Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,843
- 31,057
Naweza kuliita hili sakata la tozo kama kaa la moto!
Wakati watawala wakijaribu kwa kila namna kutetea tozo hizo zilizoidhinishwa na waheshimiwa wabunge wetu, upande wa pili wa wananchi wanazipinga vikali tozo hizo na hata kudiriki kuziita kuwa ni "day robbery".
Wakati huo huo wale wafanyibiashara, kama vile kampuni za simu na mabenki, ambao "wamelazimishwa" na serikali yetu, kuzipokea tu hizo tozo, wakishuhudia kupungua sana kwa wateja kwenye makampuni yao, kutokana na huo "ujambazi" unaofanywa na Serikali yetu, dhidi ya wateja wao ambao ni wananchi.
Hebu tujiulize, hivi ni kwanini watawala wetu wanazivunja sheria zao wenyewe walijoziwekea za kutomtoza mwananchi wake tozo ya zaidi ya mara moja kutokana na chanzo kile kile?
Hebu watawala wetu naomba mtueleze, hivi ni kwanini mfanyakazi wa nchi hii anakatwa kodi mara 2 kutokana na mshahara wake kukatwa PAYE, na papo hapo mshahara wake ukiingia benki ukatwe tena tozo?!
Hivi sasa tunashuhudia watawala wetu wakijiumauma, huku wakiliona hilo jambo ni la moto kweli kweli! Hebu nijaribu kueleza chanzo kikuu cha tatizo hili, ni kutokuwa na wawakilishi wa wananchi, ambao ni wabunge, ambao ni chaguo la wananchi.
Hivi unaweza kuwa na wawakilishi wa wananchi, wanaoweza kupitisha sheria za ukandamizaji, kama walivyofanya hawa wabunge wetu, kuhusiana na haya masuala ya tozo? Kama kungekuwa na uchaguzi ulio huru na haki, basi hizi dhuluma zote tunazofanyiwa na watawala wetu zingekoma.
#Kataa tozo