SAKATA LA LUGUMI: Tamko la Ofisi ya Bunge kuhusu mkataba wa LUGUMI

Na hivi vyombo vyetu vya habari navyo sijui vipi, mweee, hembu tuone kama vitajitetea...
 
Magu akiliweza hili atakuwa ameshinda, lakini hili jipu limekaa pabaya, kulikamua linahitaji mkamuaji ajipige kazi na mkamuliwaji apigwe kaputi
 
Bunge lenye meno kibogoyo tumemsikia Aishi siku tatu mfululizo akitolea maelezo mkataba upelekwe ha ha magufuli chali hawezi kutumbua jipu la katikati ya matako
Mkuu hili jipu la moto na limejaa ukakasi ata mkuu awezi thubutu kuligusa.
 
Mwenyekiti wa PAC Aishi anautaka huo mkataba kama nani..Mbona wabunge mishahara yao wanafanya siri..Mkataba ni wa siri
hivi we ni mtanzania kweli au ni interahamwe mijitu mingine sijui ikoje rais yuko bize kutumbua majipu mengine yanamshika mkono asitumbue
 
Si ni bora hii taarifa angeletwa na mwenye taarifa ya kwanza walau tungeelewa : NINANUKUU: TUMEWANDIKIA BARUA NA TUMEWAPA SIKU 3 WAWE WAMEWASILISHA MKATABA KWENYE KAMATI NA WAKISHINDWA KUFANYAIVO WATAKUWA WAMEDHALAU KAMATI NA BUNGE KWA UJUMLA
 
Kama wahusika watamruhusu kuona hakuna shida lakini wanaweza kumzuia na asifanye lolote...
kwanini nyie mafisiem mmefanya mbinu na kutia fitia kwenye ishu lugumi. hapa kuna ufisadi mkubwa kwani ni nini kinafichwa humo ndani.
 
Siamin kama hii taarifa imetolewa na Bunge, maana sijui ni kwa vip hiyo kamati itayapitia hayo maelezo ya utekelezaji bila kuuona huo mkataba unasemaje ..!!

Kamati ipo sahihi sana kuuomba huo mkataba ili ione kifungu kwa kifungu vya makubaliano yao, then ndo iombe maelezo ya utekelezaji..!!

Nadhan ni vema kusema waz kuwa hili jipu limekaa pabaya hamuwezi kulikamua, kuliko kumzungusha mgonjwa (mwananchi)
 
SHIKAMOO Lugumi Enterprises, ndani ya siku tatu, umeshaitepetesha mihimili yote ya serikali! Endelea kula keki mkuu!
 
PAC wanajipa madaraka ambayo sio yao...hawana mamlaka ya kukagua mikataba bila idhini ya wahusika

Kwa bahati mbaya sana watu wote tulimsikia Aeshi Hilaly alichokuwa anataka kwenye huo mkataba wa Lugumi, hivyo huo ufafanuzi wa bunge labda mkawape wanavijijji ndio bado wamelala. Enzi za kuliamini bunge limepitwa na wakati hasa wanapotoa ufafanuzi wa kupotosha kwa jambo lililo wazi kama hili. Hivi mnadhani hizi ni zile enzi tulikuwa tunaenda kuangalia sinema za vita vya urusi halafu tusubiri Nyerere aseme ameota kwamba Israel itapigana vita? Wananchi wamestuka/wameamka lakini viongozi bado wamelala huku wakitegemea dola kulinda uozo wao. Kwa mwendo huu huwa ndio nacheka kweli nikisikia nchi yetu inajiandaa kuwa ya viwanda.
 
Unawezaje kuomba maelezo ya mkataba, bila mkataba wenyewe?

Au kwa mfano rahisi,
unawezaje kuomba harufu ya chakula badala ya chakula chenyewe?

Hii taarifa kwa Umma imeandikwa kwa Ku panic.
 
Nimeamini na ninaanza kuamini JPM majipu yanaweza kumshinda kutumbua. Kumbe vipele ndo vinatumbuliwa
 

Kwanza nikupongeze kwa kujitahidi kujibu kwa busara japo najua kwa hili sakata limekushuka. Halafu kwa mambo ya kitoto hivi ndio eti watu wanaaminisha wananchi kwamba nchi hii haitegemei misaada na itakuwa nchi ya viwanda!! Kweli unaweza kusimama mbele ya hadhara ukahubiri nchi kuwa ya viwanda huku ukipindisha ukweli wa wazi kiasi hiki!!? Yaani hata ile imani haba niliyoanza kuipata kwa hili debe mlilokuwa mkiipigia serekali hii ya Magufuli imefutika rasmi kwa tangazo la utumbo kama huo. Ila si mbaya endeleeni kudanganya wananchi kwamba mnapambana na ufisadi huku mkiwachombeza na matumaini hewa ya viwanda huku kukiwa hakuna mpango wala dalili za dhahiri la hilo kutokea zaidi ya kupiga siasa.

CC: Humphrey Polepole, mzee mwanakijiji
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…