Sakata la kisheria linalomkabili Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM), Melkisedeki Kaijage, limechukua sura mpya baada ya upande wa mashtaka kubadilisha mashtaka yake na kumfungulia rasmi kesi ya ugaidi. Hatua hiyo imezua taharuki na masikitiko makubwa miongoni mwa wanataaluma waliokuwa wakifanya naye kazi chuoni hapo.
Akizungumzia suala hilo, Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Taaluma UDOM (UDOMASA), Dkt. Gerald Enos Shija, ameeleza kuwa hatua hiyo imeshusha sana morali ya wafanyakazi na kuwatia hofu. Ameonya kuwa kukamatwa kwa wanataaluma wanapotoa fikra tofauti kunatishia uhuru wa kitaaluma (academic freedom) na kunaweza kuua msingi mzima wa elimu nchini.
Kutokana na hali hiyo, UDOMASA imepanga kuchukua hatua za makusudi kufanya mazungumzo na mamlaka za serikali ili kunusuru uwezekano wa kutokea kwa mgomo gerezani na katika taasisi za elimu. Viongozi hao wanasisitiza haja ya kufikia muafaka wa kitaifa utakaohakikisha wanataaluma wanakuwa huru kufikiri na kutafuta majawabu ya matatizo ya nchi.
Soma Pia:
View attachment 3636173