Mama...
Nimependezewa sana na hili tusi kuwa mimi ni nguruwe.
Kwa nini mtu anatukana?
Mtu anatukana pale anapoghadhibika na kuwa hana zaidi la kufanya kuondoa ghadhabu zake ila kutoa matusi.
Nini kilichokuudhi wewe?
Umaghadhibika kwa kuwa hutaki kusikia historia ya Waislam.
Hii si mara yangu ya kwanza kutukanwa.
Mara ya kwanza kutukanwa ilikuwa mwaka wa 1988 baada ya jarida maarufu Africa Events lililokuiwa linachapwa London kuchapa makala yangu, ''In Praise of Ancestors.''
Siku zote historia ya TANU na kudai uhuru wa Tanganyika ilikuwa inaanza na Mwalimu Nyerere.
Katika makala ile niliandika kuwa historia ya uhuru imewasahau waasisi wa TANU mfano wa Abdul Sykes na ndugu yake Ally Sykes, Saadan Abdul Kandoro, John Rupia nk.
Makala ikaeleza pia mchango wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika (Umoja wa Waislam wa Tanganyika) ulioundwa mwaka wa 1933 baada ya kuundwa kwa African Association 1929.
Dr. Mayanja Kiwanuku kutoka CCM Dodoma Idara ya Uhamasishaji Umma akajibu makala yangu kwa jibu kali sana.
Alighadhibishwa na kuona nimeiunganisha historia ya TANU na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na nimetaja mchango wa Waislam.
Majibu yake kwangu yalijaa kejeli na vitisho na mwisho akanitukana kwa kuniita, ''Mbilikimo.''
Nikawa nimefahamu kuwa kilichomghadhibisa ni ile historia ya Waislam katika siasa za Tanganyika.
Hili linawachoma watu wengi sana na limewapendeza wengi pia.
Ningeweza kutoa taarifa kwa Adm kuwa umeniita nguruwe na ukapigwa ban.
Mimi sitaki hili.
Nataka ubakie hapa usome niandikayo.