Sakata la Ndugai: Mashabiki wako mkao wa Kula

Sakata la Ndugai: Mashabiki wako mkao wa Kula

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Siasa si ushabiki, wala vita vya kisiasa si lelemama.

Haipo shaka aina za kina Lissu, Mbowe na wa namna hiyo ni machampioni kweli kweli.

Si haba pia kwa kina Polepole, Kinana, Makamba au kina Membe kwa wakati wao. Kwa hakika nao walijaribu.

Wa kuzingatiwa katika vita huwa ni maadui na washirika, si mashabiki.

Kwamba pia kina Mwingira, Mzee wa Upako, Askofu Shoo au Polepole, hata kwa matamko ya mshikamano tu ilikuwa kama vile?

Kwa hakika tungali na safari ndefu.

"Nani ni maadui wa Mh. Ndugai?Hao wanaonekana labda hata kujulikana ni kwa nini."

Wako wapi washirika wake?

"Ina maana makelele yote tunayoyasikia ni ya mashabiki tu?"

Ikumbukwe mashabiki kama walivyo wapenzi watazamaji wao wako kiburudani zaidi.

Kwamba tuko mkao wa kula.

Inawezekana namna gani?!
________
Angalizo: "You are either with us or ..." -- George Bush.
 
Ndugai ameacha jambo lake kila mwenye akili timamu lazima ajiulize kulikoni, kuomba kwake msamaha hakuondoi jambo hilo vichwani mwa watu.

Kujisahaulisha au kulipuuza ni dalili ya uoga, upeo mdogo, au kutojua unachoshabikia/kufanya, kama alieanzisha hoja ni Ndugai lazima atajwe popote itakapohusika hoja hiyo bila kujali msamaha wake au vyovyote.
 
-Sufuria - Nchi
-Mafiga matatu - Mihimili mitatu

Mihimili miwili haina, Nchi ili iwe imara inagemea mihimili yote, pia Hii mihimili inashindwa kujitegemea (Separation of power) hadi inaegemea muhimili mwengine

Tukutane matesoni [emoji16]

Tengemea haya kila wakati.
IMG_20220106_080234.jpg
 
Ndugai kinachomponza haeleweki yupo kundi gani:
• Sukuma Gang hayupo
• Msoga Gang hayupo
• Makunduchi Gang hayupo
• Kwa wananchi nako hayupo

Yaani hayupo kokote na yupo kote, ndiyo maana hana mtetezi.
 
Ndugai kinachomponza haeleweki yupo kundi gani:
• Sukuma Gang hayupo
• Msoga Gang hayupo
• Makunduchi Gang hayupo
• Kwa wananchi nako hayupo

Yaani hayupo kokote na yupo kote, ndiyo maana hana mtetezi.

Muhimu ni hoja mkuu. Kinachoungwa mkono ni hoja. Sukuma, Msoga au Makunduchi kwani ni matambiko?
 
Tunaongelea hoja au utetezi?

Vyote. Hoja ya mikopo Ndugai hayo ni maoni kama binadamu na kama mbunge.

Utetezi kajaribu kufunika kumbe labda baada ya kugundua kumbe naye kesi za ugaidi zinaweza kumhusu.

Kwa vile sasa hakuna pa kwenda moto faya si ndipo wananchi tuliko?

Kumbuka watatu wale ni kimatambiko zaidi.

Au nasema uongo ndugu yangu?
 
Hii inatudhihirishia umuhimu wa kuwa na katiba mpya na inaonyesha jinsi mihimili mingine ilivyo subordinate kwa mhimili mmoja.

Kitendo cha Ndugai kumpigia rais magoti eti kuomba radhi ni dalili tosha kwamba hii mihimili mingine miwili ni boya tu na haina tofauti na idara zingine za serikali.

Ingekuwa katika nchi zingine za kidemokrasia Ndugai angekomaa na msimamo wake na kuamini alichokisema lakini kwa mazingira ya Tanzania ambapo rais ndiye huamua nani awe wapi na kwa wakati gani ndio matokeo yake hayo ya akina Ndugai kuonyesha jinsi walivyo walamba viatu vya rais. Bure kabisa.
 
Sijaelewa vizuri. Nazani kuna viunganishi vya mawazo hujaviandika.
 
Vyote. Hoja ya mikopo Ndugai hayo ni maoni kama binadamu na kama mbunge.

Utetezi kajaribu kufunika kumbe labda baada ya kugundua kumbe naye kesi za ugaidi zinaweza kumhusu...
Kumtetea mtu siyo lazima awe sahihi.

Ni kama debate tu, unachagua upande wowote then unajenga hoja.

Samia hayupo sahihi lakini anatetewa, Ndugai yupo sahihi lakini hana watetezi.

Na hana watetezi kwa kuwa he belongs nowhere.
 
Hii ni vita mkuu wala si kwa Jaji Tiganga. Hapa si suala la kuteteana.

"Nani ni maadui wa Mh. Ndugai? Hao wanaonekana na labda hata kujulikana ni kwa nini."

Msingi wa hoja uko hapa:

Wako wapi washirika wake?

"Ina maana makelele yote tunayoyasikia ni ya mashabiki tu?"

Tuko wapi Chadema? Tuko wapi wanaharakati? Tuko wapi wananchi?

Hatuioni fursa ya katiba mpya hapa?

Kwamba wengine tungali tuko mkao wa kula?
 
-Sufuria - Nchi
-Mafiga matatu - Mihimili mitatu

Mihimili miwili haina, Nchi ili iwe imara inagemea mihimili yote, pia Hii mihimili inashindwa kujitegemea (Separation of power) hadi inaegemea muhimili mwengine

Tukutane matesoni [emoji16]

Tengemea haya kila wakati.View attachment 2070219

Kila mhimili kusimama kivyake vyake ni jambo la afya sana kwa wananchi.

Mashabiki ni mzigo kwenye kuifikia adhma hiyo, bali washirika.
 
Kazi ipo haswa

Maswali ya msingi:

"Viko wapi vyama vya siasa?Tuko wapi Chadema? Tuko wapi wanaharakati? Tuko wapi wananchi?

Hatuioni fursa ya katiba mpya hapa?"

Au nasi ni mkao wa kula tu?
 
Hii ni vita mkuu wala si kwa Jaji Tiganga. Hapa si suala la kuteteana.

"Nani ni maadui wa Mh. Ndugai? Hao wanaonekana na labda hata kujulikana ni kwa nini."

Msingi wa hoja uko hapa:

Wako wapi washirika wake?

"Ina maana makelele yote tunayoyasikia ni ya mashabiki tu?"

Tuko wapi Chadema? Tuko wapi wanaharakati? Tuko wapi wananchi?

Hatuioni fursa ya katiba mpya hapa?

Kwamba wengine tungali tuko mkao wa kula?
Hana washirika.
• Sukuma Gang siyo washirika wake
• Msoga Gang siyo washirika wake
• Makunduchi Gang siyo washirika wake pia
 
Back
Top Bottom