Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari


HUU SASA ndo uzalendo
 
Mleta mada asante sana. Kwa sasa keep low profile huku ukifuatilia kinachoendelea. Polepole kasema mambo manne ambayo wahuni wanaweza kukufanyia. Mleta mada bado tunakuhitaji. Tafadhali zingatia ushauri wangu.
 
Kati ya idara hovyo za serikali uhamiaji ni nambari moja.hiyo idara imeoza sana.wakubwa wengi sio raia wa nchi hii kwahiyo wanafaidika na udhaifu wa uhamiaji.
 
Duh! Shukurani sana kabisa!

Hili lifanyiwe kazi na mamlaka husika
 
Huyo mama kabebwa na gender tu hamna kitu pale, pia Magu alipenda watu ndio mzee yaani nyuma geuka tembea watu wa kupokea amri
 
Sijasoma yote Ila wewe jamaa inaonekana ni mzalendo kwerii kweriii.. kuna sehemu nilipita huko Kagera , wanyarwanda wamepata NIDA kibaoo, na wanajitambilisha kuwa wao ni watz wa kuzaliwa
True ni mzalendo ni nadra Sana kwa mtza kumripoti mgeni haramu sehemu husika labda tu kama wanagombea interest mfano wanawake, fitina za biashara nk.
 
Hongera mkuu kwa kuumizwa na utendaji wa uhamiaji! Mimi binafsi ningependa kamishna wa uhamiaji nchini APUMZISHWE! Naona kama anapwaya sana yule Madam! Mambo ya rushwa uhamiaji ni kama wimbo maarufu miaka yote.
 
Kati ya idara hovyo za serikali uhamiaji ni nambari moja.hiyo idara imeoza sana.wakubwa wengi sio raia wa nchi hii kwahiyo wanafaidika na udhaifu wa uhamiaji.
Yule mama haiwezi ile idara anachojua ni kusimamisha na kufukuza watumishi na sio kufanya maboresho au kutatua changamoto.
Alifukuza watoto wa watu 15 bila huruma eti kisa wapewa hela ya soda, sasa abiria vichenji vidogo elf 5 elf 10 anazipeleka wapi hali ategemei kurudi tena Bongo wala nchini kwake Hakuna bureau ya kubadili shilingi, mtu kapanda tax chenji imebaki, karidhika na huduma kaamua utakunywa soda chenji hio sirudi Bongo pia hata nikirudi nayo kwetu ni useless, wivu unamfukuza Kazi eti kisa kapewa soda bila kujali gharama ulizotumia kumtrain, mswahili hana roho mbaya sana akipata madaraka.

Ukimfukuza mtu Kazi haimaaishi utapewa mishahara yake.
 
Una lengo jema ila chukua tahadhari, usijaribu kuweka wazi your true id, waovu ni wengi kuliko wema na wapo kila pahala mpaka ndani ya nyumba za ibada.Rejea kilichompata amina etc.
 
Hongera mkuu kwa kuumizwa na utendaji wa uhamiaji! Mimi binafsi ningependa kamishna wa uhamiaji nchini APUMZISHWE! Naona kama anapwaya sana yule Madam! Mambo ya rushwa uhamiaji ni kama wimbo maarufu miaka yote
True kuwa na phd sio kuweza uongozi, uongozi ni inborn character, uongozi yafaa anapewa mtu anaeijua taasisi kama ni Waziri wa elimu yafaa aliyepanda madaraja ya ualimu so ni rahisi kujua maboresho ni yepi.
 
Hongera mkuu kwa kuumizwa na utendaji wa uhamiaji! Mimi binafsi ningependa kamishna wa uhamiaji nchini APUMZISHWE! Naona kama anapwaya sana yule Madam! Mambo ya rushwa uhamiaji ni kama wimbo maarufu miaka yote
Kiongozi rushwa haiwezi kuisha hata siku moja yeyote utakayweka hata ukiwekwa wewe. Kinachowezekana ni kupunguza tu na kama una ushauri namna ya kupunguza hiyo rushwa unaweza kutoa.
 
True kuwa na phd sio kuweza uongozi, uongozi ni inborn character, uongozi yafaa anapewa mtu anaeijua taasisi kama ni Waziri wa elimu yafaa aliyepanda madaraja ya ualimu so ni rahisi kujua maboresho ni yepi.
Sometime leaders are made and not born
 
Sisi kama taifa tunaelekea wapi, yaani unakuta passport ya Tanzania inauzwa kwa thamani ya bucket ya windhoek..

Mfumo ujitathiminj kwa hili na watendaji wale wakumbuke kile kiapo walichokula wakati wanakabidhiwa zile identity, the same goes to vipenyo wote ambao wako hapo Uhamiaji.
 
Hongera mkuu kwa kuumizwa na utendaji wa uhamiaji! Mimi binafsi ningependa kamishna wa uhamiaji nchini APUMZISHWE! Naona kama anapwaya sana yule Madam! Mambo ya rushwa uhamiaji ni kama wimbo maarufu miaka yote
Wanawake wanalindana hata kama ni dhaifu ukimbilia jenda.
 
Uhamiaji rushwa nje nje Hadi unashangaa tuko serious, Yani ukitaka passport ni hela yako tu, tena wageni huwa rahisi ukiwa na hela
 
Naomba kueleza lengo la taarifa hii

1. Nimeonyesha namna Mawakili na wanadheria wanavyoweza kuhatarisha usalama wa nchi Kwa kutotambua thamani ya mihuri waliyopewa. Mfano affidavit inagharamiwa elfu kumi au ishirini na 100,000+ kwenye firm ambazo Zina hadhi ya juu. Shilingi elfu kumi ya kiapo imekuwa ikitumiwa vibaya na Mawakili wengi binafsi na hata waliopo Serikalini, Mawakili wanashawishi wamtengenezee kiapo Mteja akiwepo au asiwepo. Nitato mfano eneo hili, baba zetu na ndugu zetu wapo vijijini lakini huku mjini kuna watu wanaghushi signature zao na kutumia majina yao kutengeneza viapo bila wao kujua. Huu ni uhalifu unaofanywa na wanasheria na hapa ndipo hizi affidavit za wageni wasio watanzania zinapotolewa. Mkenya anatafuta affidavit kama requirement ya kupata pasipoti au kadi ya NIDA, hivyo niombe awali UHAMIAJI waangalie umuhimu wa viapo na uhalali wa viapo wanavyopokea. Pili maongeze mahojiano na wateja.

2. Eneo la pili nilitaka kumweleza Kamishna Mkuu wa Uhamiaji kwamba Wapo viongoz wakubwa wanatumia vibaya madaraka na mishahara yao kutoa huduma. Badala wasimamie haki wamekuwa wepesi Sana kusikiliza laghai za wanasheria na mawakala nakutoa maelekezo yenye madhara kwenye hizo huduma zao. Mwanasheria anaingia mkataba wa Milioni let say ishirini kumtetea Mteja, then akiona kesi Katika ngazi ya chini Ina ugumu anakwenda kupakazia wakubwa kwamba Mteja wake anaoneo na maneno mengine, badala wakubwa wasimamie haki wanapindisha haki na hapa ndipo zinapopitia hizi pasipoti za wageni. Lakini pia Kuna wakati unakua engaged na Mteja kwenye kesi, unabaini mapungufu na unatamani kuisaidia Jamhuri mara Mteja anarudi kwako kwamba ameshamalizana na mkubwa na mkataba wenu unafungwa. Ukifuatilia unagundua a lot of money zimepitia mikononi mwa mtu wa Kati na wageni wamerejeshewa hati zao. Hapa sijui Hawa wakubwa wanafanya kwa upofu Gani.

3. Nimeleta Uzi huu kuwaomba watanzania tuulinde Utanzania wetu, naamini wapo watu wanachukizwa sisi kusema huu ukweli na niviongozi wakubwa ila ninachoomba kuwaeleza ni kwamba Hawa wageni wakiingilia soko la ajira, wakiingia magaidi, wakiingia watu wenye uchu na madaraka tukawapa nchi, wakijaa nchini wataanza kutuletea machafuko yaliyotokea Libya, watatuletea kubaguana kama south Afrika na kwingine. Wakati tunapigana Hawa wanaokula Rushwa Leo watakuwa wamestaafu wapo wamewekewa ulinzi makwao wanakula pensheni au wamekufa. Hivyo kwenye ya uadilifu na uraia wetu tusikubali kurudi nyuma, fedha tuchukue lakini tuwachome Viongozi wanatoa huduma Kwa wageni

4. Leo ukienda NIDA ukafuatili Kwa miezi sita wametoa vitambulisho kiasi Gani vya watu wenye rangi, wenye asili ya Mataifa ya nje utabaini ni wengi na walipewa huduma Kwa muda mfupi Sana lakini qapo Watanzania Wana miaka mitatu wanatumia namba. Kwanini Hawa watu wanapewa haraka nikwa sababu Hawana muda wakupoteza wanataka Pasipoti wavuke waende au wakwepe kusumbuliwa na dola

Mwisho; endapo tutachukilia Uzi huu kuwalaumu Uhamiaji tutakuwa tunakosea. Tatizo ni la Kitaifa kwa sababu Hawa watu wanasaidiwa na sisi wasomi na wasio soma. Wanakarimiwa na sisi na wanahudumiwa na maafisa wa serikali ambao ni watoto wetu. Tusaidie wageni wapokonywe pasipoti Taifa Liwe salama, tusaidie NIDA wafute vitambulisho Taifa Liwe salama.
Lakini pia tukumbuke serikali inataka uwe na kadi ya NIDA upate line ya simu, niambieni ni mgeni Gani unayemfahamu Kijiji au mjini Hana simu? Hiyo line kasajili Kwa namba zipi za NiDA? Tulione kama bomu na tunapolalamika ajira may be ajira nyingi wameshika wao. Tuanze kuchujana

Katika kuliangalia kisheria utabaini sheria ya Uhamiaji imekaa kuvutia wageni wahalifu, kama mtu anaweza kutoa Milioni ishirini kuweka wakili au kutoa Rushwa asishtakiwe au asichunguzwe atashindwaje kulipa fine laki Tano mahakamani? Kesi za Uhamiaji ukienda mahakamani unaenda na laki Tano unamaliza, lakini sheria ya pasipoti fine laki mbili sijui Hawa watu wanaiona pasipoti ya Tanzania ni kama hati isiyo na hadhi? Mtu adanganye apate pasipoti akose laki mbili?

Natamani watokee watu makini wachambue tatizo la uraia wa Tanzania kiusalama ikiwezekana ukikutwa na pasipoti kinyume Cha sheria iwe lazima kufikishwa mahakamani na huku iwe kifungo hata miaka 30 na viongozi wa Uhamiaji wasipewe Uhuru wakufanya administration procedure kama hizi zakutoa pasipoti ndogo au kufukuza. Mgeni akasote jela kwanza alime ndipo arejeshwe kwao utaona kama huu ujinga wakuweka Mawakili wakatetee usichunguzwe uraia kama utaendelea. Lakini pia itawasaidia Mawakili wa Tanzania kulipwa fedha nzito ambazo zitaendeleza uchumi wetu.

Tujadili bila kuwaona Uhamiaji kama tatizo, wanatekeleza wajibu wao ambao sisi pia ni wajibu wetu. Umetimiza wajibu wako? Tuwafichue Hawa wahuni wanaotaka kuliteka Taifa letu baada yakuvurugana kwao
 
Ukweli ni kwamba wahamiaji haramu huwa wa mwanzo kabisa kutafuta passport, vitambulisho vya taifa, ukaribu na viongozi , hati za umiliki wa ardhi na hata uongozi (zaidi sana kupitia chama tawala)

Hali hii ikikomaa sana, huweza kudhibiti idara nyeti za serikali, kupata uwaziri na hata urais.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…