MAFANIKIO NA UBORA VITU SAWA, KIPIMO NI NAMBA, HAIEPUKIKI.
Ubora na mafanikio ni vitu pacha kijana embu elewa vizuri, tena mafanikio ni kipimo cha ubora fuatilia mifano dhahiri ifuatayo;
Mathalani, akitajwa mwanafunzi bora kitaaluma, basi atakae simama dhidi ya wengine ni yule aliyepiga hatua (hapa namba haiepukiki), anaweza akawa ndiye aliongoza darasani ama anafanya vizuri mtaani yaani ana mafanikio fulani na haya yanatathiminiwa kwa namba, yumkini ana fedha nyingi ama ameibua wanataaluma wengi ktk fani fulani n.k (nasisitiza hisabati na namba haziepukiki).
Ukitaja mchezaji bora, basi yumkini utaangalia idadi ya magoli na ni ishara ya mafanikio yake (namba haiepukiki).
Ukitafuta msanii bora, basi utaangalia kiasi ama idadi ya mfanikio mfano, je ana nyimbo kubwa zilizobamba yaani hit song ngapi? ama ameuza nakala ngapi? kwa wenzetu wana viwango mfano ukifikia idadi ya nakala kadhaa basi mauzo yako ama yatakuwa na hadhi ya platinum, gold n.k (namba haipekuki).
Ukitaka kulinganisha mtangazaji bora dhidi ya mwingine, ktk kutafuta nani ana kitu bora zaidi ya mwingine bila shaka utaangalia wingi wa sifa nzuri kisha utahitimisha nani bora zaidi ya mwingine na tukitaja wingi na uchache basi (namba haiepukiki).
Yatosha kusema, yawezekana hupendi namba ama huziwezi lakini haziepukiki ndo mzani wa tafiti ama hoja iliyofanyiwa tafiti inakuja na facts and figures sio maneno maneno tu.