Sakata la Panda Hill: Mkuu wa Mkoa na RPC Mbeya mnapaswa kuachia nafasi zenu haraka

Sakata la Panda Hill: Mkuu wa Mkoa na RPC Mbeya mnapaswa kuachia nafasi zenu haraka

Nchi ya maelekezo kila mahali, kuna siku mtaleta maafa makubwa sana nchi hii.

Ndugu Watanzania, tukiwa katikati ya sakata la DPW, lilibuka sakata la mwanafunzi wa Panda hill school kupotea, kwa jina Ester.

Sakata hili lilivuta hisia za wengi kiasi cha waziri mkuu kutoa tamko kuwa anawaagiza polisi wantafute kwa haraka ili apatikane.

Jambo hili lilizua gumzo kubwa na hisia kali katika jamii.

Katika kupotea kwake Ester, inasemekana aliacha ujumbe usemao " mjihadhari na mwl Jimmy"

Jamii ilijiuliza kwanini Jimmy?

Baada ya agizo la Waziri mkuu, mtoto alipatikana kwa haraka sana, ikadaiwa alikuwa kwa muuza mkaa kwa jina baba Jose akishirikiana na mama muuza genge, mara fundi cherehani...mkanganyiko.

Wote tulishuhudia Ester akihojiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa na alirudia kumtaja Jimmy kuwa ashughukiwe bila ya kufunguka zaidi.


Leo tena kwenye vyombo vya habari, nimeshtushwa mnoo kumsikiliza Ester akihojiwa na ameelezaza kuwa;

1. Mwl Jimmy aliingia bwenini akisaka wanafunzi waliochewa kutoka bwenini.
2. Alimkuta Ester ametoka kuoga na akiwa na kanga moja
3. Akampiga kuwa kwanini amechelewa kuwahi darasani
4. Akamsukumiza kitandani, akamziba mdomo na shuka na KUMWINGILIA KIMWILI

WAZAZI/WALEZI WA ESTER
1. Wamelalamika kuwa mtoto alipopatikana mazingira yalitia shaka
2. Pamoja na mashaka viongozi waliwazuia kuongea tofauti na MAELEKEZO waliopewa
3. Sasa wanaomba haki itendeke kwani ukweli ulifichwa.

MASWALI YANGU KWA MKUU WA MKOA NA RPC
1. Kwanini mlificha ukweli wa jambo hili?
2. Kwanini mkuu wa mkoa alikuwa soft sana alipoiongelea shule ya Panda hill na zaidi akiwamwagia sifa?

3. Hii shule ya Panda hill ni ya kigogo gani serikalini?

HITIMISHO
Mazingira ya kupotea na kupatikana kwa Ester yalizua maswali mengi sana ( HUENDA HATA JINA BABA JOSE NI MAELEKEZO TU).

1. Alitorokaje shuleni wakati kuna geti na ukuta mrefu?

2. Kwanini alimtaja Jimmy?

3. Polisi na mkuu wa mkoa walishindwa nini kumwita Jimmy ahojiwe mbele ya mtoto majibu sahihi yapatikane?
4. Ni lini mtuhumiwa kama huyo hakuchukuliwa hatua za haraka bali waliamua kumfuata kwa muda wao?

4. Kwanini mkuu wa mkoa hakujitokeza tena kuliambia taifa undani wa sakata hilo badala yake Pandahill schooll ndio walipewa nafasi ya kutoa taarifa?

SAKATA HILI LINA VIASHIRIA VYA RUSHWA.

ANGALIZO:
Ninasikitika sana endapo Ester angekuwa ni binti yangu.
1. Jimmy angekuwa mlemavu au mfu kabisa.
2. Hayo maelekezo mliyowapa wazazi...ingekuwa mimi mngenifunga au kunizika, pasingetosha.

Katika maisha yangu kamwe huwezi kumdhalilisha mtoti na mwanamke mbele yangu nikavumilia...sasa awe binti yangu dunia yote ingeiona gharabu yangu.

Kwa mazingira haya Mkuu wa Mkoa na RPC mbeya:
1. Mmewakosea sana watoto wa kike kwa kutokumpa Ester haki yake.

2. Mmewakosea wazazi wote.

3. Mmelikosea na kulikosesha taifa la Tanzania.

ACHIENI NGAZI HARAKAView attachment 2675028
Mimi mtoto wa kike siwezi kumuamini hata kwa machozi ya damu, haswa hawa watoto wa siku hizi.
Mimi ni mzazi pia .

Mleta mada unafikia hitimisho gafla sana
 
Alikiri na alisema ni msamaria mwema kwake, na km maelezo ya mama wa genge ni tofauti, mbna yeye Esther haku kana??

Kwan huyo kupotea kwake kumechukua mda gani had kupatikana?
je uongozi wa shule haupo? ama ni shule ya kata nachoamini shule mpaka iwe mabweni sio ya kilelemama kwa hio break ya kwanza........ kuna walakini
 
Esther wa miaka 18,kidato cha 5 si mtoto!
In otherwords ni "mwalimu" wa form 1 to 4.
Hayo aliyoyaeleza akihojiwa ipo siku yatajiweka peupeee peeee!
Sina shaka na imani yangu;
Wanafunzi ni waongo sana,
Wanafunzi si wa kuwaamini sana,
Wanafunzi ni wachomganishi mnoo!

Anaeleza haya baada ya mwezi mmoja na nusu! Kweli? Kweli? Kweli?
SIMWAMINI !
Je,mnamkumbuka Babu Seya?
 
Binti wa kidato Cha 5, mwenye akili timamu, anasoma masomo ya sayansi. Baada ya kubakwa na mwalimu Jimmy anaondoka kwenda kukaa kwa muuza mkaa Baba Jose badala ya kwenda kuripoti polisi au kurudi na kuripoti nyumbani.

Pelekeni mahakamani ili tijue mbivu na mbchi. Uongo na ukweli haupikiki chungu kimoja. Ma classmates wataitwa na tabia halisi ya Esther itawekwa hadharani
safii.. there chances ya kwamba Esther nae ni muhuni tu!
 
Mr Q
Haijalishi mtoto huyu alikuwa akiliwa na baba Jose au la.
Haihalalishi kubakwa na mwingine.

My concern ni ubakaji wa mwalimu na RC na RPC kuwapa wazazi maelekexo ya kuongea mbele ya midia.

Why waelekezawe?
Ulikuwepo wakati wanapewa maelekezo ya kile cha kuongea
 
Limalaya tu hilo litoto, ....,Baadala ya kwenda hospital /police kupima shahawa kama ushahidi, linaenda kwa baba jose Kuongezea shahawa zingine tena juu....,Afu eti form 5PCB.....,Nashauri shule imfukuze shule na imshtaki kwa kuichafua shule/Mwl Jimmy.
Yaan watu wanapoteza muda buree, ni kuliachaa tyuuh likaolewe kwa baba jose wake, amuache mwalimu wa watu, khaaah
 
Mwalimu Jimmy is guilty Hata Km hakubaka inaelekea ndio Tabia zake kunyanyasa watoto mpaka wanaona shule ni ngumu, atafutwe ahojiwe na wabobezi, asiendelee kufanya psychological damage kwa watoto wengine zaidi, ingependeza kama atasimamishwa kupisha uchunguzi juu yake
 
Hakuna hiki kitu, bas huyo mama wa Gengeni alokutwa na Esther ndo atoe maelezo kamiliii, mbna rahisii tyuuh.
Ndio maana unaambiwa kuwa huu mkanda una mashaka naona unakomaa kama vile ulimshikia baba Jose aweke😂
 
Hivi mtoto aliwezaje kutoka shuleni?
hapo sasa hio ni kicheche imeshindikana kama ameweza toka nje ya shule na mlinzi hajamwona si balaa jingine. Waongeze mafuta ya taa kwenye chakula nahisi waliacha alikuwa high sana huyo.
 
Back
Top Bottom