Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Huyu mzee ni mtu mzima na msomi mtu aliyetembea nchi mbalimbali duniani na kupata exposure kubwa lkn nakiri kuwa vyote hivyo havijasaidia kumkomboa utumwani. Ni mtu mdini, mnafiki na mchonganishi ukimpa madaraka mtu kama huyu ni hatari kuliko ukimwi au corona
 
Ralph...
Tundu Lissu hanihitaji mimi kumsemea halikadhalika Freeman Mbowe.
Hawa wana watu wa kutosha kuwasimamia.

Nakuwekea hapo chini kisa kingine ambacho hakuna chombo cha habari kiliripoti ingawa walikuwa na taarifa zote:

Mauaji ya Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir wa Kijiji cha Madina

Tarehe 25 Oktoba 2013 siku ya Ijumaa Waislam katika kujiji cha Madina walishambuliwa na askari na Waislam wawili waliuawa kwa kupigwa risasi.

Waislam hao ni Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir.
Hamisi Ramadhani amezikwa Handeni katika makaburi ya hospitali maiti ilipokuwa imehifadiwa.

Abu Zubeir maiti yake ilihamishwa kutoka Handeni kwa kuwa hospitali haikuwa na chumba cha barafu cha kuhifadhi maiti ikapelekwa Korogwe.

Ndugu zake Abu Zubeir waliogopa kujitokeza kuchukua maiti yake kwa kuwa askari walikuwa wakimkamata kila aliyefika hospitali kuuliza taarifa za maiti hao.

Haijulikani nani wamemzika Abu Zubeir na hadi sasa ndugu zake hawajajitokeza kujua ndugu yao kazikwa wapi kwa hofu ya kukamatwa.

Sheikh Waziri anasema yeye na wenzake walikabidhiwa maiti ya Hamisi Ramadhani siku ya Jumapili na siku hiyo hiyo walimzika katika makaburi ya hospitali sanda yake ikiwa shuka ile iliyofunika maiti yake.

Sheikh Waziri anasema juu ya kuwa maiti zile zilikuwa hazikuhifadhiwa katika baridi hali ya maiti ilikuwa nzuri kabisa.

Mashuhuda wa kifo cha Hamisi Ramadhani wanasema alipopigwa risasi Hamisi Ramadhani alishahadia kwa sauti na kila mtu alisikia shahada ile.

Allah awalaze mahali pema peponi.
Amin.

Maelezo Mafupi ya Sheikh Waziri Shuza

Siku ile ya mashambulizi tarehe 25 Oktoba 2013 Sheikh Waziri akiwa kama kiongozi wa Waislam alipigiwa simu yeye akiwa Mkata katika shughuli za biashara kujulishwa kuwa kuna watu wameuawa kwa hiyo akaombwa aende Hospitali ya Wilaya Handeni akaagalie waliouawa na majeruhi.

Taarifa zilizomfikia alipofika Handeni jioni ile zilikuwa taarifa za kuogofya.

Hali pale hospitali ilikuwa ya kutia hofu palikuwa na ulinzi mkali hospitali nzima imezungukwa na maaskari. Kwa ajili hii Sheikh Waziri hakuweza kwenda hospitali siku hiyo na hata siku ya pili yaani Jumamosi hakuweza kwenda.

Waislam walibakia majumbani kwao wakisubiri na kuomba dua.

Sheikh Waziri akiwa kiongozi alipiga marufuku shura ya aina yoyote msikitini kuhusu mauaji yale kutafuta salama.

Waislam walikuwa wanakuja kuswali na wakimaliza wanaondoka kurudi majumbani kwao.

Lakini Sheikh Waziri akawa na wasiwasi kuwa ikiwa hatafanya jambo kuna hatari ya wale marehemu kutozikwa Kiislam.

Sheikh Waziri ilipofika Jumapili ikamjia fikra ya kumpigia diwani Mushashi. Alimweleza diwani huyu kuwa Waislam wangeshukuru kama serikali wangeruhusu maiti zile wapewe ili wazizike.

Haukupita muda diwani akamfahamisha Sheikh Zuberi kuwa anaweza kwenda hospitali na kuonana na Mganga Mkuu kwa ajili ya kupewa zile maiti mbili.

Lakini Mganga Mkuu akasema kuwa amri aliyopewa na Mkuu wa Mkoa Bi. Chiku Galawa ni kuwa maiti zile zipelekwe Tanga kwa mazishi ikiwa ndugu zao hawajajitokeza na huko maiti hizo zitachangwanywa na maiti nyingine za wasio na ndugu na zitazikwa na serikali.

Ikawa sasa lazima Mkuu wa Mkoa asubiriwe ili abatilishe amri yake ya awali na endapo ruksa itatoka Waislam wa Handeni watazizika maiti hizo.

Sheikh Hamisi akaondoka kusubiri amri ya Mkuu wa Mkoa.

Mwishowe maiti ilitolewa kwa Sheikh Waziri baada ya mazungumzo marefu kati ya Mganga Mkuu na Sheikh Waziri ikizingatiwa kuwa kwa siku tatu hakuna ndugu wa marehemu aliyejitokeza kuchukua maiti.

Sheikh Waziri alifunuliwa maiti ya Hamisi Ramadhani na Mganga Mkuu mbele ya askari.akaonyeshwa jeraha la mguuni alipopigwa risasi.

Shuka haikufunuliwa kuoneshwa majeraha mengine...
Sheikh Waziri hakuwa na haja ya kutaka mengi lililomshughulisha ilikuwa ni kupata maiti ili waisiitiri.

Sheikh Waziri anasema ilikuwa wazi kuwa Polisi na Mganga Mkuu walikuwa wameshakubaliana nini cha kufanya wakati watakapoonyesha maiti kwa ndugu zao.

Mganga Mkuu alionyesha jeraha la risasi mguuni akisema kuwa hapo ndipo zilipotoka damu nyingi kusababisha kifo cha Hamisi Ramadhani.

Lakini wao walikuwa na habari kamili kutoka kwa mke wa marehemu na jamaa wengine kuwa ndugu yao alikuwa amepigwa risasi katika kibofu cha mkojo na kwa hakika sehemu ile ingawa ilikuwa imefunikwa na shuka palikuwa na uvimbe mkubwa.

Sheikh Waziri na Waislam wachache walimzika ndugu yao usiku katika makaburi hapo hospitalini.
Wewe mzee acha mentality ya udini. Unafeli sana...watu wamekueleza ukweli kabisaa..waislam na wakristo wote wamekueleza ukweli kabisaa ..achana na mentality ya udini. Ukifuatilia watu wa makabila yote na dini zote wanakumbana na changamoto..zungumzia watanzania wotee
 
Tukuamini wewe au mahakama?
Mama....
Mimi siandiki uniamini hata kidogo.
Naandika kukueleza kile usichokijua.

Nilipata kuulizwa swali kama hilo lako.
Muulizaji anasema, "Unasema ikiwa unataka kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika inabidi tuanze na Abdul Sykes. Mimi sijamsoma huyu mtu popote katika historia ya Tanganyika. "

Tuko mubashara kipindi cha televisheni.

Nilimuhurumia yule kijana kama ninavyokuhurmia wewe.

Nilitoa jibu langu: "Kadi ya TANU No. 3 ni Abdul Sykes kadi No. 2 ni Ally Sykes na kadi no. 1 ni Julius Kambarage Nyerere RANU Territorial President.

Unaweza kuamini upendacho."

Kutotajwa kwa Abdul Sykes hakuondoi ukweli kuwa historia ya TANU inaanza katika ukoo wao.

Ndugu yangu amini upendacho.
 
Huyu mzee ni mtu mzima na msomi mtu aliyetembea nchi mbalimbali duniani na kupata exposure kubwa lkn nakiri kuwa vyote hivyo havijasaidia kumkomboa utumwani. Ni mtu mdini, mnafiki na mchonganishi ukimpa madaraka mtu kama huyu ni hatari kuliko ukimwi au corona

Ndio kiongozi wa chokochoko za mwembechai,kuvunja bucha za nguruwe magomeni,kuingiza sera ya kuvalisha hijabu wanafunzi wa shule za msingi na sekondali,kiufupi huyo ni extremity gaidi aliyejificha.
 
Mbona hata haielewweki mzee. Kama kuna Jambo basi umeruka yale ya muhimu,hasa yanayowahusu makosa waliyofanya hao waislam. Kama umeifanyia uchunguzi wa miaka 10 kama ulivyosema,basi ulete kwa kueleweka. Lete kwa mtiririko ulio sahihi na kweli tupu. Ili tujadiri na kutolea uamuzi kwa Jambo lililo kamili

Halafu nimesoma naona nia yako unataka kutengeneza kwamba waislam wanaonewa.
 
Mama....
Mimi siandiki uniamini hata kidogo.
Naandika kukueleza kile usichokijua.

Nilipata kuulizwa swali kama hilo lako.
Muulizaji anasema, "Unasema ikiwa unataka kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika inabidi tuanze na Abdul Sykes. Mimi sijamsoma huyu mtu popote katika historia ya Tanganyika. "

Tuko mubashara kipindi cha televisheni.

Nilimuhurumia yule kijana kama ninavyokuhurmia wewe.

Nilitoa jibu langu: "Kadi ya TANU No. 3 ni Abdul Sykes kadi No. 2 ni Ally Sykes na kadi no. 1 ni Julius Kambarage Nyerere RANU Territorial President.

Unaweza kuamini upendacho."

Kutotajwa kwa Abdul Sykes hakuondoi ukweli kuwa historia ya TANU inaanza katika ukoo wao.

Ndugu yangu amini upendacho.
Hao wazee wako walikomeshwa na Mwalimu Nyerere. Wangeachwa hii nchi ingeshakuwa ya kidini. Hata wewe unaishia kubwabwaja kwasababu unajua huo moto utakaokuwakia ukivuka mipaka.
 
Mbaya zaidi mzee wetu umekaza fuvu, hautaki kuelewa
Ata waislamu wenzako wameamua wakae pembeni, jinsi gani peni yako ilivyo na udini

Sio kwamba swala la kibiti haulijui lahasha, upo bias Sana na UDINI

Kufumbia macho swala la kibiti au kutotoa neno linakuweka kwenye nafasi ya MNAFKI
Hili litachukua muda Sana kulitambua

Kutokuwepo kwako jf ni bora sana kuliko uwepo wako
 
Hao wazee wako walikomeshwa na Mwalimu Nyerere. Wangeachwa hii nchi ingeshakuwa ya kidini. Hata wewe unaishia kubwabwaja kwasababu unajua huo moto utakaokuwakia ukivuka mipaka.
Mama...
Unaandika hasira zimekupanda.
Huijui historia ya uhuru wa Tanganyika.

Hii ndiyo sababu unasema linalokujia kwa ghadhabu.
Nivuke mipaka gani sijaelewa hapo.

Moto uniwakie kwa kosa gani?
Mimi sibwabwaji.

Mimi naandika historia wewe hujapata kuisikia hata siku moja.

Wanahistoria wengi katika vyuo vikuu Afrika, Ulaya na Marekani wanafuata staili ya usomeshaji wangu katika somo la Nationalist Politics in Tanganyika.

Wanaanza na Kleist Sykes (1894 - 1949) katika African Association (1929) kisha wanamgusa Abdul Sykes 1950.

Hapa rejea zao ni Dictionary of African Biography (2011) na "The Life and Times of Abdulwahid Sykes..." (1998).

Nimo kama mwandishi katika Dictionary of African Biography.
Bahati mbaya sana kwako ikiwa historia hii inakuumiza.

1687805251736.png

1687805312519.jpeg
 
Mbaya zaidi mzee wetu umekaza fuvu, hautaki kuelewa
Ata waislamu wenzako wameamua wakae pembeni, jinsi gani peni yako ilivyo na udini

Sio kwamba swala la kibiti haulijui lahasha, upo bias Sana na UDINI

Kufumbia macho swala la kibiti au kutotoa neno linakuweka kwenye nafasi ya MNAFKI
Hili litachukua muda Sana kulitambua

Kutokuwepo kwako jf ni bora sana kuliko uwepo wako
Mkorea,
Kuhusu ugaidi nimeweka post #41 link ya muhadhara niliofanya University of Ibadan kuhusu tatizo hili.

Naamini post hiyo imekupita hukuiona.
Rejea nyuma.

Hapa JF nimechaguliwa Mwandishi Bora kwa miaka miwili mfululizo 2021 na 2022.
 
Mbona hata haielewweki mzee. Kama kuna Jambo basi umeruka yale ya muhimu,hasa yanayowahusu makosa waliyofanya hao waislam. Kama umeifanyia uchunguzi wa miaka 10 kama ulivyosema,basi ulete kwa kueleweka. Lete kwa mtiririko ulio sahihi na kweli tupu. Ili tujadiri na kutolea uamuzi kwa Jambo lililo kamili

Halafu nimesoma naona nia yako unataka kutengeneza kwamba waislam wanaonewa.
Village...
Huko unakosema wewe tumepita miaka mingi sana.
 
Umeingiza udini mahali ambapo hapastahili. Kutokana na maelezo yako mwenyewe Rajab alikamatwa kwa mara ya kwanza kwa sababu mtu aliyemuuzia hiliki alikataa kuzilipia ushuru. Ingawa ulikuwa ni uonezi mkubwa hakukamatwa kwa sababu ni muislamu. Umetuambia kuwa ndugu zake walienda kujaribu kumtoa ndio vurugu zikatokea ambapo mtu mmoja aliuawa. Ingawa bila shaka ndugu zake wengi kama sio wote walikuwa waislamu lakini hawakwenda kituoni kumtoa Rajab kwa sababu ni muislamu bali kwa sababu ni ndugu yao. Mkuu wa Mkoa unayemtaja Chiku alikuwa muislamu na sidhani kama alifanya unayomshutumu kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu.

Kugeuziwa kibao na kesi kugeuzwa kuwa ya ugaidi si kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu bali ilikuwa njia ya kuhakikisha kuwa hawachomoki kirahisi. Hata Freeman Mbowe alifunguliwa kesi ya ugaidi na hamna hata mmoja aliwahi kusema kuwa ilikuwa kwa sababu yeye ni mkristu na Rais muislamu.

Kama unayosimulia yana ukweli wowote ni dhahiri kuwa uonevu mkubwa umefanyika dhidi ya Rajab na ndugu zake. Kuingiza udini hakuwatendei haki maana unageuza suala lao kuwa la maonevu dhidi ya waislamu ( yanayofanywa na wakristu na vibaraka wao) wakati ni mfano mwingine wa watu kutumia nafasi zao kuwaonea na kuwafanyia ukatili binadamu wenzao. Badala ya hili suala kuwa letu wote maana watu wa imani zote wamewahi kufanyiwa ukatili (mfano Mdude Nyangali) nyie mnaligeuza kuni ya kuchochea chuki kati ya waislamu na wakristu. Sio vizuri mnavyofanya.

Amandla....
Umemueleza barabara!! na bayana.

Seme alishajichagulia upande so hamtoelewana.

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Anaitendea Vibaya sana Nchi yake kuingiza dini.

Mzee MS, katika utafiti wako sungusungu hao walikuwa Dini gani?
Asilimia 80 kama sio 90 ya wakazi wa handeni na viunga vgake ni waislamu.

Naweza sema asilimia 80 ya wakazi wa Tanga ni waislamu.

Mkoa wa pwani huu

Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Hivi waislamu mkoani Tanga, wako Handeni tu? Na kwanini wahisiwe ni magaidi wa Handeni, na sio Lushoto au Korogwe au kwingineko? Kuna wakati inataka utulivu na hekima ya juu kuelewa jinsi watu wanavyoleka mambo na kujificha kwenye kichaka cha kuonewa dini zao
80% na zaidi ya wakazi wa mkoa wa Tanga na wilaya zake ni waislamu.

Yawezekana mtana alipigwa au kuuwawa na waislamu wenzake.

Ila inatafuta sababu hapa au Kuna dini au kikunda Cha watu kinatafutwa kipewe lawama Ili kuonekana waislamu wanaonewa na dini zingine au mamlaka.

Hizi ni propaganda za kidini zenye kueneza chuki na kuharibu mshikamano kayiia Taifa.



Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom