Sakata la Mechi ya YangaSc vs Simba, Kigogo Mmoja abwaga Manyanga bodi ya ligi kuu

Sakata la Mechi ya YangaSc vs Simba, Kigogo Mmoja abwaga Manyanga bodi ya ligi kuu

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
BREAKING: Mjumbe wa kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa ligi kuu Tanzania bara Ndugu Filimon Ntahilaja amejihudhuru nafasi yake muda mfupi uliopita na kutoka nje ya kikao baada ya maamuzi ya kutolewa ambapo yeye anaamini hayakuwa maamuzi sahihi.

Imefahamika kuwa Ndugu Filimon Ntahilaja hakuridhishwa na sababu Nyepesi za kuahirisha mechi hiyo na kuvunja kanuni kwa makusudi.

Ndugu Filimon Ntahilaja Rasmi sasa ameamua kujiondoa katika nafasi zake za kiuongozi kwenye mpira wa Tanzania.
 
Jambo dogo tu; kwa nini watanzania wengi wa siku hizi hawajui kiswahili? Mtanzania anayedai kiswahili ni lugha ya taifa anaandika "afisa amejiudhuru": kiswahili gani hicho?. Nimewahi kuuliza matumizi ya neno kuweza sijapata majibu hadi leo. Utasikia mtu anasema "mchezo huo ambao umeweza kuahirishwa" badala ya kusema kuwa "mchezo huo ambao umeahirishwa" Kiswahili cha ajabu kabisa. Hatujui kiingereza na sasa tushindwe hata kiswahili jamani.
 
Ni unafiki tu,

Derby ambayo Yanga aligomea mechi ilikuwa ni upuuzi wa hiyo kamati 100℅ kubadili muda bila sababu ya msingi kinyume na kanuni.

Je ulisikia mtu kuachia ngazi au kuwajibishwa?
 
utopolo ni laana ya taifa.mmesababisha mpaka mtu anaacha nafasi yake kwa ujinga wenu.
 
"Amejihudhuru", ni kiswahili gani hiki. Inaonekana hakuna lugha tunayoijua vixuri sisi watanzania.

Kuhusu huyo jamaa, sina maoni.
Vixuri ndo nini? Una mkosoa na na wewe unafanya makosa zaidi.
 
Vixuri ndo nini? Una mkosoa na na wewe unafanya makosa zaidi.
Angalia X na Z zilipo kwe keyboard, hilo ni kosa la ku-type, tofautisha na kosa la jamaa. Au unadhani ni wale wa kuandika xaxa?
 
Jambo dogo tu; kwa nini watanzania wengi wa siku hizi hawajui kiswahili? Mtanzania anayedai kiswahili ni lugha ya taifa anaandika "afisa amejiudhuru": kiswahili gani hicho?. Nimeahi kuuliza matumizi ya neno kuweza sijapata majibu hadi leo. Utasikia mtu anasema "mchezo huo ambo umeweza kuahirishwa" badla ya kusema kuwa "mchezo huo ambao umeahirishwa" Kiswahili cha ajabu kabisa. Hatujui kiingereza na sasa tushindwe hata kiswahili jamani.
Na wewe " Nimeahi" Ndiyo nini!!! Sema " Nimewahi"
 
Jambo dogo tu; kwa nini watanzania wengi wa siku hizi hawajui kiswahili? Mtanzania anayedai kiswahili ni lugha ya taifa anaandika "afisa amejiudhuru": kiswahili gani hicho?. Nimewahi kuuliza matumizi ya neno kuweza sijapata majibu hadi leo. Utasikia mtu anasema "mchezo huo ambao umeweza kuahirishwa" badala ya kusema kuwa "mchezo huo ambao umeahirishwa" Kiswahili cha ajabu kabisa. Hatujui kiingereza na sasa tushindwe hata kiswahili jamani.
Asante kwa constructive criticism 🙏
 
Lugha zote duniani ni ngumu. Hata Mchina, Mwarabu,Muingireza, Mpare, Msukuma, Mjapani n.k na mother tongue zao wanakosea sawa na sisi na Kiswahili chetu maana mazingira yanayosababisha ni hayo hayo.
Almuhimu ni kurekebishana kwa staha bila kuzodoana wala kulaumiana
 
Hata ningekua mimi ningejihudhuru. Wiki nzima ya maandalizi ushindwe kucheza mechi sababu ya kukosa saa moja ya kufanya mazoezi kwa mkapa, ni sababu ya kitoto sana
Kusema ukweli hii sababu imewakera wadau wengi wa michezo. Na nina imani hata shabiki wa simba mwenye akili timamu, hawezi kukubaliana na huu upuuzi.

Maana kwa taarifa zilizopo ni kwamba Yanga kwenye mechi iliyopita, haikuruhusiwa kuingia siku ya mwisho kufanya mazoezi kwenye huo uwanja! Lakini haikuja na hili wazo la kitoto la kugomea mechi!

Ila kwa simba limekuwa ni wazo sahihi, na Bodi ya ligi imebariki, pasipo kuangalia hasara na usumbufu kwa mashabiki na wadau wengine waliowekeza raslimali zao za kila aina kuelekea kwenye huu mchezo. This is not fair at all.

Yaani ni kwamba simba ni wageni wa uwanja wa Mkapa, kiasi cha kulazimisha kufanya mazoezi siku ya mwisho kabla ya mchezo! Na kwa nini hawakutoa taarifa mapema kwa wasimamizi wa uwanja, ili maandalizi yafanyike? Au walikuwa wanatafuta tu kisingizio cha kugoma?
 
Back
Top Bottom