!!
Kama wao wanao Uhuru na haki ya kuabudu na kusali usiku kucha, basi wakumbuke watu wengine na majirani zao nao wana hakiki ya kutopigiwa kelele za muziki ambao hauwahusu, wana haki ya kuishi ktk mazingira tulivu na yenye amani...
Asante...