Salam ya Mh.Raisi Samia kufunga mwaka 2024 haina chembe ya uwajibikaji wa serikali katika kupunguza ajali barabarani

Salam ya Mh.Raisi Samia kufunga mwaka 2024 haina chembe ya uwajibikaji wa serikali katika kupunguza ajali barabarani

dmkali

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2014
Posts
11,793
Reaction score
22,552
Matatizo ya ajali barabarani tunaweza kuyaondoa haraka endapo mamlaka za serikali zitachukua hatua leo.

kama hatutabadili namna ya kufikiri itatuchukua miaka mingi sana kupunguza matatizo ya ajali Tanzania.
Takwimu alizotoa rais wakati akifunga mwaka 2024 zinaonesha ajali zilizotokea ni 1735 na katika ajali hizo watu 1715 wamepoteza maisha ndani ya mwaka mmoja!

Ajali hizo ni zile tu zilizosajiliwa katika report za polisi, zipo zingine ambazo hazijulikani, pia zipo zingine za boda boda n.k

Kwa takwimu hii maana yake ajali zilizotokea mwaka 2024 asilimia 99.9% zilighalimu maisha ya binadam!

Kwa idadi hiyo ya vifo ni sawa na wastani wa watu 5 kila siku waliokufa kwa ajali barabarani!

Ebu naomba wadau tujiulize! Ungekuwa ugonjwa wa mlipuko unaoua watu 5 kila siku serikali ingekaa kimya?

Kama ni ndiyo basi hii serikali haina huruma hata kidogo!

Rais kataja sababu kuu za ajali hizo kuwa imechangiwa na uzembe wa madereva kwa aslimia 97%

HAKUNA hata sehemu moja alipotaja uzembe wa serikali katika miundombinuu mechangia ajali hizo!

HAKUNA Hata sehemu moja kikosi cha usalama kimetajwa kwa kutokuwajibika kwa magari chakavu.

HAKUNA Hata sehemu moja TANROAD wametajwa kuwa chanzo cha ajali hizo

Kiufupi HAKUNA uwajibikaji wowote wa serikali katika report aliyoisoma ili kuondoa ajali hizo!

LAWAMA Zote wamepewa MAREHEMU Waliokufa kwenye ajali kwa uzembe wao!

Kama taifa mwaka 2025 tubadili namna kufikiri, Yamkini waliomuandalia hotuba Rais hawataki kushtua ubongo wa Rais ili atambue ukweli wa tatizo hilo kubwa huko barabarani!

Nimetembea barabaa kuu za wilaya ya ilala nikahesabu mashimo barabari yalikuwa 582

Nikatembea wilaya ya kinondoni mashimo ya barabarani yalikuwa 617

Nikatembea huko wilaya ya temeke mashimo yalikuwa 436

Nikazunguka hadi huko kigamboni, nazani huko hata ofisi za Tarula/ Tanroads zilishakufa zamani, Nimekuta mashimo katika barabara kuu yapo 876 wastani wa kila mita 200 kuna shimo!

Kilichonishangaza zaidi maeneo yote hayo wakurugenzi wanapita nakuona wanakwepa mashimo hayo

Mawaziri wanapita wanakwepa mashimo hayo

Makatibu wakuu wanapita wanayaona

Wakuu wa wilaya wanayaona

Mameneja Tanroads wanayaona lakini wapo kimya!

Wanachonishangaza zaidi mengine yachimbuliwa kama hatua ya. Awali ya kurekebishwa halafu walivyokunja pesa ya kuchimbua wakayatelekeza!

Swali kama hawakuwa na bajeti kwanini waliyafukua kuwa na hali mbaya zaidi?

Utafiti wangu pia nimebaini hakuna alama za usalama barabarani kwenye baadhi ya matuta mapya na ya zamani.

Wataalam wetu huanza kujenga kujenga kwanza tuta usiku wa manane kama wachawi pasipo kuweka alama yoyote ya kuashiria tahadhali.

Nimetembea kote hakuna hata mtaalam mmoja aliyetanguliza kujenga alama ili baadae ndipo ajenge tuta!

Wote wanajenga matuta chini ya kiwango halafu yanajengwa usiku wa manane?

Kiufupi kuendesha gari tanzania ya leo tunaongozwa na hisia na uzoefu tu.

Sheria za usalama barabarani zinaangaliwa zaidi katika kumwajibisha mtumia barabara kwa onyo na faini na siyo kumlinda mtumiaji.

Nani akamwambie ukweli Rais kwamba ajali zinazoua watu 5 kila Siku chanzo ni ubovu wa miundombinu na uzembe wa wasaidizi wake?
 
Huyo nchi ilishamshinda tangu siku anakanyaga ikulu, yeye mwenyewe aliye na mamlaka analalamika unadhani ni nani mwingine wa kufanya?

Tuombe 2025, itokee namna Hawa C+C+M wajitathmini kuleta mgombea mpya tofauti na huyu bimkubwa
 
Andiko bora kabisa la kufungua Mwaka.
Sijui nini kinaendelea ila Rais Samia yupo mbali sana....
Anakatisha tamaa sana...sijui kama kuna kutoboa..
Anyway muda utaongea...
 
Huyo nchi ilishamshinda tangu siku anakanyaga ikulu, yeye mwenyewe aliye na mamlaka analalamika unadhani ni nani mwingine wa kufanya?

Tuombe 2025, itokee namna Hawa C+C+M wajitathmini kuleta mgombea mpya tofauti na huyu bimkubwa
Yaani.kila mtu kaota sharubu
 
Andiko bora kabisa la kufungua Mwaka.
Sijui nini kinaendelea ila Rais Samia yupo mbali sana....
Anakatisha tamaa sana...sijui kama kuna kutoboa..
Anyway muda utaongea...
Utawala wetu utusaidie katika hili kuliko kujificha kwenye kichaka cha uzembe wa madereva
 
Sasa wanamsomea takwimu nani ili afanye ninj!?

Anaposema ajali nyingi zimetokea then what...kwanini hatuambiii amechukua maamuzi gani kupunguza ajali namuunga mkono mtoa mada
Sema na wewe
 
Back
Top Bottom