Sakata la Yusuph Kagoma kusaini timu mbili Klabu ya Simba kukatwa alama

Sakata la Yusuph Kagoma kusaini timu mbili Klabu ya Simba kukatwa alama

Wameshaanza kuingia baridi eti ndio timu kubwa hiyo,mtu hakutaki unamlazimisha
Hili ndio linalotokea hata kumruhusu kijana akapate maisha Mazuri wydad,ingekua simba hili na mchezaji mwenyewe akiwa na utayari wangekwisha fanya biashara lkn watamkomoa mtoto Mzize na kukosa fursa na ukipita hii Mzize asitegemee muujiza wakupata offer tena it happens only once in life time
 
Kwaiyo kama wamelalamika Awana haki ya kusikilizwa? Au mlitakaje labda? Kama wameona mchezaji kakiuka Sheria za Mpira lazima walalamike kwanini waache? Mamlaka za Mpira ndizo zitaamua kama wako sahihi ama lah na sio kuwaelekeza wafuate matakwa ya mtu kwa manufaa yake, uyo dogo ni mtu mzima na anayo menejiment yake walifanya vile kusaini sehemu mbili kwa sababu zipi?
Ndiyo, wana haki ya kusikilizwa 👨‍⚖️
 
Mbona mnalazimisha mambo? Wao timu husika walisema wanaijua Simba na Simba ndo ilisign na Kagoma...
Eti wapokwe point 6 point 6 ya mafwi....
Usikurupuke ukatumia ushabiki pasipo kuangalia facts

Huyo Kagoma kaleta mambo ya kiswahili kwenye vitu vya maana / kibiashara, amesaini mkataba Yanga kabla hajasaini team yako.

Haya mambo kuyachekea ndio yanatuharibia mpira na yataendelea kila leo. Busara naamini itatumika tu kusolve hili.

Na nakazia, point waachiwe wasijeleta visingizio mwisho wa msimu
 
Mbumbumbu bakini na points zenu hazikatwi, japo kikanuni mnapaswa kukatwa.
Sisi tunaitaka kagoma atulipe mil 500 na agombee radhi mashabiki wa Yanga kupitoa Yanga app basi
 
Hili ndio linalotokea hata kumruhusu kijana akapate maisha Mazuri wydad,ingekua simba hili na mchezaji mwenyewe akiwa na utayari wangekwisha fanya biashara lkn watamkomoa mtoto Mzize na kukosa fursa na ukipita hii Mzize asitegemee muujiza wakupata offer tena it happens only once in life time
Wana mambo ya ajabu sana hawa watu
 
Muwe mnaacha mihemko ya kijinga, kwaiyo kama kamati ya Sheria na hadhi za wachezaji wameona tatizo wangeacha tu wakakaa kimya? Uyo mchezaji inawezekana kweli alisaini pande zote na ndio maana suala lake limekuwa gumu, pia ni kwanini Simba walimchezesha mchezaji ambae bado wanajua usajili wake una matatizo?
Sidhani kama viongozi wa yanga na kamati yenyewe Awana akili au awazijui Sheria mpaka wakomae na kagoma aiwezekani, kama alisaini kotekote basi Sheria ifate mkondo wake na sio busara ili kutoka onto kwa wachezaji wote Wenye tamaa za kipumbavu na Simba wapokwe point ambazo mchezaji alihusika kwenye mechi walizoshinda, akuna cha msalia mtume apo!
Kaka umeeleze kama mtu ambae hujaenda kama umeenda bas hujaelimika kwann nakwambia hivo hiyo kesi simba hahusiki nayo direct simba ni mtu wa 4 kwenye hiyo kesi wakwanza ni yanga,wapili ni singida ,wa3 ni TFF Ambayo ilipitisha usajili wa kagoma had TMS inasoma singida yupo simba,wachezaji wote wanaocheza simba wameidhinishwa na TFF had FIFA...
Ukiangalia kwa umakini hapa ni yanga kuumia roho waonekne wababe kwa simba sabb madai yao yanakinzana sabb mara walitaka kagoma atoke front aombe msamaha afu jammaa kawapuuza anaubonda tu nisawa na mwanamke kaolew na jamaa mwingn roho inakuuma....YANGA WAJISHIKILIE licha ya ubora wa kikosi chao lkn msimu huu simba tumekuja kivingine timu inamorali na nivijana ambao wananjaa ya mafanikio middle ya KAGOMA OKAJEPHA DEBORA JEAN CHARLES NA MBELE MUKWALA ikija kutulia inaweza zua balaa
 
Inafikirisha sana kwamba wachezaji wote waliosajiliwa na simba wazawa wana migogoro kwa nn international players hawana shida na simba yanga wana roho mbaya.
 
Hivi yanga walimsajili vipi Kagoma wakati walikuwa wamefungiwa kufanya usajili wa ndani?
TFF wanatakiwa kuwaadhibu kwa kukiuka Sheria.
 
Wanaosajili wachezaji na kuwaingiza kwenye mfumo ni nani? Sio TFF?! Walikuwa hawajui hili..
Utopolo mwaka huu mtalia sana.
 
TFF waache mambo za kizamanj waende na mfumo mpya wa FIFA wa mtu akishasajiriwa ni ngumu kuingia kwenye hiyo portal na kusajiriwa na Timu ingine Nchi nyingi wanatumia ila wakina Ndimbo hakuna kitu wanajua wao wapo kizamani tu Dunia hii ya 2024 bado mpo kwenye Saini mbili kweli?
 
Kama amesaini timu mbili akiwa na akili zake timamu sheria ifuate mkondo wake, haya mambo ya kusema busara itumike uhuni huu hautaisha.
 
Simba roho juu, huwenda waka-katwa alama ishu ya mchezaji Yusuph Kagoma kusaini Yanga kisha kuwatosa na kuibukia mitaa ya Msimbazi.
Mchambuzi na expert wa mambo ya usajili, Hans Rafael amedai kuwa Kamati ya sheria na hadhi za wachezaji, Leo asubuhi imesikiliza kesi ya kiungo wa Simba Yusuph Kagoma, na kuamuru mchezaji huyo asimame haraka kuitumikia klabu hiyo.

Yanga wao wamethibitisha kuwa hawajamsamehe Kagoma, na wanataka haki ifuatwe.

Pia Yanga wanashinikiza Simba wapokwe pointi sita za ligi ambazo walizipata kwa kumtumia mchezaji batili (Kagoma) kwenye mechi dhidi ya Tabora na Fountain Gate.

Sakata hili pia lilimuibua mdau wa michezo na Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba na kuzungumza uhalisia wa namna anvyofahamu sakata hili la Kagoma kusaini pande zote mbili.

Swali la kujiuliza aliwezaje kucheza mechi kama usajili wake ulikuwa na utata kuitumikia Simba SC?

Soma ==>Mwigulu awaomba viongozi wa Yanga wapotezee suala la Kagoma ili aweze kucheza Simba
Mchezaji anayeidhinishwa na TFF ndiye anayeruhusiwa kutumika katika michuano rasmi, kama TFF ilivyokuwa haikumuidhinisha Awesu kwenye Charity Shield na hakutumika.

Hivyo, Kagoma alicheza kwa sababu TFF ilimwidhinisha kucheza Simba msimu huu, kwa hiyo suala la kukatwa points kwa mechi alizocheza halipo kabisa na halitatokea.

Ova
 
Taratibu ,kanuni na Sheria za usajili lazima zifuatwe,tukiruhusu haya ya KAGOMA yatajirudia Tena Yale ya FEI NA DUBE .Kama Simba amekiuka taratibu za usajili adhabu ifuate juu yake pia KAGOMA aadhibiwe ili kuweka fundisho kwa timu na wachezaji wengine wajao wenye Tamaa.
 
Back
Top Bottom