Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari

Salamu kwa Kamishna Mkuu wa Uhamiaji, Passport za Tanzania zinakimbilia mikononi mwa wageni kupitia viongozi waandamizi na askari

Passpot ya Tz inatakiwa sana na nchi nyingi za africa kwa kuwa ina free visa nchi nyingi watu wengi wanafanya uhalifu halafu wakikamatwa wanaonekana wanatoka Tz lkn kiuhalisia si Tz mzee Magu kajitahd sana kuwaondoa hawa lkn sasa wanarudi tena upyaaa....
Umeharibu ulipomtaja MAGU. Huwezi changia mada hadi ufananishe na mtu aliyekwisha rejea mbele ya Mola wake???
 
ni rahisi sana kumtambua asie mtanzania il ndo ivyo rushwa zinatembea sanaaa
 
Nyie machogo si mlijiita pan african na mko mbele kulikomboa bara zima? Sasa mbona mnalalamika waafrika wenzenu wakichukua paspoti? Au kinachowasumbua ni Waarabu wakipewa paspoti? Zanzibar kihistoria ni sehemu ya Oman, kule kuna ndugu hata mpinge vipi. Kama hamtaki vunjeni huo mnaouita muungano, ondoeni majeshi ya vamizi ili Zanzibar ijitawale na itoe paspoti zake. Zanzibar kihistoria ni chi ya kiislamu na nchi ya kiarabu. Penda msipende machogo.
 
Napingana na wote wanaodai Dr. Makakala Hana uwezi, Mimi nimuumini wa haki: sijawahi kusikia huyu Kamishna akilalamikiwa Kwa Rushwa, Kwa kutoa kauli zisizo za kiuongozi na issue za maadili. Naamini ni Moja ya viongozi waliotoa huduma awamu ya Tano bila kuathiri watu na bila kuwa Muungu mtu. Kwa wale mnaoamini awezi kusimamia napingana nanyi. Lakini ninakubali kwa taasisi yake inawatu wanaopenda rushwa na wasiojiamini apambane nao.

Kuhusu mada ya pasipoti naomba afanye yafutayo;
1. Pasipoti zote zinatolewa na mfumo wa kielekroniki na ukitaka lazima uchukuliwe vidole na picha, aangalie restricted pasipoti zimetolewa ngapi Toka waanze mfumo mpya?
2. Apate picha na taarifa za wote waliowahi kupewa hizi pasipoti
3. Aangalie kwanini walipewa restricted pasipoti
4. Je baada ya kupewa reatricted ni hatua gani zilifuata? Walichukuliwa hatua gani?
5. Ni nani aliyetoa hizo restricted?

Akijiuliza haya maswali kwanza naamini hakuna mweusi atakutwa na kadhia hii, pili yawezekana aliyetoa hizo ni mtu mmoja na hakuna hatua zilizochukuliwa badala yake atakuta baada ya muda waliopewa restricted wamepewa ten years pasipoti.

Hii itasaidia Sana kuwashtaki wageni watakaobainika na itamsaidia kuboresha utoaji huduma na kudhibiti hati hii nyeti

Jambo jingine nimeona sheria ipo kama haipo, mwizi na mdanganyifu wa pasipoti lazima ana pesa hivyo faini nadhani kwake nimchekea. Mahakama waanze kuwafunga bila faini au sheria iondoe faini Ili tukimtaja mtu anaenda kunyea debe na pesa zake.

Wakoraaaaaaaaaa; mada tamu kama bia imejaa uzalendo.
 
Pole sana Mkuu mzalendo kama ww unaweza ukaishia jela kwa keshi za kugushi kisa tu umetibua madili ya wakubwa
 
Uzi mzuri hongera chief uliyeanzisha, bila shaka atapita au watu wake wa karibu watapita humu na kufikisha ujumbe.
 
Ahsante kwa hoja ILA kama wengi wetu huwa tunalaumu tulikoangukia SIO kujikwaa,solution hapa ni LAZIMA tuanze upya kabisa,na tuanzie na watoto wanaozaliwa,mara mtoto anapozaliwa mzazi/wazazi wanampa jina na serikali PIA lazima impe jina(ID number)hii number ataishi nayo na kufa nayo,na number hii inakua kwenye system's ya nchi na ambayo inaongea nchi nzima.Mtoto huyu anapofikia 16yrs ni LAZIMA aombe id book na kitabu hiki ndicho popote anapokwenda ndio utambulisho wake,anapoamua kuomba passport unahitaji ID book/card only,immigration officer akipachi id number yako informations zako zote zinakuwepo pale,within 5working day's unapewa passport yako,kinyume cha hapa ni utapeli na tutalalama sana.Happy new year!!
Hili wazo hata mimi huwa naliwaza sana,tusingekuwa na kesi za watumishi hewa wala nini kila kitu kinakuwa hewani,
Maana hata sasa kujua huyu mtu ashawahi kukamatwa na polisi ni ngumu sana labda awepo msamaria mwema ajue atoe taarifa sababu vituo vya polisi havionani.!
 
Passpot ya Tz inatakiwa sana na nchi nyingi za africa kwa kuwa ina free visa nchi nyingi watu wengi wanafanya uhalifu halafu wakikamatwa wanaonekana wanatoka Tz lkn kiuhalisia si Tz mzee Magu kajitahd sana kuwaondoa hawa lkn sasa wanarudi tena upyaaa....
Siku za nyuma kidogo kuna watu walikamatwa Syria kama wapiganaji wa ISIS wakiwa na passport za Tanzania. Ikasababisha Tanzania kuwekwa kwenye kitabu cheusi cha Ugaidi Marekani. Baadaye ikaja gundulika kuwa jamaa wale walikuwa wasomali na wala hawajawahi kuishi Tanzania.
 
Haya mambo sio rahisi hivi kuyamaliza kama tunavyofikiria
Kwa Africa ni rushwa kwenda mbele
Nakumbuka miaka ya 70 nikiwa seco kuna mtu aliingia nchini akakamatwa na passport nne yes nne za nchi tofauti za Jirani ikiwamo na yetu

Cha ajabu tukamuona mitaani tena na hiyo ilikuwa miaka ya 70

Kweli huwezi kumzuia mtu kusafiri anakotaka na kama ana nia ya kuishi mahali ataishi tu huu ndio ukweli
Mipaka ilitrngenezwa tu ili kugawana utawala na sio vingine

Watu wanahama na kila kukicha kutafuta maisha na watafanya kila kitu ili waishi wanapoona pana wafaa

Uhamiaji hautaisha duniani na kila leo wapo wanaokubaliwa na wapo wanaorudishwa walikotoka
Na sio kwetu tu bali duniani kote, na kila mtu anatafuta simple life

Hakuna anaezurura kwenda kutafuta mabaya labda wale mapandikizi na hao wapo pia ila hawa unaowataja wanatafuta maisha tu

Kama wataomba kuishi na kufuata utaratibu well and good ila na nyie acheni kuwarahisishia njia kwa kupokea chochote ingawa ndio njia rahisi kwao na kwa baadhi ya watendaji

Haya mambo ya kupata passport ni rahisi duniani kama unafuata sheria na kukaa mda unaotakiwa inategemea nchi na nchi

Mungu ibariki Africa
 
Pale kkoo Kuna mtaa unaotwa Omary Nundu sijui, ktk huo mtaa Kuna wasomali wanaongea kisomali waziwazi ..bila Shaka wale sio wa Tz Wanabiashara pale, unakuta
Wamejificha ktk maduka ila wame waweka na wa Swahili
 
Siku za nyuma kidogo kuna watu walikamatwa Syria kama wapiganaji wa ISIS wakiwa na passport za Tanzania. Ikasababisha Tanzania kuwekwa kwenye kitabu cheusi cha Ugaidi Marekani. Baadaye ikaja gundulika kuwa jamaa wale walikuwa wasomali na wala hawajawahi kuishi Tanzania.
Hata Mandela na ANC wenzake wa MK ambao Nyerere aliwapa paspoti za Tanzania waliwahi kuwekwa kwenye hicho kitabu cha ugaidi Marekani. Lakini mpaka leo mnajivunia wale magaidi wa Afrika Kusini kutumia paspoti za Tanzania. Waarabu au Waislamu wakipewa paspoti za Tanzania mnapiga kelele mnaona jina la nchi linachafuliwa. Ubaguzi na udini umewajaa hamna jipya.
 
Kamishna wa uhamiaji nae kakaa sana ofisi hii nyeti harafu mpole kupitiliza!. Ni kweli uhamiaji ni rushwa kwa kwenda mbele. Watu weupe ndiyo waliojaa uhamiaji kuomba pass za tz unakuta wanaongea lugha mbali2 siyo kiswahili, lakini utakuta wanahudumiwa bila shida. Mhe.Rais wananchi tunaomba uweke nguvu ya kutosha ktk hii ofisi maana ndiyo usalama wetu. Tukianza kulipuana humu ndani sisi wakulima hatuwajui uhamiaji tunakujua wewe mwenye dhamana ya nchi.
 
Hata Mandela na ANC wenzake wa MK ambao Nyerere aliwapa paspoti za Tanzania waliwahi kuwekwa kwenye hicho kitabu cha ugaidi Marekani. Lakini mpaka leo mnajivunia wale magaidi wa Afrika Kusini kutumia paspoti za Tanzania. Waarabu au Waislamu wakipewa paspoti za Tanzania mnapiga kelele mnaona jina la nchi linachafuliwa. Ubaguzi na udini umewajaa hamna jipya.
Umetoka kilabu gani; inabidi uwaambie wakurudishe pesa yako kwani makarapusi uliyokunywa yameharibu ubongo wako.
 
Hili nakubaliana na wewe kabisa, wa Kenya na wasomali wanaongoza kupata pasport za Tanzania kirahisi, ili hali mtanzania ulihitaji pasport utaanza unaambiwa kalete cheti cha kuzaliwa cha babu na bibi yako.
Na nchi rahisi kufanya magumashi hayo Africa ni hapa kwetu tu,
Mzawa hapati passport kirahisi unaweza ukaomba Leo,ukazungushwa miaka miwili ,
Wakati wageni wanaomba kwa sim tu wakiwa nyumbani,
Na wanapata kwa muda mfupi, Uzalendo hatuna kabisa ila ubinafsi ndio umejaa
 
Umetoka kilabu gani; inabidi uwaambie wakurudishe pesa yako kwani makarapusi uliyokunywa yameharibu ubongo wako.
Vipi ukweli unauma? Sijasema uongo lakini

Yet throughout his life, Mandela had a habit of saying that he was “not a saint,” as TIME noted in his 2013 obituary. Perhaps more surprisingly from today’s perspective, many people around the world felt the same way. In fact, Mandela remained on U.S. terrorist watch lists until 2008.

 
Vipi ukweli unauma? Sijasema uongo lakini



Uliyoandika hayana uhusiano wowote na mada hii; badala yake wewe umeiweka kidini. Ndiyo maana ninaamini kuwa akili yako imeharibiwa kidogo. Wagombea uhuru kupewa diplomatic passport na serikali ya tanzania wakati huo kwa vile wasingezipata nchini mwao, haina uhusiano kabisa na wasomalia kuwa na passport za Tanzania ambazo hata haijulikani walipata kwa kigezo gani.

Halafu mandela kuwa kwenye terror list, haikuwa na uhusiano wowote na yeye kuwa na passport ya Tanzania. Mwaka juzi wapiganaji wa ISIS waliokamatwa Syria wakiwa na passport za nchi mbalimbali kulisababishwa nchi hizo ziongezwe kwenye travel ban iliyotolewa na trump januray 31 mwaka 2020; Tanzania ilikuwa ni mojawapo.
 
Back
Top Bottom