Sakata la Mpina na Waziri Bashe, nilivyoelewa kwa Lugha Rahisi

M
Mpina ni mtoto wa mjini ni mzalendo alijua kabisa ushahidi huu angeupeleka kwa spika ungeishia kuwekwa kwenye makabati tu sasa yy kalisanua wenye akili tu ndo watamuelewa mpina.
 
Jikite kwenye mada kuu ya mleta uzi
 
Hivi wananchi kweli tunashindwa kuwaadhibu hawa watu mwakani kweli?
Wanaiba mchana kweupe, wanaingiza kura haramu mbele ya vyombo vya dola. Askari anakimbia na sanduku la kura mchana kabisa. Msimamizi anatangaza matokeo yake aliyokuja nayo, matokeo ya baadhi ya majimbo huwa yanazidi hadi idadi ya waliojiandikisha. Sijui wananchi watatumia mbinu gani nyingine, lakini 2025 lazima waendelee kushikilia dola na hawajawahi kuwa na nia ya kuibadilisha nchi hii kimaendeleo.
 
Kwahiyo kosa nii kwenda. Kwenye media. Je wakilisho lake liko sahihi?
Ukimsikiliza vizuri Spika point yake ni kwanini aende kwenye media wakati spika ndio ameitisha huo ushahidi, sasa kanuni za bunge zinamfunga mpina hata kama anaweza kuwa na Ushahidi sahihi dhidi Ya Bashe
 
Hawalazimishi bali Kanuni ndio zinambana Mpina, ni sawa wewe uwe mgombea halafu ujitangazie matokea ya Kura Mapema Kabla ya Tume,, Mpina Hakupaswa kuja kwa Media angetulia kwanza
 
Unajua waandishi wetu wengi sana ni Bogus
Hapa ingekuwa wenzetu hiyo Stationary na kampuni ya simu tayari ingejukina na kuwekwa wazi hata kama ni ya Waziri, Rais au yeyote

Kama kuna freedom of information basi wayaweke bayana
 
h
Ukimsikiliza vizuri Spika point yake ni kwanini aende kwenye media wakati spika ndio ameitisha huo ushahidi, sasa kanuni za bunge zinamfunga mpina hata kama anaweza kuwa na Ushahidi sahihi dhidi Ya Bashe
hata sheria za makaburu zilikuwa sahihi wakati ule ila zilikuwa batili!!Hii ni sawa na kusema mwanachama wa chama cha siasa akiwa na mgogoro na uongozi wa chama hapaswi kwenda mahakamani akienda ndo amejifuta uanachama!!

Sheria m za namna hyo hatuzitaki.Sisi ndio umma na tunahaki ya kujua sio tu vitu vidogo kama hivi hata mikataba anayosaini mama we have to know basi angalau hata kupitia bunge!
 
Spika anamshambulia muwasilishaji ili iwe ngao ya kupotezea kilichowasilishwa,
 
Ameenda kwa media kwa sababu anajua kutakuwa na twists na turns nyingi na mwisho wananchi(ambao ndio wamemuweka mjengoni) hawatajua ukweli.
 
Kuhusu hili suala la sukari ni jambo kubwa sana ambalo kimsingi Ni suala nyeti ambalo limaonyesha kiwango cha ufisadi kilivyo kithiri nchini
Na ambavyo hutaweza kuamini waziri ukimskiliza ni kama alikua na uchungu kweli na kwamba ana nia ya dhati ya kuwasaidia wananchi ndio mana akatoa vibali kwa watu nje ya wale walio kwenye takwa la sheria kumbe wapi ndugu ni kuwahadaa chenga ya mwili tu
 
Ni ujinga wetu tu wananchi tukiamua kweli kweli haishindikani mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…