Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Utingo,
Nakuomba uwe na subra.

Anza kuusoma huu uzi toka mwanzo uelewe mkasa wa Madina.

Baada ya hapo unaweza kuja na maswali.
Ok mkuu.....nimesoma tangu mwanzo au umeshawishika kuupa sula ya udini baada ya poor judgement ya mkuu wa mkoa?

But you know majority of these people (RCs) are just poor politicians who lack tools of analysis. To me kilichofanyika ni jinai tu baada ya mnunuzi wa hiliki kukataa kulipa ushuru wa hiliki yote kijiji kimoja. Na alikuwa sahihi. Na waliomfuata mkulima walikosea maana kisheria au utaratibu unaojulikana nchi nzima anayelipia ni mnunuzi, walipaswa wahangaike na mnunuzi tu na si mkulima mwanakijiji mwenzao.

Wao ndiyo walisababisha yote yaliyotokea na damu yote iliyomwagika na itakayomwagika iko juu yao
 
Mama...
Ukisoma makala zangu na ukachangia ni vyema sana kwangu na mimi nakuahidi nitakujibu kistaarabu.

Usikae kimya.

Tatizo ninaloliona kwako ni hasira na kutoa matusi.

Hii inaharibu mjadala.

Mkuu mohamed mimi naona ungeendelea kuelezea ILI sisi tujue unachoandika kinajikita katika udini kama watu wengi wanavyodai au kulikuwa na udhalimu juu ya watu uliowataja.
Embu jaribu kueleza kwa undani kwanini liwepo neno waislamu na si watanzania ungejikita kumaliza hii stori ILI tujue kiongozi
 
Kbsa bwana tashwishi.....MZee huyu Ni mvuruga amani na ninashangaha sna jf kuendelea kumpa tuzo mbali mbali na kuendelea kumvuga Happ alitakiwa awe amepigwa ban life ban
 
mwandishi mara nyingi kwa uandishi wake amejitanabaisha kuwa ni mwislamu mwenye chuki dhidi ya wasiyo waislamu. Unaposoma makala zake ni kama unasoma makala za al-shabaab. Ni mchochezi aliyepitiliza
 
Ungesema Wanakijiji 10 au ukipenda ungesema watu 10 kunyongwa.Ulipotia neno waislam 10 huo ni uchochezi na ujinga ulipitiliza.

Mzee unataka kuvuruga amani ya nchi kupitia mgongo wa dini sijui utakimbilia Sudan au Syria !.
 
Ntamfungia kesi MamaSamia2025 kwa kosa la kufananisha mnyama mwenye nyama pendwa ulimwenguni na lizeee lisilo na staha lizee lisilojitambua!

Nguruwe ana thamani kubwa sana
Kwa niaba yangu binafsi ninaomba radhi kwa kumfananisha mnyama mwenye nyama pendwa duniani na huyu mzee mpuuzi wa kuitwa Mohamed Said. Ninakiri kumkosea heshima Nguruwe.
 
Acha upumbavu.
 
Id yako na ulichokiandika vimenipa picha halisi juu ya kipi hasa unachokitaka.
 
Acha upumbavu.
Mama...
Nitakupa kisa cha Prof. Haroub Othman, Mwalimu Nyerere na kitabu cha Abdul Sykes.

Mimi ndiyo mapenzi ya Mwenyezi Mungu nimezaliwa 1952 wakati vuguvugu za kudai uhuru wa Tanganyika zinaanza.

Baba yangu ananihadithia anasema huo ndiyo mwaka alimuona Nyerere nyumbani kwa Abdul Sykes Mtaa wa Aggrey na Sikukuuu.

Baba yangu anasema pembeni Abdul alimfahamisha kuwa kuna mpango wa kuunda chama cha siasa kudai uhuru na Nyerere atakuwa kiongozi wa harakati hizi.

Kipindi hiki Abdul Sykes alikuwa TAA Secretary na Act. President.

Babu yangu Salum Abdallah alikuwa katika siasa za kupigania uhuru na alikuwa pia kati ya wafadhili wa TAA na TANU Tabora na pia akawa muasisi wa TANU na Tanganyika Railways African Union (TRAU).

Nilipokuja kusoma historia ya TANU nikagundua kuwa wale wote ambao nilikuwa nikiwasikia wakitajwa nyumbani kwetu katika historia ya TANU wote wamefutika.

Anatajwa mtu mmoja tu - Julius Kambarage Nyerere.

Siku moja nikamsikia baba yangu anasema, ''Hawa wanaweza vipi kuandika historia ya TANU wasimtaje Abdul?''

Lakini ndiyo ukweli uliokuwapo.

Historia ya TANU ipo lakini Abdul Sykes hayumo wala babu yangu hayumo na wazalendo wengi sana hawamo na wengi wao Waislam.

Hapa ndipo nikajiuliza kwa nini?

Nikaamua kuandika kitabu cha maisha ya Abdul Sykes kueleza harakati za kuunda TANU kupitia maisha ya Abdul Sykes na kwa kutumia Nyaraka za Sykes.

Prof. Haroub Othman alipokisoma kitabu changu alipata mshtuko mkubwa sana.
Akaomba miadi na Mwalimu.

Prof. Haroub akamwambia Mwalimu kuwa kitabu changu kimebadilisha historia yake (Nyerere) na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Prof. Haroub akamwambia kubwa ni kuwa hata ''legacy'' yake imeguswa pakubwa ni lazima Mwalimu na yeye aeleze historia ya maisha yake hadi kufika kuwa kiongozi wa TAA 1953 na kiongozi wa TANU 1954.

Ukipendezewa naweza nikaendelea na kisa hiki.

Kwa sasa tusimame hapa.

Kitabu ni hicho hapo chini:


The Life and Times od Abdulwahid Sykes (1924 - 1968)
The Untold Story of the Muslim Struggle Against British Colonialism in Tanganyika
(Minerva Press, London 1998)​
 

Utakua mgeni wa Muddy Said wewe. Good luck with that.
 
Duuuh inafikirisha hii..

naamini si haki kudhulumu haki ya mtu yeyote awe islam au budha..

kila penye neno muislamu hapo nadhani ungefaa kuweka mtanzania..
katika hukumu hiyo ..
Hata mm ananishabgaza sana kuweka neno waislam, kwa nn si watanzania ?
 
Mleta maada inaonyesha wazi utafita wako uliegamia upande mmoja..

Pia umeathirika na udini,

so conclusion fanya utafiti upande wa pili.
 
Kawasimulie wala nguruwe wenzako pale Kigogo Sambusa
 
Genius! 🙌🤛
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…