Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Sakata la Zumaridi na namna alivyokamatwa na polisi ni kichefuchefu, sheria haikuzingatiwa

Wenyewe wanataka wapigaji kama kina Mwam anawaambie kondoo wajimalize kila kitu,kondoo wanaanza kuhaha jinsi ya? kufika chamanzi yeye anasepa na V8 lake.... Eti wanadai ile ni usafirishaji haramu hakika haaingii akilini
😂😂😂 figisu tu anafanyiwa hakuna lolote hapo, wakimhukumu huyo mama basi wanatakiwa kuyahukumu makanisa yote ya wachumia tumbo.
 
😂😂😂 figisu tu anafanyiwa hakuna lolote hapo, wakimhukumu huyo mama basi wanatakiwa kuyahukumu makanisa yote ya wachumia tumbo.
Na Mimi Niko na mawazo kama yako.. Zumaridi ni mpigaji kama wenzie sasa kwa Mimi yeye awe mbuzi wakafara??
 
Ila huu uzi ndo unaweza jua akili na fikra za wa TZ walio wengi,. Kwakweli tuna safari ndefu mno khaaah. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
😂😂😂 figisu tu anafanyiwa hakuna lolote hapo, wakimhukumu huyo mama basi wanatakiwa kuyahukumu makanisa yote ya wachumia tumbo.
Kuna watu ndo wananielewa Leo kwamba Zuma anakosewa sana ....
 
Mhalifu hawi mhalifu hadi pale itakapothibitika!

Sakata la mfalme Zumaridi (Kiongozi wa kanisa la Zumaridi huko Mwanza) Linaacha midomo wazi kwa wapenda haki na utii wa sheria!

Sipo hapa kumtetea Mfalme Zumaridi, Bali nashangaa namna ya uharamu wa ukamtaji!

Taratibu za ukamataji kwa mujibu wa sheria ziko wazi kabisa lakini mamlaka zimekuwa zikionesha kufeli Mara kwa Mara kutekeleza sheria hiyo jambo ambalo limekuwa likitweza utu wa watu wasio na hatia.

MFANO! mambo kama haya yalitokea huko mtwara hadi kufedhehesha uongozi wa polisi ambayo yalianza hihivi kwa kufumbafumba mambo,

Mfano 2. Ni huko ARUSHA Kuna taarifa ya askali mzalendo kulalamika kutaka kuuwawa na polisi wenzake kwa mambo Yale Yale kama ya mtwara na serikali iko kimya.

SASA NI HILI SAKATA LA TATU LINALOTIA KICHEFCHEFU

Ni TUKIO LA zumalidi Siku ya kwanza inaripotiwa kwamba polisi waliruka ukuta/geti ili kuingia kwa Zumalidi! Kitendo hiki kilitakiwa kulaaniwa na kila mtu! (Waliruka kwa Zumalidi kesho wataruka kwako)

Kama kulikuwa na ulazima wa kufika pale kwanini hawakufuata utaratibu wa upekuzi unavyotaka? Kwanini hawa kumshirikisha mwenyekiti wa mtaa/mjumbe? Kwanini waliruka ukuta kama jambazi! (VIPI KAMA ZUMARIDI ANGEJIBU MASHAMBULIZI KWA KUFYATUA RISASI KWA POLISI ALIYEVAA KIRAIA ALIPORUKA UKUTA?) Ina maana wangejibu kwamba walikuwa kwenye mapambano na majambazi au?

Kwa utaratibu walio utumia polisi hauna tofauti na utarabu wa kijambazi! Na hili linachangia sana siku hizi RAIA kutokutofautisha kati ya jambazi na polisi.

Tukiachana na mbinu ya ukamataji!

Riport ya polisi ina ukakasi mkubwa juu ya mtuhumiwa Zumaridi!

Kosa walilo utaarifu Umma kwamba anasafilisha BINADAMU 149, kosa hilo Linatia aibu nyingine!

Hivi tangu lini watu wanaokusanyika kusali pamoja imekuwa kosa la jinai?

Mbona jumuiya na taasisi kibao tunawaona wanakusanyika na kukesha na haijawahi kutajwa kuwa ni kosa?

Zumalidi kasafirisha binadamu kutoka wapi kwenda wapi kwa lengo gani? Kuna jinai gani pale?

Hapo taifa juzi wakatoliki walikusanyika mbona haikutamkwa kuwa ni usafirishaji wa binadamu?

Kina mwingira na wachungaji kibao Tanzania kila kutwa wanakusanya watu na haisemwi ni usafirishaji,

INAKUWAJE JAMBO LILE LILE LIWE HALALI KWA MWAMPOSA LAKINI LIWE HARAMU KWA ZUMARIDI?

Mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni! Nawashauri TAKUKURU WAINGILIE KATI!
Haiwezekani sheria zipo wazi, kwanini zisingefuatwa kama kweli ZUMALIDI anamakosa makubwa hivyo!

Mimi kwa utashi wangu nahisi sakata la Zumaridi lina maslahi binafisi!

TUKIRUHUSU HAYA YA UKIUKWAJI WA SHERIA HAKUNA ATAKAYEBAKI SALAMA!

Itakuwa mtu akikosana na polisi wanakuja kuluka ukuta! Na majambazi nao watatumia mwanya huohuo kufanya uharifu!
Wazee wa PGO kazini! Wala haishangazi maana hawajaanza leo. Intelijensia labda iliwataka waruke ukuta kama ambavyo huwa inawaambia uharamu wa mikutano ya wapinzani
 
😂😂😂 figisu tu anafanyiwa hakuna lolote hapo, wakimhukumu huyo mama basi wanatakiwa kuyahukumu makanisa yote ya wachumia tumbo.
Nasikia wamemwambia upelelezi bado sasa walimkamata na kumpiga kwa kosa gani, kama hawajakamilisha
 
Nasikia wamemwambia upelelezi bado sasa walimkamata na kumpiga kwa kosa gani, kama hawajakamilisha
Hii nchi ni ya watu wa ovyo sana wanamtesa dada wa watu bila sababu, wamempiga kama jambazi, wachungaji na manabii wauongo wakiachwa wakiendelea kutapeli wananchi.
 
Ila huu uzi ndo unaweza jua akili na fikra za wa TZ walio wengi,. Kwakweli tuna safari ndefu mno khaaah. [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Niliwaambia hakuna kesi pale
 
Hii nchi ni ya watu wa ovyo sana wanamtesa dada wa watu bila sababu, wamempiga kama jambazi, wachungaji na manabii wauongo wakiachwa wakiendelea kutapeli wananchi.
Tulisema mapema hakuna cha maana ilikuwa kujisafisha baada ya kuruka ukuta kiharamia
 
Yule mama wamemuonea bure, Hakuna kesi pale. Mungu ni kamilifu wala hajahitaji msaada wa mwanadamu ampiganie. Hakuna kesi pale, alichofanya ndicho waganga wa kienyeji , mitume na manabii wa uongo ndicho wanavyofanya KILA siku. Kumkamata yeye pekee na kuacha kuwakamata waganga wa kienyeji ni uonevu na dabo standard.
Hakuna guts ya kesi pale Hakuna ushahidi dhidi ya tuhuma ya human trafficking pale hata tu kwa wakili bush lawyers.
 
Back
Top Bottom