Uchaguzi 2020 Sakata la Sheikh Ponda na "masheikh rasmi"

Uchaguzi 2020 Sakata la Sheikh Ponda na "masheikh rasmi"

1) Mzee Said unataka kusema kwamba waislamu wakimchagua Lissu mgombea alienadiwa na Ponda ndio matatizo ya waislamu yataisha, au huyo mgombea atakuwa sababu ya waislamu kuingia peponi?

2) Kwa mwendo huu wa Ponda kuwaambia waisilamu wamchague Lissu akitokea kiongozi anaekubalika na wakristo wengi nae akasema wakristo wamchague JPM, huoni kwamba tunaelekea kuligawa taifa kidini?

Natanguliza shukran zangu kwako Mzee wetu Said wa jukwaa la history.
Labda Askofu Kakobe baada ya kunyoosha mikono juu. Ni next to impossible kiongozi wa Wakristo kufanya hivyo kwani wengi wapo wapo tu kwa hofu kubwa ya kupatwa na yale ya Kakobe.
 
MIE NAIoGOPA SANA AMANI ISIYO NA HAKI kwa mawazo yangu kwenye haki amani inakuwepo lakini kama haki hakuna kuna woga unyonge kukatatamaa ( labda hiyo ndio mnayoiita amani) au...........

Mzee,

Ingawa nina admire sana kipaji chako cha uandishi na hifadhi ya historia lakini kuna jambo moja baya sana linakuhusu.

Unapenda Tanzania iwe nchi ya Kiislam na unalazimisha historia itambue kwamba Watanganyika wote kabla ya Uhuru walikuwa hawana muamko wa kusaka uhuru zaidi ya kikundi cha masheikh wachache wa Mzizima na Bagamoyo ambao waliamua kumtunuku Mwalimu Nyerere ashike bendera ya kudai uhuru.

Katika hoja zako zote lazima uweke udini tena udini unaolenga kujenga chuki.

Unatumia uzee wako vibaya sana. Unapaswa kuheshimu sheria na taratibu za nchi. Kitendo cha kuunga mkono harakati za marehemu sheikh Ilunga ni sahihi sana kukuona hauna tofauti na wapiga ramli wanaoiombea nchi yetu iingie kwenye janga tena la machafuko.

Waache masheikh wamtumikie Mola wao, kama unachukia nenda kawshtaki kwa Mungu na siyo kuwadhalilisha.

Ponda anajulikana tangu awali kuwa anasaka umaarufu bila kujali athari zake.

Nakupinga sana kwenye hili
Mkuu, mimi mwenyewe ni CCM na kura yangu ni kwa Magufuli.
Lakini linapokuja swala la imani, chama changu (CCM) kwa miaka mingi imetukandamiza Waislam, kwa kutuundia chombo (Bakwata) kinacho tetea serkali kuliko Waislam.

Kwahiyo Ponda yuko sahihi kuwaamasisha Waislam waipigie chadema kwa kuamini kitawafuta machozi yao.

NB: Upande wangu, Wakrsto wamesha shika hatamu nchi hii, hivyo hata CDM wakishinda sidhani kama wataifuta Bakwata.

Tena ndio wenda hata Adhana watasema kelele.
 
Sasa Mzee wangu, ikitokea Wakatoliki au walutheri au wakristo wote kwa ujumla wakatangaza kura ni kwa flani(upande tofauti na aliochagua sheikh wako)kama alivyofanya Sheikh Ponda unadhani nini kitatokea baada ya matokeo!?
wanazo sababu za msingi kama za ponda? ishu hapa sio kuamka asubuhi na kutangaza hakuna atakae wafuata,ponda ana sababu na ndio maana wanajaribu kumtungua wanashindwa"hawajawahi kuwasaidia hao watu ponda anaowasemea"
 
SAKATA LA SHEIKH PONDA: MASIKINI "MASHEIKH RASMI" HAWAJUI KUWA HAWANA WAISLAM WANAOWAONGOZA, WAKO PEKE YAO

Awali ya yote mimi sitajiingiza katika propaganda za uchaguzi bali nitajaribu kueleza hali ya Waislam ilivyo.

Kwanza ni kuwa Waislam toka ilipovunjwa EAMWS na serikali mwaka wa 1968 na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir kukamatwa na kufukuzwa nchini na serikali kuwaundia Waislam BAKWATA, Waislam wameishi na kinyongo miaka yote sasa inafika nusu karne.

Ndiyo unasikia lugha za "sheikh wa BAKWATA," Waislam wakijiweka mbali na BAKWATA.

Na ukweli ni kuwa BAKWATA haijaweza kukubalika na sababu ni ndogo kuwa si taasisi iliyoundwa na Waislam wenyewe.

Matokeo yake ni kuwa katika hii jamii kubwa ya Kiislam Waislam wana viongozi wao wanaowakubali, kuwaamini, kuwapenda na kuwasikiliza wanachowaambia.

Sheikh Ponda ni mmoja wa masheikh hawa.

Sheikh Ponda amewaeleza Waislam nani adui ya Waislam wa Tanzania na akasimama kupambana na adui huyu huku akiungwa mkono na Waislam wengi sana.

Katika juhudi hizi Sheikh Ponda kakutwa na shida nyingi.

Kalipa kwa ajili ya Allah kwa machozi na damu.

Kwa damu yake na machozi ya nduguze Waislam.

Nimeweka hapa FB makala fupi ya maisha ya Sheikh Ponda katika kuwatumikia Waislam sasa mtafute sheikh yeyote wa BAKWATA ambae amepata kusimama na Waislam katika dhiki na shida zao.

Hakuna.

Katika hali kama hii ni tabu sana kujaribu kumchafua sheikh kwa propaganda hizi za uchaguzi kwa kuwa Waislam wanamjua Ponda ni nani.

Ponda anawakilisha sauti ya Waislam wengi, wengi, wengi sana.

Wako waliotambua hili na wamejua nini wafanye waweze kupata kura za Waislam.

Hawa ni watu wenye kufikiri na kukubali ukweli kuwa Waislam wanaishi na kinyongo dhidi ya utawala kwa miaka mingi.

Hawa wametumia fursa hii kwa kuhaidi kutoka haki na fursa sawa kwa wote.

Ndiyo maana hujasikia Waislam wamefanya maandamano kumpinga Sheikh Ponda.

Wanaompinga Sheikh Ponda si masheikh bali ni "masheikh wa BAKWATA."

Chunguza.
Mbona waislam hamujiamin had muunde vi taasisi ili kuwapa comfort, mbona sisikii kuusu balaza la wakiristo, mbona sisikii chochote kuhusu mabalaza ya dini zingine au u islam ni deficiency flan ktk mind ...mnateseka sana , na shida zote duniani nyinyi ndo chanzo kwann kila siku nyinyi tu? IS, ALSHABAB BOKO HARAMU ..ifike wakati mji mji tathmin basi ndugu zetu
 
Mkuu Rubawa ,
  1. litafute lile swali, lisikilize tena, kama akili yako inakuwa muulizaji swali ni mtu wa Tiss na hilo ni swali kutoka kwa Tiss kwenda kwa CinC, then I just feel sorry for you!. Mtu wa Tiss anaweza kupandisha humu bandiko kama hili hili. TISS Ikanushe tuhuma za uvamizi, utekaji, utesaji na mauaji!. Wasijadiliwe na Bunge kwa uwazi bali wachunguzwe, wakithibitika wafumuliwe!
  2. Kinachoendelea nchini kwa sasa, ni kusubiria siku na saa tukatimize wajibu wetu, ni kishindo kile kile cha 90% +, and I'm sorry for you, najua hautapiga kura kwasababu hukujiandikisha, ila wahimize ndugu zako, wasifanye majaribio kwenye urais, tumpe mitano tena, JPM.
P
Andrew Nyerere ameshajamba shuzi huko Facebook.
Screenshot_20201024-070641.jpg
 
2010 Sheikh Ponda kampigia kampeni Kikwete kwa waislamu na ni kigezo ni kwamba Kikwete muislamu mwenzao,sasa Ponda angekuwa anafanya harakati bila kuangalia nani yupo ikulu basi asingemsaidia JK wakati huo huku akijua kwa kufanya hivyo anakuwa anakuwa amesaidia madhalimu ccm.
Mazingira ya kisiasa ya wakati huo na Sasa ni tofauti kabisa.

Isitoshe kipindi hicho mambo ya Uamsho yalikuwa hayajashika kasi mpaka ilipofika mwaka 2012 ndio upepo ulibadilika.
 
Sasa Mzee wangu, ikitokea Wakatoliki au walutheri au wakristo wote kwa ujumla wakatangaza kura ni kwa flani(upande tofauti na aliochagua sheikh wako)kama alivyofanya Sheikh Ponda unadhani nini kitatokea baada ya matokeo!?

Waambie hao wakristo wamuunge mkono wamtakaye. Ila waisilamu wanapeleka kura zao kwa mtenda haki.
 
Sana, huyu Jamaa anaweza sana kuhamisha kwa maneno ya kujaza Jazba

Sijui imekuaje Mamlaka za Nchi zinamuacha anazunguka Kwny Ngome yake ya kusini Mikoa ya Mtwara na Lindi…kule Tandahimba hadi Tunduru ana wafuasi wengi sana sana …Tume iangalie kwny orodha ya wahamasishaji wa Lissu iliyowasilishwa Tume kama Ponda yupo, otherwise aamriwe arejee Dar mara moja

Sheikh wangu Ponda namkubali sana sana sana lakin nakosana nae kwny misimamo yake mikali dhidi ya Chama na Serikali
Simama na umma wa kiislamu, achana na genge la watu wa dhulma.

Fikiria kuna kesho akhera.
 
Mzee,

Ingawa nina admire sana kipaji chako cha uandishi na hifadhi ya historia lakini kuna jambo moja baya sana linakuhusu.

Unapenda Tanzania iwe nchi ya Kiislam na unalazimisha historia itambue kwamba Watanganyika wote kabla ya Uhuru walikuwa hawana muamko wa kusaka uhuru zaidi ya kikundi cha masheikh wachache wa Mzizima na Bagamoyo ambao waliamua kumtunuku Mwalimu Nyerere ashike bendera ya kudai uhuru.

Katika hoja zako zote lazima uweke udini tena udini unaolenga kujenga chuki.

Unatumia uzee wako vibaya sana. Unapaswa kuheshimu sheria na taratibu za nchi. Kitendo cha kuunga mkono harakati za marehemu sheikh Ilunga ni sahihi sana kukuona hauna tofauti na wapiga ramli wanaoiombea nchi yetu iingie kwenye janga tena la machafuko.

Waache masheikh wamtumikie Mola wao, kama unachukia nenda kawshtaki kwa Mungu na siyo kuwadhalilisha.

Ponda anajulikana tangu awali kuwa anasaka umaarufu bila kujali athari zake.

Nakupinga sana kwenye hili

Kwani uliwahi kumuunga mkono lini? Yeye hataki kuungwa mkono bali anaongea ukweli fullstop.
 
Mbona waislam hamujiamin had muunde vi taasisi ili kuwapa comfort, mbona sisikii kuusu balaza la wakiristo, mbona sisikii chochote kuhusu mabalaza ya dini zingine au u islam ni deficiency flan ktk mind ...mnateseka sana , na shida zote duniani nyinyi ndo chanzo kwann kila siku nyinyi tu? IS, ALSHABAB BOKO HARAMU ..ifike wakati mji mji tathmin basi ndugu zetu
Wewe huna akili, TEC na CCT ni mabaraza ya nini?
 
Wewe nawe ni wale wale, 'wavurugaji na wapenda mivutano'

Waislamu wamebadilika sana, siku hizi huwazolewi kirahisi

Wewe na Shehe Ponda mnapenda mivutano

Wakati nyinyi hampendi mivutano bali mnapenda makondoo.
 
Waambie hao wakristo wamuunge mkono wamtakaye. Ila waisilamu wanapeleka kura zao kwa mtenda haki.
Wakristo ni wanufaika mkubwa wa utawala huu wa kidhalimu wa ccm, lakini wakristo wengi huwa hawaitaki kabisa ccm na kiasili watu werevu huwa wanapigia kura upinzani.

Angalia mikoa yote yenye watu werevu ccm haitakiwi kabisa.
 
Back
Top Bottom