Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Sakata la Kupotea Rajab Omari Mtana na Hukumu ya Kunyongwa kwa Masheikh 10 Tanga

Mohamed Said haya matusi uliyoporomoshewa umeyataka mwenyewe.
Miaka hii watu wanataka amani ila wewe unachochea vurugu kwa kuanzisha mada za udini.

Usijivunie sana kupewa tuzo ya uandishi bora, hata GENTAMYCINE pamoja na upopoma wake alipewa tuzo ya michezo.
Kuna Watu bila Kumtaja GENTAMYCINE hamjisikii raha kabisa. Bebeni Mimba zangu basi ili mzae akina GENTAMYCINE Wengi.
 
Umeingiza udini mahali ambapo hapastahili. Kutokana na maelezo yako mwenyewe Rajab alikamatwa kwa mara ya kwanza kwa sababu mtu aliyemuuzia hiliki alikataa kuzilipia ushuru. Ingawa ulikuwa ni uonezi mkubwa hakukamatwa kwa sababu ni muislamu. Umetuambia kuwa ndugu zake walienda kujaribu kumtoa ndio vurugu zikatokea ambapo mtu mmoja aliuawa. Ingawa bila shaka ndugu zake wengi kama sio wote walikuwa waislamu lakini hawakwenda kituoni kumtoa Rajab kwa sababu ni muislamu bali kwa sababu ni ndugu yao. Mkuu wa Mkoa unayemtaja Chiku alikuwa muislamu na sidhani kama alifanya unayomshutumu kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu.

Kugeuziwa kibao na kesi kugeuzwa kuwa ya ugaidi si kwa sababu ya chuki dhidi ya waislamu bali ilikuwa njia ya kuhakikisha kuwa hawachomoki kirahisi. Hata Freeman Mbowe alifunguliwa kesi ya ugaidi na hamna hata mmoja aliwahi kusema kuwa ilikuwa kwa sababu yeye ni mkristu na Rais muislamu.

Kama unayosimulia yana ukweli wowote ni dhahiri kuwa uonevu mkubwa umefanyika dhidi ya Rajab na ndugu zake. Kuingiza udini hakuwatendei haki maana unageuza suala lao kuwa la maonevu dhidi ya waislamu ( yanayofanywa na wakristu na vibaraka wao) wakati ni mfano mwingine wa watu kutumia nafasi zao kuwaonea na kuwafanyia ukatili binadamu wenzao. Badala ya hili suala kuwa letu wote maana watu wa imani zote wamewahi kufanyiwa ukatili (mfano Mdude Nyangali) nyie mnaligeuza kuni ya kuchochea chuki kati ya waislamu na wakristu. Sio vizuri mnavyofanya.

Amandla....
…habari nilizowahi kusikia kuhusu kijiji cha ‘madina’ zinatisha! Hata kwenye hii taarifa haijasemwa kua kuna mtoza ushuru alieuwawa na pia polisi kutoka handeni kabla ya ffu kutoka tanga ambao ndio walioweza kudhibiti hali… pengine ni UMBEA TU
 
Hapa Kuna harufufu ya udini.
Waislamu 10?
Je isingekuwa waislam ungekuja kureport hapa?
Mmeshaanza.....
Mahakamani ndio kwenye haki.
Na mbona aliyehukumu hiyo kesi pia ni muislam na hujasema?
 
By the way hayo mawazo Yako MZEE MOHAMED una haki nayo kutashikilia kwa jinsi inayokupendeza hata hata kama Ina hatarishi mshikamano wetu kama TAIFA.

Pia sio lazima kwetu kuyakubali , kuyazingatia na kuyafuata kwa mujibu wako.



Sent from my Infinix X6511B using JamiiForums mobile app
 
Hapa Kuna harufufu ya udini.
Waislamu 10?
Je isingekuwa waislam ungekuja kureport hapa?
Mmeshaanza.....
Mahakamani ndio kwenye haki.
Na mbona aliyehukumu hiyo kesi pia ni muislam na hujasema?
Huyu mzee pamoja na usomi wake lakini anamapungufu makubwa ya udini ananifanya nifikirie Islam religion is inferiority complex .
 
Hapa Kuna harufufu ya udini.
Waislamu 10?
Je isingekuwa waislam ungekuja kureport hapa?
Mmeshaanza.....
Mahakamani ndio kwenye haki.
Na mbona aliyehukumu hiyo kesi pia ni muislam na hujasema?
Mbaya Zaid jaji mkuu Ni muislamu shida iko wapi wawafunge waislamu
 
Mohamed Said haya matusi uliyoporomoshewa umeyataka mwenyewe.
Miaka hii watu wanataka amani ila wewe unachochea vurugu kwa kuanzisha mada za udini.

Usijivunie sana kupewa tuzo ya uandishi bora, hata GENTAMYCINE pamoja na upopoma wake alipewa tuzo ya michezo.
mu
Guest,
Hili jambo la matusi limekuwa sehemu ya majibu katika historia ya kalamu yangu.

Lakini hili halijawa jambo la kunizuia mimi kuandika yale ninayoyajua.

Nikitaka ningekuwa natoa taarifa kwa Adm kuwa kuna mtu ameleta matusi katika mjadala na Adm hapo hapo anampiga "ban," yaani anamfungia.

Mimi huwa sifanyi hivyo kwa kuwa namtaka huyu anaetukana abakie niwe na yeye na aendelee kunisoma hata kama atarejea kutoa matusi.

Hakuna amani inayohatarishwa kwa watu kupeana habari za kweli.

Niko hapa jamvini muda mrefu sana na nimepata umaarufu mkubwa na wasomaji wengi.

Sijasikia kama amani imevunjika kwa sababu ya makala zangu.

Kinachotokea ni kutembelewa na vyombo vingi vya habari vya ndani na nje kufanya mahojiano na mimi.
 
Ralph...
Tundu Lissu hanihitaji mimi kumsemea halikadhalika Freeman Mbowe.
Hawa wana watu wa kutosha kuwasimamia.

Nakuwekea hapo chini kisa kingine ambacho hakuna chombo cha habari kiliripoti ingawa walikuwa na taarifa zote:

Mauaji ya Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir wa Kijiji cha Madina

Tarehe 25 Oktoba 2013 siku ya Ijumaa Waislam katika kujiji cha Madina walishambuliwa na askari na Waislam wawili waliuawa kwa kupigwa risasi.

Waislam hao ni Hamisi Ramadhani na Abu Zubeir.
Hamisi Ramadhani amezikwa Handeni katika makaburi ya hospitali maiti ilipokuwa imehifadiwa.

Abu Zubeir maiti yake ilihamishwa kutoka Handeni kwa kuwa hospitali haikuwa na chumba cha barafu cha kuhifadhi maiti ikapelekwa Korogwe.

Ndugu zake Abu Zubeir waliogopa kujitokeza kuchukua maiti yake kwa kuwa askari walikuwa wakimkamata kila aliyefika hospitali kuuliza taarifa za maiti hao.

Haijulikani nani wamemzika Abu Zubeir na hadi sasa ndugu zake hawajajitokeza kujua ndugu yao kazikwa wapi kwa hofu ya kukamatwa.

Sheikh Waziri anasema yeye na wenzake walikabidhiwa maiti ya Hamisi Ramadhani siku ya Jumapili na siku hiyo hiyo walimzika katika makaburi ya hospitali sanda yake ikiwa shuka ile iliyofunika maiti yake.

Sheikh Waziri anasema juu ya kuwa maiti zile zilikuwa hazikuhifadhiwa katika baridi hali ya maiti ilikuwa nzuri kabisa.

Mashuhuda wa kifo cha Hamisi Ramadhani wanasema alipopigwa risasi Hamisi Ramadhani alishahadia kwa sauti na kila mtu alisikia shahada ile.

Allah awalaze mahali pema peponi.
Amin.

Maelezo Mafupi ya Sheikh Waziri Shuza

Siku ile ya mashambulizi tarehe 25 Oktoba 2013 Sheikh Waziri akiwa kama kiongozi wa Waislam alipigiwa simu yeye akiwa Mkata katika shughuli za biashara kujulishwa kuwa kuna watu wameuawa kwa hiyo akaombwa aende Hospitali ya Wilaya Handeni akaagalie waliouawa na majeruhi.

Taarifa zilizomfikia alipofika Handeni jioni ile zilikuwa taarifa za kuogofya.

Hali pale hospitali ilikuwa ya kutia hofu palikuwa na ulinzi mkali hospitali nzima imezungukwa na maaskari. Kwa ajili hii Sheikh Waziri hakuweza kwenda hospitali siku hiyo na hata siku ya pili yaani Jumamosi hakuweza kwenda.

Waislam walibakia majumbani kwao wakisubiri na kuomba dua.

Sheikh Waziri akiwa kiongozi alipiga marufuku shura ya aina yoyote msikitini kuhusu mauaji yale kutafuta salama.

Waislam walikuwa wanakuja kuswali na wakimaliza wanaondoka kurudi majumbani kwao.

Lakini Sheikh Waziri akawa na wasiwasi kuwa ikiwa hatafanya jambo kuna hatari ya wale marehemu kutozikwa Kiislam.

Sheikh Waziri ilipofika Jumapili ikamjia fikra ya kumpigia diwani Mushashi. Alimweleza diwani huyu kuwa Waislam wangeshukuru kama serikali wangeruhusu maiti zile wapewe ili wazizike.

Haukupita muda diwani akamfahamisha Sheikh Zuberi kuwa anaweza kwenda hospitali na kuonana na Mganga Mkuu kwa ajili ya kupewa zile maiti mbili.

Lakini Mganga Mkuu akasema kuwa amri aliyopewa na Mkuu wa Mkoa Bi. Chiku Galawa ni kuwa maiti zile zipelekwe Tanga kwa mazishi ikiwa ndugu zao hawajajitokeza na huko maiti hizo zitachangwanywa na maiti nyingine za wasio na ndugu na zitazikwa na serikali.

Ikawa sasa lazima Mkuu wa Mkoa asubiriwe ili abatilishe amri yake ya awali na endapo ruksa itatoka Waislam wa Handeni watazizika maiti hizo.

Sheikh Hamisi akaondoka kusubiri amri ya Mkuu wa Mkoa.

Mwishowe maiti ilitolewa kwa Sheikh Waziri baada ya mazungumzo marefu kati ya Mganga Mkuu na Sheikh Waziri ikizingatiwa kuwa kwa siku tatu hakuna ndugu wa marehemu aliyejitokeza kuchukua maiti.

Sheikh Waziri alifunuliwa maiti ya Hamisi Ramadhani na Mganga Mkuu mbele ya askari.akaonyeshwa jeraha la mguuni alipopigwa risasi.

Shuka haikufunuliwa kuoneshwa majeraha mengine...
Sheikh Waziri hakuwa na haja ya kutaka mengi lililomshughulisha ilikuwa ni kupata maiti ili waisiitiri.

Sheikh Waziri anasema ilikuwa wazi kuwa Polisi na Mganga Mkuu walikuwa wameshakubaliana nini cha kufanya wakati watakapoonyesha maiti kwa ndugu zao.

Mganga Mkuu alionyesha jeraha la risasi mguuni akisema kuwa hapo ndipo zilipotoka damu nyingi kusababisha kifo cha Hamisi Ramadhani.

Lakini wao walikuwa na habari kamili kutoka kwa mke wa marehemu na jamaa wengine kuwa ndugu yao alikuwa amepigwa risasi katika kibofu cha mkojo na kwa hakika sehemu ile ingawa ilikuwa imefunikwa na shuka palikuwa na uvimbe mkubwa.

Sheikh Waziri na Waislam wachache walimzika ndugu yao usiku katika makaburi hapo hospitalini.
Sheikh Mohamed......

Kama Kweli Abu zuberi haijulikni kuwa alizikwa VIP kwa hofu kuwa endapo wangejitokeza ndugh zao Basi wangekamatwa unataka kutuaminisha kuwa police walishindwa VIP kuwafikia ndugu wa marejhemu na ksha kuwa kamata ?
Ni wasi kuwa askra hawashindwi kukamta mtu yoyote wakimuhitaji SAS Hapa unamdanaganya Nani kwa faida gani
 
99% ya mabandiko yako ni Uislam na waislame wake
It's okey sio Jambo baya, Ila uwasilishaji wa matukio ni uenezaji wa chuki

Kama muandishi na mtafiti umejaribu kufikiria unachokipanda mioyoni mwa waisalm wenzako?
Kama lengo lako ni Hilo 99% unafanikiwa[emoji120]

Peni yako inawaandika waislam tu, Mkuu umekua mdini Sana kuliko uhalisia,

Udini unafanya uonekane mpuuzi
Hahahah
 
…habari nilizowahi kusikia kuhusu kijiji cha ‘madina’ zinatisha! Hata kwenye hii taarifa haijasemwa kua kuna mtoza ushuru alieuwawa na pia polisi kutoka handeni kabla ya ffu kutoka tanga ambao ndio walioweza kudhibiti hali… pengine ni UMBEA TU
Gkileo,
Yaliyotokea Madina miaka 10 iliyopita yaliwashtua watu wengi sana.

Vyombo vyote vya habari ndani na nje ya nchi viliogopa kuandika yaliyotokea Madina.

Baadhi ya vyombo kama DW ambao ni wepesi sana kwangu kunihoji nilipowaeleza yaliyotokea walisema ni habari kubwa lakini si ya kutangazwa.

Mimi nilifika hadi Handeni kufanya uchunguzi.

Yapo mengi nitaeleza kadri mjadala unavyoenfelea.

Nina picha na sauti za wahusika.
 
Sheikh Mohamed......

Kama Kweli Abu zuberi haijulikni kuwa alizikwa VIP kwa hofu kuwa endapo wangejitokeza ndugh zao Basi wangekamatwa unataka kutuaminisha kuwa police walishindwa VIP kuwafikia ndugu wa marejhemu na ksha kuwa kamata ?
Ni wasi kuwa askra hawashindwi kukamta mtu yoyote wakimuhitaji SAS Hapa unamdanaganya Nani kwa faida gani
Dr.
Huu ndiyo uzuri wa janga linapokuwa limepita.

Muda unatupa nafasi ya kusema bila hofu na kutafuta makosa.

Mimi siko hapa kubishana na yoyote.
Wewe hukuwa unayajua haya wala huwajui ndugu zake Abu Zuberi.

Ikiwa unaona mimi nadanganya si kitu.

Vita subra bado yapo mengi nitaeleza In Shaa Allah.
 
SAKATA LA KUPOTEA RAJAB OMARI MTANA KIJIJI CHA LULAGO HANDENI 2013

Waislam 10 wamehukumiwa kunyongwa kwa tuhuma za kuua mlinzi mmoja.

Kufikia hukumu hii kuna mengi na chanzo chake kilianzia katika biashara ya hiliki na malipo ya ushuru kijijini Lulago.

Ninaanza leo kueleza kisa hiki kama nilivyotafiti na kuweka kumbukumbu miaka 10 iliyopita.

Rajab Omar Mtana alikuwa mwanakijiji wa kawaida tu akiishi kijijini Lulago, Handeni kama wanavijiji wengine wanavyoishi na alikuwa na biashara yake ya kuuza hiliki kama mkulima wa zao hilo.

Siku moja akaja mnunuzi mfanyabiashara wa hiliki nyumbani kwake kununua hiliki na akamuuzia.

Yule mfanyabiashara alipokuwa anatoka na gari yake akasimama kwenye kizuizi cha kulipia ushuru.

Alipotakiwa kulipa ushuru akasema kuwa si hiliki yote amenunua katika kijiji hicho kwa hiyo hawezi kulipa ushuru wa hiliki yote.

Hapo palitokea ubishi na mfanyabiashara yule akagonga lile geti na akaondoka.

Hii ikapelekea kwa wakusanya ushuru wa hapo kijijini kwenda nyumbani kwa Rajab Omar Mtana kumkamata na kumweka chini ya ulinzi katika ofisi ya serikali ya kijiji hadi hapo atakapolipa ushuru ambao yule mfanyabiashara alitakiwa alipe.

Ndugu zake Rajab Omar Mtana wakaenda pale ofisini kwa nia ya kumtoa ndugu yao na hapo pakatokea vurugu na mapigano.

Katika mapigano hayo, mgambo ambae ndiye aliyekuwa akishughulika na kudai ushuru akauawa.

Kisa hiki cha ushuru wa hiliki ndicho kilichozua balaa kubwa la mauaji na uchomwaji moto nyumba za Waislam wa kijiji cha jirani cha Madina na kuvunjwa kwa misikiti katika vijiji ambavyo vilikuwa na idadi kubwa ya wakazi wake Waislam.

Baada ya haya Mkuu wa Mkoa wa Tanga Chiku Galawa akatoa amri kuwa hapana ruhusa tena ya sehemu hizo kuwa makazi kwa kuwa hizo ni kambi za ugaidi.

Mkuu wa Mkoa alisema mengi ambayo takriban yote yamedhihirika baadae kuwa hayakuwa na ukweli.

Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wapo Al Shabab vijijini, kumechimbwa mahandaki ya vita katika vijiji na kuna silaha za kutungulia ndege nk. nk.

Mkuu wa Mkoa alizungumza na Radio Nuur, Tanga inayomilokiwa na Msikiti wa Ibadh.
Nilifunga safari hadi Radio Nuur Tanga kwa nia ya kupata taarifa kamili yalivyorushwa.

Radio Nuur waliogopa kunipa juu wala kuniruhusu kusikiliza kipindi hicho cha Mkuu wa Mkoa ingawa kabla sijahama Tanga nilikuwa mmoja wa Wakurugenzu wa radio hiyo.

Lakini niliwahoji watu waliosikia kipindi hicho.

Katika Waislam waliokamatwa na kufunguliwa mashtaka mahakamani Handeni ni huyu kijana Rajab Omari Mtana.

Baada ya kukaa rumande alipata dhamana yeye pamoja na wenzake na akawa nje.
Rajab Omar Mtana alirejea kijijini kwake.

Wakati anakaribia kuingia kijijini alisimamishwa na askari wa kijiji akapekuliwa na akanyang'anywa simu yake na fedha taslimu.

Baada ya mkasa huu walimwachia na yeye akaendelea na safari yake.

Lakini wakati akiwa rumande nyumba yake ilikuwa imevurugwa haifai kuishi mtu kwa hiyo alifikia kwa dada yake.

Akiwa nyumbani kwa dada yake alifatwa na watu wa serikali ya kijiji usiku akatolewa ndani na kuanza kupigwa kwa bakora na kisha kwa mapanga.

Kujitetea kijana huyu alikimbia huku akikimbizwa.
Asubuhi kulipokucha palionekana damu nyingi sana.

Taarifa ilitolewa polisi lakini hakuna kilichofanyika.
Polisi walitoa taarifa (SON/RB346/2014).

Dada yake na mumewe walikamatwa na kushitakiwa katika mahakama ya hapo kijijini na wakapigwa faini ya kila mtu shs. 20.000.

Kosa lao ni kumleta kijiji Rajab Omari Mtana mtu asiyetakiwa.

Miaka 10 imetimia Rajab Omar Mtana hajulikani alipo na inasadikiwa ameuawa na wale waliokuja kumtoa nyumbani kwa dada yake.

Rajab Omar Mtana ametafutwa kote hajapatikana na waliompiga na kumjeruhi wako huru nje hawajaguswa wala kuhojiwa na polisi.

Lakini wale waliotumiwa kwa mauaji ya mlinzi wa kijiji wamehukumiwa kifo.

Hapa kuna mengi sana ya kufikirisha mbali ya yale kuwa kulikuwapo na silaha za kutungua ndege katika vijiji hivi vya Waislam wa Handeni vilivyokuwa na nyumba za nyasi na udongo.

View attachment 2668468
samahani lakini ni kwa nini suala hili umelipa suala la udini sana as if kulikuwa vita ya kati ya waislamu na wasiyo waislamu hapo kijijini? ....ulichofanya si sahihi hata kidogo, wewe ni mchochezi, unless una ushahidi kuwa waliotenda unyama huo ni watu wa dini zingine.
 
samahani lakini ni kwa nini suala hili umelipa suala la udini sana as if kulikuwa vita ya kati ya waislamu na wasiyo waislamu hapo kijijini? ....ulichofanya si sahihi hata kidogo, wewe ni mchochezi, unless una ushahidi kuwa waliotenda unyama huo ni watu wa dini zingine.
Utingo,
Nakuomba uwe na subra.

Anza kuusoma huu uzi toka mwanzo uelewe mkasa wa Madina.

Baada ya hapo unaweza kuja na maswali.
 
Guest,
Hili jambo la matusi limekuwa sehemu ya majibu katika historia ya kalamu yangu.

Lakini hili halijawa jambo la kunizuia mimi kuandika yale ninayoyajua.

Nikitaka ningekuwa natoa taarifa kwa Adm kuwa kuna mtu ameleta matusi katika mjadala na Adm hapo hapo anampiga "ban," yaani anamfungia.

Mimi huwa sifanyi hivyo kwa kuwa namtaka huyu anaetukana abakie niwe na yeye na aendelee kunisoma hata kama atarejea kutoa matusi.

Hakuna amani inayohatarishwa kwa watu kupeana habari za kweli.

Niko hapa jamvini muda mrefu sana na nimepata umaarufu mkubwa na wasomaji wengi.

Sijasikia kama amani imevunjika kwa sababu ya makala zangu.

Kinachotokea ni kutembelewa na vyombo vingi vya habari vya ndani na nje kufanya mahojiano na mimi.
Ikikuoendeza tupe story ya waislamu wa kibiti walio dhibitiwa na magufuli for real
 
Dr.
Huu ndiyo uzuri wa janga linapokuwa limepita.

Muda unatupa nafasi ya kusema bila hofu na kutafuta makosa.

Mimi siko hapa kubishana na yoyote.
Wewe hukuwa unayajua haya wala huwajui ndugu zake Abu Zuberi.

Ikiwa unaona mimi nadanganya si kitu.

Vita subra bado yapo mengi nitaeleza In Shaa Allah.
Bas eleza MZee bill kuficha kitu na kamwe usiwausishe wakristo kwenye mjada huu
 
Back
Top Bottom