Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sii kweli wewe fuatilia maelezo ya Mzee ES,.... nafiki bado yupo hapa kijiweni hadi kesho au sio?...Kumbuka deal limepitishwa Kreist Sykes akiwa bado meya wetu Dar!
 
Invicible,
Thanks. Ni IPTL. Unajua hivi abbreviations zikizidi nazo huchanganya akili.
 
Nasikia uchungu sana ninapoona sisi Watanzania, wana wa Nyerere tunavyochezewa akili na kuonewa watakavyo hawa tunaofikiri tumewaamini kumbe tumemkabidhi FISI bucha za Nyama!!!

Ukweli kuhusu Richmond Development ni huu:- RDC si kampuni ya kimarekani kama walivyojitangazia. Hii imetokana na tabia ya waafrica kufikiri kampuni za Ulaya na Amerika ndizo za maana hivyo wakatumia njia hiyo kuwazuga. RDC Ni kampuni ya Waarabu na wapo mtaa wa Mosque karibu na Jambo Inn Hotel wanashughulika na Internet pamoja na kupigisha simu za nje kwa gharama nafufuu kuliko mtandao wote niliowahi kuuona!!! Wanapigisha kwa Tshs 200 Per Min. simu za nje nchi yeyote ile Ulaya. Na hii ndiyo biashara yao iliyowaleta hapa Tz. Wanayo ofisi nyingine pale Mnazi mmoja inafanya kazi kama hiyo.

RDC wanaposema wameuza contract kwa hiyo kampuni ya UAE ambayo ni mali ya familia ya Kifalume huko Uarabuni si kweli. Ni Mazingaombwe aliyosema mwanakijiji ndiyo yanafanyika. Hao Wamilki wa hiyo Kampuni ngeni na hao waaarabu wa RDC ni kitu kimoja kasoro pua tu.

Hapa naanza kuamini yale maneno yaliyokuwepo kuwa kuna wagombea wamechukua pesa za kampeni Uarabuni, !!! huenda ndiyo muda wa kuzirudisha umeshafika. Kitendo cha rais mzima kusimama na kuanza kutetea RDC kinanipa wasiwasi kama kweli yeye au jamaa zake wakaribu hawajahusika na hilo deal. !!! Kama utakumbuka Mkapa aliwahi tetea kwa nguvu zake na sauti ya ukali kwenye TV, kuwa NMB inaingiza hasara na yeye ndiye anajua, na hakuna Mtanzania anaweza kuiendesha!! LAZIMA iuzwe!!!. Lakini muungwana mpenda Tanzania na watu wake,, Director aliamua kujitosa na na ku sacrifice maisha yake, akasema ukweli the next day. Akatoa data zote zinazonyesha bank inapata faida mabillion. Na kesho yake akaacha kazi akaishia USA. Na hiyo ilikuwa kwa sababu ilipangwa iuzwe achukue Mramba maana alikuwa ameshasimamia migao ya wazee, na zamu yake ilikuwa hiyo. Bila kupiga kelele ilikuwa imekwenda.

Hivyo hili la RDC muungwana hana cha kukwepa, lazima atueleze kama muda wa kulipa lile deni UAE umefika? Tukubaliane basi tulipe kidogo kidogo, maana kama kwa mwaka mmoja tu kiasi hiki. Baada ya 10yrs tutakuwa tumekwisha.

Nilimwamini sana alivyoingia madarakani 100% na nilimpigia kura na nikashawishi watu wengi sana hata kwa kubishana hadi tunapigana, LAKINI nimeshaanza kutoa waminifu wangu, hadi sasa ni 80% imebaki. Na kama hiyo tabia itaendelea basi nitatoa zote.

MUNGU IBARIKI TANZANIA NA WATU WAKE!!!!
 
Hongera mwanakijiji Article yako nimeiona na nimeisoma imekwenda shule.
Keep it up

Wenye masikio na wasikie, wenye macho na waangalie
 
Mwanakijiji

Nice article.

Thanks Poorman for the info...are these backed up by credible data/sources??


Kama kuna Mtanzania yoyote alikuwa bado hajapata kizunguzungu na hili kasheshe la Richmond then naona baada ya kusoma post ya Poorman anaweza kunywa sumu kabisa.
 
Lordtical,
Somehow I believe the Poorman. Sihitaji ushahidi kuona kwamba something is awfully wrong with the current leadership in Bongo. Poorman, karibu sana jamvini hapa ndipo tunakata issues zote za Bongo. Mchango wako utasaidia sana.
 
Yaahp! Mzee Bob,

Nimekusikia mkuu, na kesho utakuwa ndio mwisho wangu kwenye majira ya mchana nitatoa tamko la mwisho na utakuwa mwisho, but, forum inaendelea kupata wakali na watakuja zaidi bado wanakuja,

RDC isssue sasa hivi imepamba moto, ninawashukuru wale walionitumia more info kwenye private, leo nzima nilikuwa ninazikusanya tayari kuzikabidhi kesho kwa wakubwa wa nchi wanaozihitaji, kwa hiyo bado tunahitaji kusema more kwenye the issue, sasa serikalini kuna mtafutano maana wengi walikuwa hawajui kilichotokea, nina wasi wasi kwenye hili la RDC, likiendelea kulia kidogo kama wiki moja zaidi litamshusha mtu kwenye madaraka, maana hawa wanaotaka independent info ni watu wa kamati kuu watupu ambao wako tayari kumshusha mtu Dodoma, hivi karibuni,

We can hope, maana unawajua CCM kwa mazingaombwe ila for us ni ku-press full speed let the chips fall where they may!
 
Watanganyika tumelala sana. Tunasemea uvunguni wakipita twapiga makofi na kutoa sifa kemkem .Je mnategemea wao wafanye nini wakati wamesha jua uozo ulipo ?
 
Poorman: Yaani bado unatoa 80%??! Hiyo ni distinction kali sana. Wewe hujachoshwa bado mpaka hapo!
 
Angalia sehemu ya habari katika Nipashe ya leo:
"Na katika hatua nyingine, kampuni ya Messrs Dowans Holdings ya Falme za Kiarabu iliyonunua kampuni ya Richmond Development (RDC) ya Marekani, imeingiza nchini mitambo yenye uwezo wa kuzalisha megawati 20 za umeme".

Ina maana RDC walikuwa hawajaleta huo mtambo wa mgawati 20 au mimi nilielewa vibaya?
 
These guys are bunch of bustards they deserve to be shot
 
Mwanasiasa,
Nadhani Dowans wamenunua zile turbines za Boeing 707 zilizoletwa na Richmond mpaka tukaonyeshwa picha pale International Airport. Sasa watakachofanya (my speculation) ni kuleta jet fuel na utasikia turbines zinawaka. Meanwhile nchi inaendelea kuliwa.
 
Habari za Kitaifa Habari nyingine zaidi!
Richmond yazidi kung'ang'aniwa
Oscar Mbuza
HabariLeo; Tuesday,January 02, 2007 @00:06

CHAMA cha NCCR –Mageuzi, kimesema kitaishinikiza Serikali kueleza ukweli wa mazingira yaliyoifanya kuingia mkataba wa uzalishaji umeme na Kampuni ya Richmond Development (RDC) ambayo ilishindwa kuzalisha umeme kama ilivyotarajiwa na kuuzwa kwa kampuni nyingine.

Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, James Mbatia, aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam jana, wakati akitoa tamko la chama hicho kuhusiana na matukio muhimu yaliyotokea nchini mwaka 2006.

Mbatia alisema kampuni ya Richmond imewaongezea mzigo wa madeni Watanzania kwa vile mkataba uliofikiwa baina yake na Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) una gharama kubwa kuliko ule wa kampuni ya kuzalisha umeme ya IPTL.

Alisema wakati mkataba baina ya Tanesco na IPTL una gharama ya dola za Marekani milioni 150, mkataba wa Richmond una gharama ya dola za Marekani milioni 175. Mwenyekiti huyo alisema kutokana na Tanzania kujiingiza katika mikataba mibovu kama mkataba wa Richmond, unafanya deni lake nje ya nchi kuongezeka kutoka sh bilioni 7.8 mwaka juzi, hadi sh bilioni 9.9, mwaka jana.

"Ongezeko la deni hili linamfanya kila Mtanzania sasa kubebeshwa mzigo wa deni la sh. 350,000, badala ya sh. 200,000, walilokuwa wamebebeshwa mwaka juzi." Alisema uongozi wa chama hicho bado unatafakari hatua za kuchukua kuhusiana na mkataba huo baina ya TANESCO na kampuni ya Richmond. Alisema chama hicho pia kimesikitishwa na hatua ya Rais Jakaya Kikwete, kushindwa kulizungumzia suala la Richmond katika hotuba yake ya kuaga mwaka aliyoitoa juzi.

Alisema baada ya Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kutolizungumzia suala hilo, wakati akieleza utekelezaji wa ahadi za Serikali katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita, mjini Dodoma Desemba 21, mwaka jana, chama hicho kilitegemea kwamba Rais Kikwete angelizungumzia suala hilo juzi. Alimwomba Rais Kikwete, kuwawajibisha mara moja, viongozi aliodai walimpa maelezo ya uongo.


NCCR wameamua kulivalia njuga hili vipi CHADEMA? Au mnasubiri mkutano?
 
Rais aliye patikana kwa Rushwa lazima ataendeleza rushwa .Ndiyo maana PM alienda Thailand kuomba mvua wakati Nchi ile na serikali ile ilijaa rushwa hadi ikapinduliwa . JK katuuza na kampuni ile yeye ana mkono ndiyo maana hawezi kuisemea ipasavyo je unategemea nini wewe bwana Mbatia ?
 
Waache akina Mbatia waseme iingie katika record. Bila record Sadam asingehukumiwa!
 
Wajinga ndio waliwao!
Kheeee heeeee heeee.................Ehh!
 
Hivi hawa wakina Chadema, NCCR na CUF etc kwa nini wasifanye MAANDAMANO ya pamoja kupinga mambo kama haya.??

Hawa jamaa kweli wapo kwa manufaa ya wananchi??...issue kama hizi za RDC ndio za kuchukulia ujiko maana kila mtanzania anaelewa na kukerwa na ukosefu wa umeme hivyo ni rahisi kupata watu, wanafunzi, vijana, wakinamama na wazee. Lakini wao aahhhh KALAGHABAHO
 
Back
Top Bottom