Sakata la Mhadhiri wa Chuo Kikuu kupewa kesi ya ugaidi, Mgomo wa wafanyakazi UDOM wanukia

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Sakata la kisheria linalomkabili Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, limechukua sura mpya baada ya upande wa mashtaka kubadilisha mashtaka yake na kumfungulia rasmi kesi ya ugaidi. Hatua hiyo imezua taharuki na masikitiko makubwa miongoni mwa wanataaluma waliokuwa wakifanya naye kazi chuoni hapo.

1784896082919.png

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taaluma UDOM (UDOMASA), Dkt. Gerald Enos Shija, ameeleza kuwa hatua hiyo imeshusha sana morali ya wafanyakazi na kuwatia hofu. Ameonya kuwa kukamatwa kwa wanataaluma wanapotoa fikra tofauti kunatishia uhuru wa kitaaluma (academic freedom) na kunaweza kuua msingi mzima wa elimu nchini.

Kutokana na hali hiyo, UDOMASA imepanga kuchukua hatua za makusudi kufanya mazungumzo na mamlaka za serikali ili kunusuru uwezekano wa kutokea kwa mgomo gerezani na katika taasisi za elimu. Viongozi hao wanasisitiza haja ya kufikia muafaka wa kitaifa utakaohakikisha wanataaluma wanakuwa huru kufikiri na kutafuta majawabu ya matatizo ya nchi.

Soma Pia:

Nililitegemea hili..
Nchi inaenda kuingia sasa kwenye Migomo baridi katika taasisi nyingi za Umma.
Na Matokeo yake huduma zinakwenda kudorora na rushwa kutamalaki kila sehemu.
Watumishi wa Umma watakuwa wanauza huduma..hutaki acha.
Hii Hali iliwahi kutokea kipindi fulani cha Utawala wa Hayati Mzee Mwinyi.
Ilifika mahali mtumishi anakutamukia..-' Mwambie Rais wako aje akuhudumie-'

Serikali haina muunganiko tena.Pata picha tu mtu kama Wassira anasema 29/Oktoba..hapakuwa na jambo tu la kutisha sana ..ilikuwa kawaida tu..na yeye alipiga kura Bunda akaja kulala Mwanza hali ikiwa shwari kabisa....-'Lissu Kesi yake ni yeye anaichelewsha kwa kuweka mapingamizi..'
Sasa huyo ndiye miongoni mwa washauri wa Raisi!!!!!??
Haya..'Watanzania piganieni Katiba mpya..' huyo ni Makamu wa Rais mwenye jukumu la kuiwezesha hiyo Katiba mpya ipatikane...?!!!!?
 
Hakuna aliye salama, ni suala la muda tu. Hii nchi haina kiongozi hata mmoja mwenye AKILI akatoka nje akakemea huu ujinga? Yaani serikali nzima ya CCM ni wapumbavu kiasi hiki? Mnawezaje kucheza na UGAIDI?
 
Nililitegemea hili..
Nchi inaenda kuingia sasa kwenye Migomo baridi katika taasisi nyingi za Umma.
Na Matokeo yake huduma zinakwenda kudorora na rushwa kutamalaki kila sehemu.
Watumishi wa Umma watakuwa wanauza huduma..hutaki acha.
Hii Hali iliwahi kutokea kipindi fulani cha Utawala wa Hayati Mzee Mwinyi.
Ilifika mahali mtumishi anakutamukia..-' Mwambie Rais wako aje akuhudumie-'

Serikali haina muunganiko tena.Pata picha tu mtu kama Wassira anasema 29/Oktoba..hapakuwa na jambo tu la kutisha sana ..ilikuwa kawaida tu..na yeye alipiga kura Bunda akaja kulala Mwanza hali ikiwa shwari kabisa....-'Lissu Kesi yake ni yeye anaichelewsha kwa kuweka mapingamizi..'
Sasa huyo ndiye miongoni mwa washauri wa Raisi!!!!!??
Haya..'Watanzania piganieni Katiba mpya..' huyo ni Makamu wa Rais mwenye jukumu la kuiwezesha hiyo Katiba mpya ipatikane...?!!!!?
Mgomo baridi umeshaanza, kinachofanyika ni kuendelea kuukoleza
 
Sakata la kisheria linalomkabili Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, limechukua sura mpya baada ya upande wa mashtaka kubadilisha mashtaka yake na kumfungulia rasmi kesi ya ugaidi. Hatua hiyo imezua taharuki na masikitiko makubwa miongoni mwa wanataaluma waliokuwa wakifanya naye kazi chuoni hapo.

Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taaluma UDOM (UDOMASA), Dkt. Gerald Enos Shija, ameeleza kuwa hatua hiyo imeshusha sana morali ya wafanyakazi na kuwatia hofu. Ameonya kuwa kukamatwa kwa wanataaluma wanapotoa fikra tofauti kunatishia uhuru wa kitaaluma (academic freedom) na kunaweza kuua msingi mzima wa elimu nchini.

Kutokana na hali hiyo, UDOMASA imepanga kuchukua hatua za makusudi kufanya mazungumzo na mamlaka za serikali ili kunusuru uwezekano wa kutokea kwa mgomo gerezani na katika taasisi za elimu. Viongozi hao wanasisitiza haja ya kufikia muafaka wa kitaifa utakaohakikisha wanataaluma wanakuwa huru kufikiri na kutafuta majawabu ya matatizo ya nchi.

Soma Pia:
Safi kabisa nilishauri humu ndani kuwa njia pekee ya kumnusuru ni kugoma hamna suluhu nyingine.si mmesikia na ya kule kwanza?serikali sasa inadili na wanyonge baada ya kushindwa kufikia na mafisadi.
 
Back
Top Bottom