Mkuu Maalim Sheikh
Mohamed Said , poleni sana ndugu zetu Waislamu wa Tanzania, kwa madhila yaliyowakuta, tangu baada ya kuvunjwa kwa EAMWS na serikali mwaka wa 1968 na Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Ameir kukamatwa na kufukuzwa nchini na serikali kuwaundia Waislam BAKWATA, Waislam wameishi na kinyongo miaka yote sasa inafika nusu karne.
Kwenye hili la kunyoosha kidole upande fulani na kusema kuna adui wa Waislamu na adui wa Uislamu, naomba tuwe wakweli, na ukweli wa kwanza, naomba utuelimishe kidogo kumhusu Mufti wa kwanza wa Tanganyika na baadaye Tanzania, Sheikh Hassan bin Ameir,
- alikuwa ni mtu wa wapi?.
- Alikamatiwa wapi?
- Kwa kosa gani?
- Alikuzwa nchini na serikali, na kufukuziwa wapi?.
Tuanzie hapo ili tufike mahali tumjue adui halisi wa Waislamu ni nani, tusije kunyoosheana vidole, tukawashawishi ndugu zetu Waislamu, kupiga kura za chuki, kutokana na vinyongo bandia, kwa kudhani adui yao ni fulani kumbe sio kweli, huku kutakuwa ni kuwatendesha Waislamu wa Tanzania, dhambi ya ubaguzi, hao Waislamu wanaoishi kwa kinyongo dhidi ya utawala kwa miaka mingi, naomba pia waambiwe ukweli kuwa wasipeleke kura zao upande fulani kwasababu ya kinyongo cha miaka mingi, kwasababu hata huko watakapopelekehizo kura zao, zitapotea bure, hivyo sio tuu kuendelea kuishi na kinyongo, wataishi na kihoro!.
Dawa ya madhila, sio kuishi kwa kinyongo, bali ni kwa kukaa chini na watawala na kuyazungumza, tuyajenge, tuwe kitu kimoja!.
Na kwa vile kwa sasa mimi pia ni kada, naomba kuchukua fursa hii kuwaomba kura Waislamu wote wa Tanzania, kura ni JPM, na CCM, ndio pakee anaweza kumaliza madhila yote ya Waislamu, na hapa tulipo, nitamuomba Mwenyekiti wetu, kesho Jumatatu, awaachie huru wale Masheikh wote wa Uamsho wanaoshikiliwa, ili Jumanne waungane na familia zao, na Jumatano, Waislamu wote kwa sauti moja, wamshukuru kwa vitendo, aliyewaachia masheikh wa uamsho.
P
P