Kuna vijana wanakuwa na utajiri wa shaka sana.Kuna utajiri kwa uchumi wetu na hali halisi lazima ujiulize.Ukiona kijana jumba alilojenga,investment anazomiliki,historia ya familia yake,elimu yake, unakosa connection kabisa.
Wapo vijana matajiri kwa namna ya kueleweka lakini hali ya sasa inatisha! Unakuta kijana mdogo lakini ana utajiri unaoshangaza!!
Anyway kila mtu na maisha yake lakini effects za haya tunayopuuzia ndio vinavyoharibu uchumi na kuleta impact kwa majority.Madhara ya madawa ya kulevya yanaeleweka lakini pia njia zingine za utajiri kama Ufisadi na ujambazi/Dhuluma zinaishia kuwaumiza maskini walio wengi (refer yule mjane aliyetaka kuporwa kiwanja chake na akina Papaa Msofe hadi Pinda akaingilia kati,I mean mtu kama Pinda kuingilia baada ya system nzima kushindwa kutenda haki).
Nyie viongozi wenye dhamana ya hii nchi hata kama hamjali kinachoendelea lakini adhabu ya kupuuzia kwenu mtaipata hapa hapa duniani maana wanaokuja kuumia ni wasio na hatia.