Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Sakata la Kashfa ya Richmond: The Facts

Niseme nini zaidi?...
Damn!...Mwanakijiji rusha muziki huu ktk FM nzito yenye masafa marefu...
Ama kweli hili kimba!
 
Mzee yaani hadi kichwa kimeniuma leo; Maana kama mambo ndivyo yalivyo basi tutafika kweli sisi?
 
Kuhusu muda wa dharura wa mkataba wa Richmond, ripoti ya wanasheria wa Bunge inasema hivi:

"Kwa mujibu wa tangazo la zabuni la TANESCO, muda wa kukodi jenereta hizo
ulikuwa ni miezi kumi na mbili tu na ungeweza kuongezwa kutegemeana na hali
ya uzalishaji umeme nchini. Kamati ya Serikali ya Majadiliano iliongeza muda wa
kukodi mitambo hiyo kutoka miezi kumi na mbili mpaka ishirini na nne ambayo
itaanza kutumika rasmi baada ya uzinduzi wa mitambo (full capacity).
Kwa kuwa madhumuni ya Mkataba huu ilikuwa ni kuzalisha umeme wa dharura,
(Emergency Power Supply Agreement) Serikali ilipaswa kutilia maanani hali ya
uzalishaji umeme wa baadae ikiwa upatikanaji wa maji ungerejea katika hali yake
ya kawaida. Muda huo unafanya udharura wa mkataba huu utiliwe mashaka"

Na kuhusu uhalali wa kampuni ya Richmond, wanasheria watu wanasema hivi:

"Hata hivyo, utafiti wetu umebaini kuwa, Kampuni ya Richmond Development
Company LLC, ilitoa taarifa za uongo ( misreprestantion of its corporate status )
kuhusu uhalali wake kisheria wakati wa kuingia mkataba na TANESCO . [Tazama
Kifungu cha 5 cha Waraka wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO (Memorandum
for the TANESCO Board of Directors Concerning the Contract with Richmond
Development Company LLC)]
Kitendo hicho ni cha ukiukaji wa Mkataba kwa mujibu wa masharti ya Kifungu
12.1(g) cha Mkataba huo (i.e Event of Default) yanayotamka kwamba, Richmond
Development Company LLCitakuwa imekiuka Mkataba iwapo itatoa maelezo au
taarifa ambazo zitathibitika kuwa ni za uongo wakati zilipotolewa na ambazo
zinaathiri uwezo wa Kampuni hiyo kutekeleza majukumu yake yaliyoainishwa
katika Mkataba."

Na wanahitimisha kwa kusema hivi-

Aidha, kwa mujibu wa masharti ya Kifungu cha 12.3(c), Shirika la TANESCO
linayo haki ya kuvunja Mkataba huo kutokana na kitendo hicho cha Richmond
Development Companuy LLC cha kukiuka Mkataba.
Kwa ufasaha na uwazi zaidi, vifungu hivyo husika vya Mkataba vinatamka kama
ifuatavyo:-
“12.1 Each of the following events shall – become a supplier event of Default:-
(g) any statement, representation or warranty by the supplier in this Agreement
proving to have been incorrect, in any material respect, when made or when
deemed to have been made and such incorrect statement, representation or
warranty materially and adversely affects the supplier’s ability to perform it
obligations under this Agreement”.
“12.3(c) TANESCO shall have the option, upon not less than 30 days prior written
notice, to terminate this Agreement on default and the supplier shall be entitled to
legal remedies as prescribed by the applicable laws”.
Pamoja na TANESCO kuwa na haki ya kuvunja pia haki ya kulipwa fidia kwa
mujibu wa Kifungu cha 4.4 cha Mkataba, uchambuzi wetu umebaini kuwa
TANESCO haikuzitumia kabisa haki hizo.

Na wanasheria hawa mahiri wanauliza swali hili ambalo linaonesha wazi kilele cha ufisadi na angalia majibu yao ambayo hata Mkono na umahiri wake ameshindwa kuyaangalia hata Chenge na uanasheria wake wote ameshindwa kuonesha anajua!!

Kamati Teule imepata bei za
mitambo kutoka kwa baadhi ya watengenezaji wa mitambo ya uzalishaji wa
umeme huko huko Houston Marekani kwa Kampuni iitwayo Kawasaki Gas Turbines
– Americas. Mtambo mpya aina ya GPB180 wenye uwezo wa kuzalisha MWs
17.5 ni dola za kimarekani 7.5 milioni.
2. Iwapo TANESCO au Serikali iliweza kufungua Barua ya Dhamana ya Benki ya
thamani ya dola za kimarekani 30,696,598, je, fedha hizo zisingeweza kutosheleza
kununua mitambo mipya ya uzalishaji umeme, na mitambo hiyo
kubakia mali ya TANESCO, badala ya kuingia katika Mikataba ya ukodishaji
umeme?
Aidha, taarifa za watendaji wa Wizara ya Nishati na Madini kwamba wakati wa
kipindi cha mchakato wa Zabuni ya umeme wa dharura kulikuwa na ugumu wa
kupatikana mitambo ya umeme wa dharura zimeonekana sio za kweli.
Ni ukweli kwamba kulikuwa na ukame, lakini ukame huo haukuwa wa majenereta
kwani majenereta hutengenezwa muda wote na sio kwa kutegemea mvua.
Aidha, utafiti wetu umebaini kuwa katika kipindi hicho cha matatizo ya umeme
nchini Kampuni hiyo ya Kawasaki ilikuwa na mitambo 8 ya kisasa tena ile yenye
kutumia gesi na dizeli (dual fuel plant). Mitambo hii pia ina uwezo wa kusukuma
maji na hapo hapo kuzalisha umeme. Na hii bei ya dola 7.5 miliono kwa mtambo
mmoja ni bei ya kuanzia tu kwani mteja anaweza kupunguziwa. Ushahidi wa hili
ni kwamba Serikali ya Nigeria mwaka huo 2006 iliuziwa mitambo hiyo kwa dola
6.7 milioni kwa mtambo mmoja.

Tutaendelea....
 
Nijulisheni basi kama huu mziki umewakolea ili wengi zaidi washaurike kuusikiliza.........

..kuishi ni kuona mengi!

..hujafa hujaumbika!

..elimu haina mwisho!

..ndondondo si chururu!

...hayo ndo nnayoweza kusema kwasasa!
 
Mimi napata kizunguzungu hapa,kutokana na mkataba mwenye uwezo wa kusitisha mkataba ni tanesco,lakini wao wanasema ni serikali, kunani hapa?
 
Kumbuka kuwa hawa jamaa watatu waliweza kupitia mikataba hiyo sita ndani ya siku saba na kuichambua kama vile mtu anavyochambua mchele na chuya!
 
Kumbuka kuwa hawa jamaa watatu waliweza kupitia mikataba hiyo sita ndani ya siku saba na kuichambua kama vile mtu anavyochambua mchele na chuya!

Sasa Taifa linaposema hatuna wataalamu wa mikataba - wakati ukweli ni kuwa wataalamu kama hawa wapo - inaleta picha gani?

a) Waliopo kwenye nafasi nyeti wapo pale kwa who-knows-who na sio kwa sifa;
b)Vilaza wamewekwa kwenye sehemu ambazo hawastahili kwa manufaa binafsi;
c)Sekta ya sheria iangaliwe upya. Kila Chuo Kikuu kinachoanzishwa kinaanza na kutoa degree ya LLB. Hivi hao Lecturers/Professors wa kutosheleza mahitaji ya ufundishaji wanawapatia wapi. We are ending getting half-baked lawyers.
 
Hili goma zito si utani... nimelisakata rhumba hapa nimelowa jasho chapachapa, ngoja nitoke nje nipate upepo kidogo....
 
Tuwekeeni basi huo wa EPA, naona huo utavunja rekodi ya THRILLER kwa mauzo. Ila huu wa sasa hadi nimechoka pumzi zote zimeniisha, mapigo yangu ya moyo yanaenda kwa kasi ya ajabu, kweli mimi kama kijana wa kitanzania nimeshindwa kupata maneno ya kueleza ni jinsi gani najisikia hivi sasa, machozi yananilenga lenga, i feel hopeless kuishi katika nchi hii, nasita kuanzisha familia kwenye ardhi hii iliyo jaa neema, nikihofia fate ya mambo haya, najionea huruma nawaonea huruma vizazi vinavyoendelea kukua na vinavyokuja, lakini kuna sauti ndani inaniambia dont lose faith, huu ni wakati wa mpito, jisikie faraja kuishi wakati mambo haya yanatokea kwani kuna wengi waliziota siku kama hizi lakini hawakupata kuziona, mmoja wapo alikuwa ni baba yangu (RIP)
9.3.6 Kwa kuzingatia kuwa Mikataba mibovu kati ya TANESCO na Makampuni mbalimbali
ambapo Makampuni hayo yanalipiwa kodi yote na TANESCO imekuwa ni chanzo cha
bei kubwa za umeme katika nchi yetu, na kwa kuzingatia kuwa Mikataba hiyo inasababisha
Sera muhimu za Taifa, kama vile, Sera ya Kupiga vita Umaskini, Sera ya Huduma
Bora kwa Jamii, Sera ya Taifa ya Nishati inayolenga kusambaza nishati ya bei nafuu vijijini
n.k. kutotekelezeka, tunashauri kuwa Mikataba hiyo ipitiwe upya ili irekebishwe,
kwa maslahi na manufaa ya Taifa letu.
9.3.7 Mwisho, kwa kuzingatia ukweli kwamba, Mikataba hiyo mibovu, kwa kiasi kikubwa inadidimiza
uchumi wa nchi yetu, tunapendekeza Serikali ichukuwe hatua muafaka zinazofaa
ili kuondoa hali hiyo ambayo inalipeleka Taifa letu shimoni.
 
tuwekeeni basi huo wa EPA, naona huo utavunja rekodi ya THRILLER kwa mauzo. ila huu wa sasa hadi nimechoka pumzi zote zimeniisha, mapigo yangu ya moyo yanaenda kwa kasi ya ajabu, kweli mimi kama kijana wa kitanzania nimeshindwa kupata maneno ya kueleza ni jinsi gani najisikia hivi sasa, machozi yananilenga lenga, i feel hopeless kuishi katika nchi hii, nasita kuanzisha familia kwenye ardhi hii iliyo jaa neema, nikihofia fate ya mambo haya, najionea huruma nawaonea huruma vizazi vinavyoendelea kukua na vinavyokuja, lakini kuna sauti ndani inaniambia dont lose faith, huu ni wakati wa mpito, jisikie faraja kuishi wakati mambo haya yanatokea kwani kuna wengi waliziota siku kama hizi lakini hawakupata kuziona, mmoja wapo alikuwa ni baba yangu (RIP)


Mama paroko usilie utatuliza na siye, ngoja tugangamale, japo remy aliimba kilio cha samaki machozi huenda na maji, lakini haya ya kwetu hapa na watanzania wengine hayawezi kwenda hivi hivi, bahari itabadilika rangi tu......lets keep on knocking
 
Hivi mnaona fahari gani kuweka mambo ya siri hadharani namna hii? Hii ripoti ilikuwa ni kwa ajili ya kamati teule, nyinyi sijui mmefanya nini mkaipata. Kwa kweli hamuisadii serikali kwa kuweka mazungumzo nyeti kama haya hadharani. Nakubali inaonesha jinsi gani wanasheria wetu walivyo wadhaifu katika mambo ya mikataba, lakini hii peke yake si sababu tosha ya kuweka ripoti nzima kwenye mtandao.

Natoa ushauri, kuna mambo mengine msithubutu kufanya hivi mnakaribisha matatizo. Niliwaonya mapema kuhusu JF mkadhani ninawatania. Mnaweza kuwa nguvu ya mabadiliko lakini wakati mwingine ni hapa JF panapohitaji mabadiliko.

asante.
 
Hivi mnaona fahari gani kuweka mambo ya siri hadharani namna hii? Hii ripoti ilikuwa ni kwa ajili ya kamati teule, nyinyi sijui mmefanya nini mkaipata. Kwa kweli hamuisadii serikali kwa kuweka mazungumzo nyeti kama haya hadharani. Nakubali inaonesha jinsi gani wanasheria wetu walivyo wadhaifu katika mambo ya mikataba, lakini hii peke yake si sababu tosha ya kuweka ripoti nzima kwenye mtandao.

Natoa ushauri, kuna mambo mengine msithubutu kufanya hivi mnakaribisha matatizo. Niliwaonya mapema kuhusu JF mkadhani ninawatania. Mnaweza kuwa nguvu ya mabadiliko lakini wakati mwingine ni hapa JF panapohitaji mabadiliko.

asante.

http://wikileaks.org

TO RID THE WORLD OF NAZISM!!
 
Hivi mnaona fahari gani kuweka mambo ya siri hadharani namna hii? Hii ripoti ilikuwa ni kwa ajili ya kamati teule, nyinyi sijui mmefanya nini mkaipata. Kwa kweli hamuisadii serikali kwa kuweka mazungumzo nyeti kama haya hadharani. Nakubali inaonesha jinsi gani wanasheria wetu walivyo wadhaifu katika mambo ya mikataba, lakini hii peke yake si sababu tosha ya kuweka ripoti nzima kwenye mtandao.

Natoa ushauri, kuna mambo mengine msithubutu kufanya hivi mnakaribisha matatizo. Niliwaonya mapema kuhusu JF mkadhani ninawatania. Mnaweza kuwa nguvu ya mabadiliko lakini wakati mwingine ni hapa JF panapohitaji mabadiliko.

asante.


Una maana gani? Mbona imekuuma sana. Sababu za kutokuweka ulizo nazo ni zipi? Hebu tueleze sababu badala ya emotions tu .Wao mbona hawa tutendei mema kama wewe unadhani doc zao zisiwe hapa?
 
Hivi mnaona fahari gani kuweka mambo ya siri hadharani namna hii? Hii ripoti ilikuwa ni kwa ajili ya kamati teule, nyinyi sijui mmefanya nini mkaipata. Kwa kweli hamuisadii serikali kwa kuweka mazungumzo nyeti kama haya hadharani. Nakubali inaonesha jinsi gani wanasheria wetu walivyo wadhaifu katika mambo ya mikataba, lakini hii peke yake si sababu tosha ya kuweka ripoti nzima kwenye mtandao.

Natoa ushauri, kuna mambo mengine msithubutu kufanya hivi mnakaribisha matatizo. Niliwaonya mapema kuhusu JF mkadhani ninawatania. Mnaweza kuwa nguvu ya mabadiliko lakini wakati mwingine ni hapa JF panapohitaji mabadiliko.

asante.

I understand your frustrations Bi . Senti 50......and if you were really smart yould would understood our frustartions too..........at least out of our frustrations we wanna do something positive to our beloved country........we don't wanna our bus into the ditch!!!.........thats all and nothing more........

Mkuu Enigma na Lunyungu
tuendelee kulijenga Taifa letu..............hao watu wanaopata mishahara kutokana na walipa kodi.......halafu wanataka kuwanyanyasa hao hao walipa kodi.......this time wameula wa chuya........we will use any opportunity possible kufichua uozo sio kwa nia mbaya bali ni katika kujenga UADILIFU ndani ya serikali yetu
 
Mkuu Enigma,

Heshima mbele, kazi nzuri mkuu, endelea kutuletea hiii Ngwasuma mkuu, ila nitakutafuta week end mkuu, saafi sana!
 
Mikataba ya namna hii inafanywa kwa kusudi na wanasheria wetu, il ikuweka loopholes za kufanyia ufisadi.
ni dhahiri kuwa nia ilikuwa ni kuwapa richmond ili watu wale mamilioni ya pesa, na haikuwa kilio cha ukosefu wa umeme kwa wananchi.

Aliouonyesha mkataba, kama anao na mwengine pia auweke. hatutaki kufanywa kama watoto wadogo. watuwekee vitu dhahiri, wasitake kuficha makucha yao kwa kupitia ATI MIKATAbA YA SIRI.

Kuna siri na pesa za umma?
 
Hivi mnaona fahari gani kuweka mambo ya siri hadharani namna hii? Hii ripoti ilikuwa ni kwa ajili ya kamati teule, nyinyi sijui mmefanya nini mkaipata. Kwa kweli hamuisadii serikali kwa kuweka mazungumzo nyeti kama haya hadharani. Nakubali inaonesha jinsi gani wanasheria wetu walivyo wadhaifu katika mambo ya mikataba, lakini hii peke yake si sababu tosha ya kuweka ripoti nzima kwenye mtandao.

Natoa ushauri, kuna mambo mengine msithubutu kufanya hivi mnakaribisha matatizo. Niliwaonya mapema kuhusu JF mkadhani ninawatania. Mnaweza kuwa nguvu ya mabadiliko lakini wakati mwingine ni hapa JF panapohitaji mabadiliko.

asante.

Babako akikaa vibaya na Msuli wake unamwambia amekaa vibaya au wewe unaondoka?? Sasa kama wewe unaona haya mambo ya siri hayafai kuanikwa hapa nenda kalale hakuna anayekulazimisha kuangalia. Huyu si baba yetu. Kakaa uchi tena kwa makusudi si mara moja, si mara mbili ila ndo kafanya mazoea ya kukaa uchi ili tumwachie sinia la ubwabwa. Safari hii tunaye tu tunamwambia ukweli. Katuchosha hana aibu wala nini. Wewe ukiona soo anza vinginevyo mwambie kabisa kuwa akija barazani ajisitiri sisi si Watanzania wa jana.
 
Rais wangu Kikwete, Richmond ni laana



Pascally B. Mayega


RAIS wangu Kikwete, nilipoandika makala yangu ya kwanza kabisa nilianza hivi: Laiti kama ningelikuwa mtabiri, ningetabiri hatima ya Rais wangu. Ningetabiri mustakabali wa nchi yangu. Ningemtabiria Rais wangu kama mtabiri wa Julius Kaizari alivyomtabiria Rais wake. Alimwambia: Kaizari jihadhari na tarehe za katikati ya mwezi Machi. Leo mimi ningetabiri: Rais wangu jihadhari na kurasa zinazokuja za ufunuo wa Richmond na EPA.

Rais wangu, katika makala iliyofuatia nilianza hivi: Mimi siyo mwandishi wa makala. Mimi ni mwandishi wa vitabu. Ukiona naandika makala sasa ujue utabiri wa wahenga unatimia. Walisema: Iko siku mawe haya yatakuja kuzungumza.
Rais wangu, kwa kuwa mimi si mtabiri na kwa kuwa mimi si mwandishi mzuri wa makala, na haya mawe sasa yamekwishakuzungumza, basi naona heri niandike hii makala iwe ndiyo makala yangu ya mwisho. Ada ya mja hunena muungwana ni kitendo.

Wengine husema ahadi ni deni. Naona sasa yanipasa niwarejee wasomaji wangu wa kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu. Niliwaahidi kuwa katika toleo lijalo majibu kuhusu kuweza au kutoweza kwa Rais ajaye yatapatikana. Mwisho kuna swali:

Je Rais aliyechaguliwa alikidhi matarajio ya waliomchagua? Na majibu ya maswali mengine.
Rais wangu, mchambuzi nguli, ndugu wa maswali magumu, Ansbert Ngurumo, katika uchambuzi wake wa Februari 24, 2008 aliandika hivi:
Maana tukizingatia Tanzania ya mzee Mwinyi ilipoishia, na mzee Mkapa alipoitoa na kuifikisha kwa miaka 10; tukipalinganisha, na ujanjaujanja na usanii unaofanyika sasa katika miaka miwili tu ya utawala wa Kikwete, baadhi yetu tunachelea kusema kwamba Watanzania walifanya makosa kukifungua kile ambacho kilifungwa na Mwalimu Nyerere... Na hapo ndipo ulipo ushindi wa Lowassa dhidi ya Nyerere. Mtandao wa Lowassa haukufa ukageuka na kuwa mtandao wa Kikwete.

Rais wangu, baada ya kusoma maneno haya nikayakumbuka maneno ya Mwalimu aliposema: Mkiwachagua vijana hawa watawapeni shida. Nimejikuta sina la kufanya isipokuwa kwa faida ya wasomaji wangu nalazimika kufafanua yale niliyoyandika katika Butiama kuna Kaburi.

Nilisema nilibahatika kualikwa nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Msasani, jijini Dar es Salaam. Alikuwa anazindua kitabu chake, Majukumu ya Nchi za Kusini. Katika maisha yangu ya kumfahamu Mwalimu nilikuwa sijapata kumsikia akiongea kwa hisia kali kama siku ile. Nathubutu kusema Mwalimu aliapiza.
Aliusia. Alitoa tamko ambalo kulivunja ni kujitafutia laana. Baadhi ya maneno yake yalikuwa hivi: ...Watu wazima wameenda Zanzibar, wakaamua waliyoyaamua. Wamerudi hawatuambii wameamua nini...

Najua mmekwishaiacha siasa ya Ujamaa na Kujitegemea na mtu kutaka kuisemea sasa itakulazimu uwe na moyo mkubwa kama wa mwendawazimu... Lakini Paolo... Paolo... na wengine, nawaambieni... (kimya kidogo, kisha kwa sauti ya juu). Mkilifuta kabisa Azimio la Arusha... (kimya kidogo kisha kwa msisitizo) Mtakuja kupata shida sana baadaye.
Paolo aliyekuwa anaitwa na Mwalimu hapo alikuwa mtu mkubwa sana serikalini. Sijui siku hizi yuko wapi. Lakini mara ya mwisho nilimsikia wakati wa pilipilika zake na Chavda wakimkwepa Mrema. Sisi tulikuwa tunamwita Paul.
Rais wangu, kilichonishtua mimi ni pale Mwalimu alipokuwa akisema na wengine. Kila aliposema na wengine, Mwalimu alimkazia macho waziri ambaye tulikuwa tumekaa kwa kukaribiana sana. Alimwita na wengine.
Hakumtaja jina hata mara moja. Baadaye tulipoingia katika chumba maalumu cha Mwalimu kwa maongezi ya faragha, alimshambulia waziri yule kwa maneno ya moja kwa moja kuhusu wizara yake. Naye alijibu: Tumekusikia Mwalimu, tumekusikia Mwalimu. Safari hii nilikaa mbali kidogo na waziri kuogopa macho makali ya Mwalimu.
Sononeko la Mwalimu lilikuwa dhahiri. Alionekana kama mtu anayeongea na mijitu isiyosikia. Mwalimu akiwa hai, waziri yule hakuwemo katika Baraza la Mawaziri lililofutwa.

Rais wangu, Baba wa Taifa alielewa fika kuwa wenye uwezo wa kulifuta Azimio la Arusha ni viongozi. Si wananchi. Hivyo aliposema: Mtakuja kupata taabu sana baadaye, alikuwa anawaapiza viongozi, si wananchi. Na hili ndilo linalotokea sasa. Wengine wanajiuzulu.

Wengine wanaondolewa. Ndesamburo akisema kama China hawa wangenyongwa, wanapapatika. Wananchi wanaposema wafilisiwe wanatetemeka na kutoka jasho katika makasri yao yenye mfano wa friji. Viongozi wanatikisika. Mwisho wao sasa ni mashaka matupu.

Rais wangu, kipindi chote hiki wananchi walikuwa safi. Hakuna aliyetikisika. Waliendelea vema na taabu zao za kila siku. Nchi si viongozi peke yao. Kusema nchi imetikisika ni kupotosha ukweli. Mtikisiko wa viongozi mafisadi hauwezi kuwa mtikisiko wa nchi. Nchi haikutikisika. Mafisadi bado wanatikisika. Wataendelea na laana ya Baba wa Taifa mpaka mwisho wa ufisadi wao.

Sasa wanaanza kujieleza wenyewe wakidhani wanajitetea. Wengine wanalipa wananchi ili wakusanyike. Wengine kwenye vyombo vya habari. Eti ajenda 21. Wanajisasua nguo mwilini mpaka watabaki watupu. Ingekuwa ni bora kwao wangebaki kimya, wananchi wakawadhania kuwa ni wezi, mafisadi, kuliko wanaposema sasa na kuthibitisha hivyo.

Kuna wale ambao upeo wao wakufikiri ni mdogo, wanatafuta sababu kama udini, ukabila, ukanda na sababu nyingine za kijinga kama hizi. Eti ripoti ya Richmond inanuka hujuma dhidi ya watu wa Monduli. Mawazo ya mtu aliyefilisika kabisa. Mawazo ya mtu anayekiri uovu alioufanya. Mtu yeyote anayetaka kutuingizia ukabila au udini katika ufisadi huu alaaniwe na sisi wote. Ashindwe na alegee. Mfa maji huyu. Anyoshe shingo yake, apokee stahili yake kwa amani.

Rais wangu, kwa nini nayajutia maneno ya Mwalimu sasa? Hivi kweli viongozi wetu, msingelifuta Azimio la Arusha wananchi wangekutana wapi na Richimond? Richmond ambayo bila huruma iliyatumia maumivu ya wananchi yaliyotokana na ukame kuwafanyia ufisadi wa kiwango cha juu kabisa.

Richmond ambayo serikali imekiri kuwa ni kampuni hewa, lakini bado inaendelea kuilipa hiyo hewa shilingi milioni 152 kila siku bila kuuziwa chochote. Richmond ambayo serikali inakiri mbele ya wananchi wake kuwa haijui inamlipa nani. Lakini inalipa kila siku bila kukosa. Richmond ambayo imekutanishwa na wananchi kwa nguvu ya ofisi ya Waziri Mkuu.

Sasa gazeti limeandika J.K. amlilia Lowassa. Eti umesema kwa utendaji kama huu, amelitumikia taifa kwa ujasiri na uzalendo mkubwa na kwamba alikuwa rafiki kikazi na kimaisha. Na sasa amepata ajali ya kisiasa. Si siri wananchi wameipokea ajali hii kwa shangwe. Wameanza tena kuwa na matumaini yaliyokuwa yamepotea.

Wakati wewe unamlilia, mimi namhurumia mtu huyu! Yuko mtaani peke yake. Kama kweli alikuwa rafiki, muwaishe kwenye vyombo vya sheria ili vikamsafishe. Vingenevyo chukua jukumu uwaeleze wananchi pesa zao milioni 152 zinazoendelea kulipwa kila siku bila kukosa analipwa nani? Hili ni muhimu sana liwekwe wazi mapema maana wananchi wengine wanaweza kudhani analipwa yeye au marafiki zake.

Hivi tunavyosema milioni 152 zinaendelea kulipwa kila siku, bila kununua chochote kwa kampuni hewa, waponda kokoto wanapiga hesabu zao. Wamachinga na wapiga debe nao wanapiga hesabu. Wanafunzi wa elimu ya juu wanapiga hesabu, wangesoma wangapi bure.

Wale wanaofiwa na ndugu zao kila siku kwa kukosa fedha ya matibabu wanawakumbuka marehemu wao. Wao wenyewe hawana uhakika wa maisha yao.

Wastaafu wazee wetu waliolitumikia taifa hili kwa uadilifu mkubwa ambao sasa wanalipwa pensheni ya sh 20,000 kwa mwezi au sh 670 kwa siku wanapiga hesabu.

Walimu wanaodai na wafanyakazi wa kima cha chini wanapiga hesabu, ambazo kila jawabu linavimbisha mioyo yao zaidi kwa hasira. Hawa hawatakoma kumlilia Baba wa Taifa. Na kwa kufanya hivyo, laana kwa viongozi mafisadi nayo haitakoma.
Rais wangu, ni nani aliwatuma wananchi kwenda kugawana mashamba na mali za Gavana Ballali? Nani aliwachochea wananchi kuwachoma moto vibaka? Machungu yote haya wananchi wataendelea kuwaona mafisadi wao kwa macho tu?
Lazima uwalinde watuhumiwa hawa kwa kuwapeleka mahakamani haraka. Watakapoangukia katika mikono ya wananchi wenye hasira kali atalaumiwa nani? Wananchi wanataka fedha yao irudiswe. Tuwarudishie mali yao kabla hawajaanza kugawana za kwetu.

Walionyanganywa mifugo pekee iliyokuwa imebaki au vyombo kama baiskeli, walioezuliwa mabati kwenye nyumba zao au kulazimika kujifungulia katika ofisi za watendaji na wale waliofungwa kwa kosa la kukosa fedha za kulipia ujenzi wa madarasa, leo wanapoambiwa kuna milioni 152 zao zinalipwa kwa kampuni hewa, nani anaweza kujua ukubwa wa fundo lililowakaba moyoni?

Maisha ya kifahari wanayoishi watuhumiwa ndiyo yaliyodunisha maisha ya wananchi hawa. Wamedhulumiwa. Wameibiwa. Hasira ya wananchi hawa dhidi yao ni kali, ngumu, tena inatisha. Ee Mungu wanusuru watu hawa!
Rais wangu, ulipovunja Baraza la Mawaziri nilikuuliza, Mawaziri wapya utawapata wapi? Ona sasa, umetuletea mawaziri wa zamani ambao wananchi wamekwisha kuwazomea.
Utawanunulia nguo gani za kutokea upya mbele za watu? Sasa tuna waziri ambaye hata kujibu swali dogo tu la nyongeza bungeni ambalo halikuandikiwa majibu, kwake haiwezekani.
Mtuhumiwa wa wizi mkubwa katika Benki Kuu eti naye ni waziri mpya. Msimamizi wa mikataba sumu karibu yote inayozidi kulinyongonyeza taifa, eti naye ni waziri mpya. Huyu mwenye migodi ambaye alipokuwa waziri wa zamani alifanya ndege za jeshi kama teksi ya kuendea kwao kusalimia, mikataba ya migodi yake imechunguzwa? Eti sasa naye ni waziri mpya.
Rais wangu, kama lengo la kuunda baraza jipya ilikuwa ni kuunda chombo safi, basi hawa wamelichafua. Sote twafahamu kuwa nzi akidondekea katika glasi ya maziwa, maziwa yote huwa hayafai tena.
Katika mapambano ya ufisadi, kwa hili tumepiga hatua moja kubwa kurudi nyuma. Kama yaliyotokea bungeni si unafiki. Hata kama ni uoga wa uchaguzi Mkuu ujao. Na kama ni kweli sera ya chama mbele wananchi wakafie mbele itakuwa imelegezwa na maslahi ya wananchi yatawekwa mbele, wabunge safi wa CCM watapimwa kwa hili. Watawazomea mawaziri hawa ndani ya Bunge lenyewe.
Sasa tuna waziri mpya ambaye yeye mwenywe ni wa zamani. Unaweza ukadhani kuwa ndiyo hirizi ya baraza. Kila baraza yumo, anachokifanya hakuna, miaka yote. Ingekuwa ni nguo imechuja kiasi kwamba hakuna anayeweza kusema kwa hakika rangi yake ya dukani ilikuwa rangi gani.
Mwandishi nguli Padri Privatus Karugendo ameandika hivi: Adam Malima alipoundiwa tume na Bunge alionyesha jeuri ambayo inaweza kuzua maswali juu ya utendaji wake. Kama Watanzania wana kumbukumbu, kuna wakati Malima na Zitto Kabwe walihojiwa kwenye kipindi cha TvT juu ya sakata la Buzwagi.
Majibu yake na utayari wake wa kutaka kuwakaribisha wawekezaji wa kila aina jimboni kwake, pia ni jambo la kutilia shaka uwezo wa utendaji kazi wake.
Nilikiangalia kipindi hicho. Mchango wake bungeni kuhusu Buzwagi pia niliusikia. Awamu ya nne, imefuta kabisa heshima yote aliyokuwa anapewa mtu anapoteuliwa kuwa waziri.
Wapo katibu kata hata baadhi ya wenyeviti wa Serikali za Mitaa wenye sifa na uwezo wa kuwa mawaziri na wakaheshimika. Tunapoletewa mawaziri ambao kwa maoni ya wengi hata sifa za ukatibu kata hawana, tuna haki ya kuuliza uongozi wa nchi yetu, unatupeleka wapi?
Bado kidonda hakijapona. Wananchi bado wana uchungu wa fedha zao zaidi ya milioni mia moja zilizotumika kuthibitisha uzushi wa kipuuzi aliouanzisha bungeni. Kwa kuwa ilithibitika kuwa alisema uongo, wananchi wataendelea kudai adhabu dhidi yake mpaka itakapotolewa.
Kinyume cha hapo shilingi milioni mia moja za maskini walipakodi wa nchi hii zitabaki juu ya kichwa chake kokote atakakokwenda. Hili Mwenyezi Mungu atalisimamia maana hatakubali wananchi wageuzwe mpira wa malapulapu. Jina la Waziri Mkuu aliyejiuzulu lilitajwa kumbeba na vyombo vya habari. Sasa haya ni mazalia? Kwa nini hamtaki harufu mbaya ya Richmond iondoke kabisa? Hasara wee!
Rais wangu, mafisadi wapo, lakini wanawema pia wapo katika nchi hii hii. Reginald Mengi, mtu wa Mungu, wakati matajiri wenzake wanahangaika huku na huko kujibu au kukanusha tuhuma mbalimbali za kifisadi dhidi yao, yeye kutwa anahangaika na walemavu wake, wagonjwa wa moyo, waathirika na maskini ambao hawakujaliwa.
Kwa misaada yake mbalimbali kwa madrasa na jamii zingine bila kujali itikadi ya kisiasa, kabila au dini, Mungu atamlipa.
Najua alivyoumia kuona maskini wale wale anaowasaidia kwa kile kidogo alichonacho, wanakamuliwa zaidi ya sh milioni 100 kugharamia upuuzi. Asikate tamaa.
Mema yote anayoifanyia jamii yatageuka moto mkali wa adhabu dhidi ya wafitini wake. Aendelee kuwasaidia wenzetu wenye kuhitaji ambao wako vile walivyo kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.
Aelewe kuwa siku zote wanaotetea haki za wengi hukumbwa na misukosuko mingi. Hawa wataishi hata baada ya kifo. Watakumbukwa na vizazi vingi vijavyo, naam, pamoja na wote walioumizwa au kulazimishwa kuuondoka ulimwengu huu kwa sababu waliwaudhi wakubwa na hivyo wakawatanguliza mbele ya haki.
Rais wangu, kama tunayafanya haya bila kuelewa, basi Mungu atusamehe. Lakini kama tumeyafanya kwa lengo la kulinda ufisadi na mafisadi, basi laana ya Baba wa Taifa iko pale pale.
Mbunge amesema wakipita mtaani watoto wanaulizana: Wanafiki waseme ndiyo. Wanajibizana: Ndiyoooooo! Hapa ndipo kasi ya viwango feki ilipolifikisha Bunge letu. Kudharauliwa hata na watoto wa mitaani.
Kujiuzulu mpaka aundiwe tume. Saa imeenea ambako wabunge waadilifu hawatakubali kubeba mafisadi wachache ndani ya chama chao. Sasa imeenea ambapo wabunge waadilifu watataka kurejea maagano ya Azimio la Arusha. Na tuipishe basi laana ya Baba wa Taifa kwa viongozi wetu ili tuwarudishie wananchi matumaini yao.
Rais wangu, katika hili waonyeshe watu wako mfupa wako katika nyama ya mwili wako. Kata katikati ili ubaki na kipande kimoja. Usitake kuwa huko na huku. Chagua bega.
Wale waliokwishaanza kutafunwa na laana ya Baba wa Taifa waache waendelee kutafunwa. Wengi watafuata, Mwakyembe kafungua mzinga wa nyuki, watu wanatoka nduki. Kuwahurumia ni kujitafutia janga wewe mwenyewe. Richmond itafungua mengi na itaifungua Tanzania. Ajidhanie amesimama aangalie asianguke. Maisha bora kwa kila Mtanzania bila Azimio la Arusha HAIWEZEKANI.
Mungu akubariki msomaji wangu.
Simu: 0713 334239
Email: ngowe2006@yahoo.com
 
Ndugu yangu Paskali, Rais wako unadhani ataweza kuchagua bega moja? Ni vigumu, ila nguvu ya wananchi itamwamulia ni bega lipi achague!
 
Back
Top Bottom