Salama J vs Millard Ayo: Yupi ni mkali zaidi akifanya interview na msanii?

Salama J vs Millard Ayo: Yupi ni mkali zaidi akifanya interview na msanii?

Energy (vibe) + detail oriented (kitu ambacho presenters wengi hawana) = lil ommy

Sikiliza interview za lil ommy nyingi utaona flow ni ya details na mostly ni vitu mtu alipost kwenye insta au twitter account ..
Kiufupi hana diversity sana kwenye maswali na hii humfanya kuwa less flexible ndo maana akikutana na mgeni ambaye yupo nje ya entertainment industry huwa anastruggle sana kuendana nao

Inshort lil ommy hana same weight na salama
ni kweli kabisa,hapa umechambua vizuri sana
 
Halafu usisahau kuwa lil ommy na millard ni vitu viwili tofauti...

Millard ana utangazaji wake upo very calm ambao unaendana na content pamoja na personality yake. Hii inamfanya kusikilizwa na rika karibia zote

Lil ommy utangazaji wake una vibe na upo relevant zaidi kwa rika la vijana maana ndo content wanazopenda

Hapo ushajua mshindi nani japo lil ommy namkubali maana kuwin audience kwenye era ya millard .alifanya kazi
Lil Ommy tukimpambanisha na DJ Fetty unasemaje kuhusu hilo? atakua kapata mtu sahihi wa kushndanishwa nae?
 
Mkuu lil ommy ni something else , ana radha yake ya maswali tofauti kabisa na watangazaji wengine. Sio kwamba amemzidi salama, hapana.. ila amekuja kitofauti sana.


Sent using Jamii Forums mobile app
Mzazi anaweza akakukuta unasikiliza redio akitangaza salama au millard akakuacha,ila akikukuta unamsikiliza LIL OMMY redio itazimwa hapo hapo utaambiwa ondoka kafanye mambo mengine,unaweza nisaidia kuniambia ni kwann redio haikuzimwa wakati nikiwaskiliza millard na salama ila LIL OMMY redio inazimwa?
 
MAFANIKIO NA UBORA VITU SAWA, KIPIMO NI NAMBA, HAIEPUKIKI.


Ubora na mafanikio ni vitu pacha kijana embu elewa vizuri, tena mafanikio ni kipimo cha ubora fuatilia mifano dhahiri ifuatayo;

Mathalani, akitajwa mwanafunzi bora kitaaluma, basi atakae simama dhidi ya wengine ni yule aliyepiga hatua (hapa namba haiepukiki), anaweza akawa ndiye aliongoza darasani ama anafanya vizuri mtaani yaani ana mafanikio fulani na haya yanatathiminiwa kwa namba, yumkini ana fedha nyingi ama ameibua wanataaluma wengi ktk fani fulani n.k (nasisitiza hisabati na namba haziepukiki).

Ukitaja mchezaji bora, basi yumkini utaangalia idadi ya magoli na ni ishara ya mafanikio yake (namba haiepukiki).

Ukitafuta msanii bora, basi utaangalia kiasi ama idadi ya mfanikio mfano, je ana nyimbo kubwa zilizobamba yaani hit song ngapi? ama ameuza nakala ngapi? kwa wenzetu wana viwango mfano ukifikia idadi ya nakala kadhaa basi mauzo yako ama yatakuwa na hadhi ya platinum, gold n.k (namba haipekuki).

Ukitaka kulinganisha mtangazaji bora dhidi ya mwingine, ktk kutafuta nani ana kitu bora zaidi ya mwingine bila shaka utaangalia wingi wa sifa nzuri kisha utahitimisha nani bora zaidi ya mwingine na tukitaja wingi na uchache basi (namba haiepukiki).

Yatosha kusema, yawezekana hupendi namba ama huziwezi lakini haziepukiki ndo mzani wa tafiti ama hoja iliyofanyiwa tafiti inakuja na facts and figures sio maneno maneno tu.

Sijacomment kuegemea preferences zangu binafsi ila UHALISIA

Pia kama unadhani numbers ndio kila kitu katika ubora wa kitu then hujui kitu kinaitwa marketing, branding and promotion..

Makampuni ya mitandao ya simu yaliishit Nigeria kwa kuangalia data za kiwango cha umaskini ila Mnet waliangalia consumers pattern which is qualitative na wakafanya investment ambayo imewafikisha mbali...

Hayo mambo ya numbers ni assurance katika maamuzi ila sio final
 
Salama J all day everyday....Ana taste flani hivi ya tofauti ukiongezea na kale kalafudhi Cha Zanzibar...
She knows how to the interview lovely and lively
 
Kwangu Salama ni best kabisa na bado sijaona Wakumfananisha nae, She is charismatic and talented, yuko well organised and focused, Millard is overrated
 
Masoud Kipanya nae Yuko Vizuri Kwenye interview na wanasiasa, nakumbuka Prof. Lipumba alibanwa mbavu hadi Kupumua halishindwa. Kila wakati anaomba Maji.. Ilikuwa issue ile Mgogoro wake na Mwalim seif kuhusu kujitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Sana sana huyo jamaa ni Yupo makini? Ana elimu gani masoud yupo updated sana
 
Masoud Kipanya nae Yuko Vizuri Kwenye interview na wanasiasa, nakumbuka Prof. Lipumba alibanwa mbavu hadi Kupumua halishindwa. Kila wakati anaomba Maji.. Ilikuwa issue ile Mgogoro wake na Mwalim seif kuhusu kujitoa

Sent using Jamii Forums mobile app
Ingawa umetoka nje ya mada lakini nakuunga mkono, prof aliminywa hadi nikaanza kupata mashaka na uprof wake, zaidi na zaidi nikaona prof anafanya wasomi wa kiislam waonekane hovyo nashukuru prof Assad akatuokoa
 
Back
Top Bottom