Sakata la Yusuph Kagoma kusaini timu mbili Klabu ya Simba kukatwa alama

Yaani mpira wa bongo kwenye usajili, mikataba kuna sakarakasi nyingi sana,ujinga huu wanaulea TFF.
 
Yanga wanaleta upumbavu wa propaganda za nje ya uwanja, mwaka huu ni ubaya ubwela na wamegundua hivyo wanatumia siasa za kijinga za nje ya uwanja.

Walishindwa kumnunua huyo Kagoma Simba wakaja na ofa nzuri zaidi wakapita nae na wao inawauma haswa ukizingatia ni mchezaji wa Singida timu ya Mwigulu Nchemba,

Yanga ndio wanaofanya watu wengi haswa vijana wa kisasa waichukie CCM kwa mambo ya kipumbavu kama haya. Kudhani kwamba wao ndio kila kitu kwenye nchi hii.
 
Ni siasa nyepesi za propaganda, ni mambo ya kawaida kwenye mpira wa bongo. Kama Mwigulu aliwaambia Yanga wamsamehe hizi kelele zinatoka wapi?.
 
Mpira wa miguu unaendeshwa kwa kanuni na taratibu zake sasa kuna mashabiki humu hawajui kuhusu mpira wao wanajua mihemko isiyokua na sababu mpira sio mapenzi et nilikukataa na kuanzisha mahusiano na mwingine pindi anasaini klabu mbili tofauti hakujua kama ni kosa?
Kama kuna shida kamati ya sheria na hadhi ya wachezaji wataamua kwa kufuata sheria sio kwa maneno ya mashabiki maandazi et haitaki Yanga wakati alisaini mkataba na Yanga..
 
mashabiki maandazi et haitaki Yanga wakati alisaini mkataba na Yanga..
Anayesimamia hizo sheria ni nani? Jee Kangoma alicheza bila ya kuwa na leseni. Na kama alikuwa na leseni nani aliitoa hiyo leseni kama si TFF na Bodi ya Ligi?

Zaidi ya yote FIFA ilishaagiza mambo ya pointi za mezani ni MARUFUKU na ndiyo maana watu wa FA wanahimizwa kuhakikisha kuwa mambo ya usajili yapo sawa kabla ya kutoa leseni.
 
Mwaka huu ni ubaya ubwela tu hakuna namna .Na bado , mwaka huu kila tundu lililopo kwenye mwili wa Amfibia lazima litowe milio kama si pwiii basi ni fwii!
 
Hahahaaa mpwaaaaaa tushaanza kuagizaaa brian viongozi wajingaaa walee wacha wafundishwe sheria
Yanga hii inayobwagwa kila siku huko FIFA ndiyo iwe na viongozi wanaojua sheria za mpira kuliko viongozi wa simba?

Hizo ni propoganda za kizamani sana za kutaka kuwatoa tu simba kwenye reli . Lakini mwaka huu ni ubaya ubwela tu hakuna namna
 
Yanga mna mbwembwe sana.

Viongozi wenu wameshachachawa wewe unajifanya huna hofu.
Kwa taarifa Yako viongozi wa Simba ni mabingwa wa ku kiuka taratibu kwa kutegemea wata bebwa na kundi kubwa la Viongozi wenye vinasaba vya Simba pale Tff.
bahati mbaya Kuna makosa ya kikanuni yakifanyika ata ao viongozi Wana shindwa kuwa beba.

Walimtangaza Lamek Lawi kwenye Official page kabla usajili wake hauja kamilika Tff waka potezea,
Wakamtambulisha Valentinon Mashaka wakati Bado anamkataba na Geita Tff wakalizima juukwa juu.

Waka Mtambulisha Awesu Awesu wakati Bado anamkataba na KMC Tff waka wabeba Simba.

Bahati mbaya wame mchezesha Yusufu Kagoma ambaye Alisha ingia mkataba wa awali na Yanga na Tukumbuke mikataba yote ya awali uwa inapelekwa Tff kwa kumbukumbu ili kusije kutokea utata.

Mchezaji alikua anajua kabisa kama anafanya Double signing lakini viongozi wenu wakamwambia wewe Sign tu mengine tuachie sisi na Ligi utacheza, na aya ndio madhara yake.

Uko nyuma Simba alishawahi kunyang'anywa point 3 kwa kumchezesha Musa Mgosi na kukosa Ubingwa.
Kwasasa Simba imemchezesha mchezaji ambaye ana double signing sijui Tff watafunika kanuni au watakuja na Sarakasi zipi kuibeba Simba.
Kuna Muda Mbeleko huchanika, Ingawa Tff walipambana ku adjust ratiba ya Ligi ili Simba mechi za awali ianze na timu ambazo wachezaji wageni wanao toka nje ya Nchi hawaja kamilisha vibali na washinde ki urahisi
Bahati mbaya Simba wenyewe wametoboa mtumbwi kwa kumchezesha Kagoma.
Yaani Tff Wana changanyikiwa wa wabebe vipi!!

Tusibiri tuone.
 
Ushabiki mbaya Sana ndugu hivi unafikili Simba anaweza akapokonywa point Kwa ujinga wa Mchezaji mwenyewe na Nani alitoa kibali ili acheze na hata Shauli lililopo ni Kati ya Yanga na Mchezaji na si Simba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…